Kwa hili la mwaka mmoja wa kifo cha Magufuli, Kanisa Katoliki linapaswa kuona aibu

Kwa hili la mwaka mmoja wa kifo cha Magufuli, Kanisa Katoliki linapaswa kuona aibu

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Sitaki kuzungumzia maovu ya kisiasa aliyoyafanya kwa Taifa huyu mtu, maana hata ukurasa huu hautatosha, nataka nizungumzie tu maovu aliyowafanyia kanisa Katoliki na Makanisa Mengine, halafu leo hii wanaadhimisha mwaka mmoja tangu kifo chake

Kwanza kabisa kulikuwa na mauaji na watu kupotea kulivyoshamiri mwaka 2017 Kanisa Katoliki lilitoa waraka wa kulaani mambo hayo na kuliombea Taifa lirudi kwenye mstari, alichojibu bwana huyu ni kulikejeli Kanisa katoliki na kusema kuwa halikukemea mauaji ya Kibiti (Kitu ambacho ni uongo, Kanisa lilikemea) na hata kama halikukemea kweli ndio itafanya mauaji ya watu wale kuwa sahihi? Ni mtu muovu namna gani anayeweza kuwaza hivi? Kanisa halioni aibu kumuadhimisha mtu kama huyu?

Pili, Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kiprotestanti nao wakatoa waraka wa kukemea mauaji yaliyokuwa yameshamiri nchini kipindi kile, lakini mtu huyu alivyokuwa wa ajabu alitoa wa notisi kwa makanisa hayo kufuta waraka huo ama yatafutiwa usajili, hii ilileta sekeseke hadi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani kipindi kile Mwigulu Nchemba kuondolewa

Tatu, Askofu Kakobe, aliposema kuwa Tanzania ni nchi ya vyama vingi na vyama vyote vinapaswa kupewa nafasi, askofu huyu alitukanwa na kudhihakiwa sana na vijana wa kazi wa huyu mzee, na kunyang’anywa paspoti yake na kuambiwa sio raia wa Tanzania, haikuishia hapo askofu Kakobe alitishiwa kufilisiwa mali zake na za kanisa endapo ‘asingeunga juhudi’ . Huytu ndiye mtu Kanisa Katoliki linamuadhimisha?

Nne, Askofu Niwemugizi aliposema kudai katiba mpya sio uchochezi, mtu huyu bila chembe ya aibu alimuundia zengwe kuwa sio raia wa Tanzania na akapokjonywa paspoti, japo Askofu huyu ndio alikuwa Askofu wake tangu kabla hajawa Rais..!

Tano, Kulipokuwa na Wimbi la ugonjwa Corona, mtu huyu kwa siasa zake za kilaghai akasema Corona imeondolewa kwa maombi ya siku 3, Kanisa Katoliki ambalo linajua kuwa Mungu katupa Sayansi ya kukabiliana na majanga, likasisitiza watu kuchukua tahadhari za kisayansi na kushauri Serikali ifuate njia zilizothibitishwa Kisayansi kukabiliana na hili Janga.

Kanisa lilienda mbali na kutoa takwimu za watumishi wake kama maaskofu, mapadri, masista n.k waliokufa wengi kwa kipindi kifupi kwa dalili za ugonjwa wa Covid. Mtu huyu mnakumbuka alifanyaje?

Alikejeli vibaya viongozi wa Dini na kusema wanapotosha watu kiimani, kuna kipindi aliingia kanisani na kumkejeli padre mmoja aliyekuwa anazingatia kanuni za kujikinga na Corona. Mtu huyu leo ndio Kanisa..Au linataka kumtangaza Mtakatifuu?

Nimechagua baadhi tu ambayo yalifanyika hadharani na mtu fmfuatiliji wa siasa atayajua, ila yapo mengi sana mtu huyu aliwafanyia viongozi wa Dini kama yale ya akina Mwingira, na kukamata mapadri huko Moshi, ila niishie hapa

Najua baadhi wanaweza kuteta na kusema alikuwa kiongozi mkubwa wa nchi aliyefanya mambo makubwa hivyo lazima wamuadhimishe.

Lakini Mkapa, ambaye ni kiongozi aliyekuwa na mapungufu yake pia japo hayakufikia kiwaongo hiki, alifanya mambo makubwa sana na alipofikisha mwaka mmoja tangu kifo chake, Kanisa Katoliki halikufanya chochote
 
Sitaki kuzungumzia madhila ya kisiasa aliyoyafanya kwa Taifa huyu mtu, maana hata ukurasa huu hautatosha, nataka nizungumzie tu madhila aliyowafanyia kanisa Katoliki na Makanisa Mengine, halafu leo hii wanaadhimisha mwaka mmoja tangu kifo chake
Duuh. Kanisa kama haliwezi kusamehe mitakuwaje tofauti na mtu huyo unayemzungumzia?
 
Magufuli amevipiga vita vilivyo vyema, vita vya roho na mwendo ameumaliza.

Sasa anangojea kupewa taji ya ushindi. Na siyo yeye peke yake, bali pamoja na wateule wengine walioshinda vita.

Keep RIP our best president, JPM.
 
Sitaki kuzungumzia madhila ya kisiasa aliyoyafanya kwa Taifa huyu mtu, maana hata ukurasa huu hautatosha, nataka nizungumzie tu madhila aliyowafanyia kanisa Katoliki na Makanisa Mengine, halafu leo hii wanaadhimisha mwaka mmoja tangu kifo chake
Kaka hayo ya kuhukumu tumuachie Muumba sisi jukumu letu Nafikiri ni UPENDO.

Hata mimi na ww tunamambo yetu meusi.

#tutubu na kuamini injili.....
 
Haha! Hujui maswala ya kiuongozi wewe kaa kwa kutulia.

Unafikiri wao hawayaoni hayo lakini pamoja na hayo kwanini wameamua kufanya hivyo?

Tukianza kutaja mapungufu ya kila pande hapatakalika hapa tulia uongozwe upande huu ulipe Kodi upande huu utoe zaka wakubwa ndo wameshaamua.
 
Sitaki kuzungumzia madhila ya kisiasa aliyoyafanya kwa Taifa huyu mtu, maana hata ukurasa huu hautatosha, nataka nizungumzie tu madhila aliyowafanyia kanisa Katoliki na Makanisa Mengine, halafu leo hii wanaadhimisha mwaka mmoja tangu kifo chake
Pambana na dhambi zako kanisa halita kusaidia , na kamwe halitaona aibu na maisha yataendelea.
 
Back
Top Bottom