Kwa hili la mwaka mmoja wa kifo cha Magufuli, Kanisa Katoliki linapaswa kuona aibu

Sitaki kuzungumzia madhila ya kisiasa aliyoyafanya kwa Taifa huyu mtu, maana hata ukurasa huu hautatosha, nataka nizungumzie tu madhila aliyowafanyia kanisa Katoliki na Makanisa Mengine, halafu leo hii wanaadhimisha...
Nahisi unajadili jambo linalokuzidi uwezo. Kwani wamesema wanampa utakatifu? Hayo unayoyataja unaamini hayakuwa majukumu ya rais au ulitaka awe kama mchungaji mwema, maana elewa viongozi wa dini unaowataja kukosewa na Magu wengine ni hovyo tu!

Mtu akishapata nafasi ya kusikilizwa anajisemea hata mambo asiyoyaweza.
 
Viongozi walikuwa wa hovyo ila baada ya kumsifia wakawa wazuri?

Kakobe alikuwa mkwepa kodi na mhaniai haramu ila alipomsifia akaitwa Ikulu...

Nyie wafuasi wa huyu mfu mnavichekesho kweli
 
Viongozi walikuwa wa hovyo ila baada ya kumsifia wakawa wazuri?
Kakobe alikuwa mkwepa kodi na mhaniai haramu ila alipomsifia akaitwa Ikulu...
Nyie wafuasi wa huyu mfu mnavichekesho kweli
Mtu akiitwa ikulu ndo anakuwa mzuri? Hao wote unaowataja ni viongozi wa dini, yupi mtu wa maana? That is a hell-https://jamii.app/JFUserGuide!
 
Mtu akiitwa ikulu ndo anakuwa mzuri? Hao wote unaowataja ni viongozi wa dini, yupi mtu wa maana? That is a hell-https://jamii.app/JFUserGuide!
So ataitaje wakwepa kodi na wahamiaji haramu ikulu na kuomba ushauri wao?
 
Mimi ni moatoliki, lakini h
Uzi wako umetuhumu tu, hakuna sehemu umeweka uthibitisho, hebu tuwekee hapa ili uwe credible.
awa maaskofu wetu kwa unafiki siwawezi. Hata askofu Nyaisonga kuwa rais wa tec, hawakuzingatia vigezo vingine zaidi ya kuwa mwendazake alikuwa rafiki mkubwa wa huyu askofu.
 

Wewe umeshafanya mangapi na ukasamehewa na mzazi wako ama mkeo/mmeo?

Ukristo hauko kama wewe ulivyo.

Walipotoa walaka pengine alitubu kisirisiri. ACHA CHUKI.
 
Pia alimnyanyasa sana Fr Raymond Saba wa TEC hadi kumnyang'anya passport
 
Sisi tunaombea waliokufa.

Kama ambavyo hatuku-mind wewe ambaye hauwaombei, so you should also mind your own fucking businesses.

As long as hatujavunja sheria za nchi na za kimataifa; tuache. Pilipili usiyoila inakuwashia nini?
Kuna vijitu hapa vinajidai kumjua sana Mungu, kumbe ni akili mbovu tu inayowafanya watoe sifa. Askofu fulani bhla!-bhla!
 
Unataka Kanisa Katoliki limhukumu mtu ambaye kabla ya kifo chake alipokea Sakramenti zote na linaamini yupo Mbinguni?
Kupewa sakramenti siyo uthibitisho kuwa yuko mbinguni. Sakramenti hizo ni haki yake kama mkristo, na ni wajibu wa kanisa kuwapa sakramenti hizo wale wanaozistahili, lakini hukumu bado ni ya Mungu mwenyewe.

Nimeshuhudia kanisa hilohilo likihukumu wafu kwa kudai kwamba hakuwa amefunga ndoa, alikuwa na suria, alikuwa hashiriki jumuiya nk; wakati hapohapo likiwatunuku sakramenti hizohizo walevi na majambazi!

Kuna walakini kubwa sana katika kuadhimisha uovu na waovu.
 
Awamu hii imekosa ubunifu imebakia kumkandia magufuli tu na kurejesha watu walioshindwa kazi madarakani.

Yaani kila aliyeharibu nafasi hii anapewa ili aharibu zaidi.
 
Mungu angekuwa kama mwanadamu ambaye anatoa huduma kulingana na nafasi ya mtu,masikini wote wasingefika mbinguni, wangefika akina Magufuli na maboss wenzake.

Kipimo cha Mungu ni kilekile uwe ulikuwa Rais, ulikuwa mfalme ulikuwa tajiri kama MO, ulikuwa kapuku wa mwisho hapa duniani kipimo ni kimoja.

Kama uliishi maisha ya kutinyanga hapa duniani jehanamu ni ileile kwa kapuku wa mwisho na muheshimiwa wa kwanza, mengine yote sijui maazimisho ya kumbukumbu kwa marehemu sijui kumwombea marehemu hizo ni mbwembwe tu za mwanadamu hazisaidii chochote.

Kwani binadamu yeyote anapokata roho tu, tayari anakuwa ameshapata haki yake kulingana na maisha aliyokuwa ana yaishi akiwa duniani, wa mbinguni anakuwa tayari ameshaingia wa jehanamu tayari anakuwa ameshatinga jehanamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…