Kwa hili la panadol, Kenya inachezewa rafu na Tanzania?

nkobhe255

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2017
Posts
234
Reaction score
292
Jamani kwa kweli kwa nilichokiona leo ni mwendelezo wa hujuma zinazofanywa na serikali ya Tanzania dhidi ya bidhaa za Kenya hapa nchini.

KWANINI?

Leo nimeingia famasi flani ambayo kila nikitoka kufanya vipimo ndo huwa nachukua dawa, sasa kilichonishangaza ni kupanda ghafla kwa bei ya dawa za Kenya. Kiukweli kuna PANADOL ya Kenya na ile ya Tanzania.

Zamani ile ya Kenya iliunzwa Tsh 1000(Tablet 1 yenye vidonge 10) huku ile ya Tanzania ikiuzwa Tsh 500(Tablet 1 yenye vidonge 10). Lakini cha kishangaza ni kwamba ile ya Kenya kwa sasa ni 1500 huku ya Tanzania ni 500 ileile. Hapo wateja lazima ile ya Kenya haitapata wateja.

MASWALI
(1)Je, hiyo ya kenya kupanda kwake bei ni kwasababu imeongezwa ubora kuliko ya Tanzania?

(2)Je,ni serikali ya Tanzania iliyoamua kuongeza ushuru wa bidhaa inayotoka Kenya ili kui-promote ile ya ndani?

(3)Au kuna sababu nyingine?

Naombeni wakenya na watanzania tutoe mawazo yetu ili tujue nini chanzo, binafsi mimi sielewi na imenibidi nichukue ile ya Tanzania-Uzalendo Kwanza. Na mpaka sasa niko fresh na namshukuru mungu
 
Shilingi ya Kenya imeimarika zaidi dhidi ya shilingi ya Tz.
 
Economic strategies.........
Napita tu watakuja hapa wazee wa uchumi kuchambua vzr
 
Panadol [emoji777]
Paracetamol [emoji736]
 
Unauhakika serikali ndio imepandisha kodi au watengenezaji wamepandisha bei au uroho wa mwenye phamacy ndio kaipandisha bei?,wewe ni mtanzania au mkenya?,kama ni mtanzania na umeandika haya kuna haja ya wewe kupimwa mkojo
 
Aisee kazi kweli kweli! [emoji116] [emoji191]
 
Soma tena details kwenye box,
Nani manufacturer?
Don't u see GSK over there???

So you are talking of chemical formula/composition?

Yeye ametaja anachokisoma... Amekwambia au kwa akili yako unaona kaulizia compostion?


1. Hakuna neno Panadol?

2. Waliondika panadol hawana uelewa?

3. Kwanini wameandika hilo neno?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…