Kwa hili la panadol, Kenya inachezewa rafu na Tanzania?

Kwa hili la panadol, Kenya inachezewa rafu na Tanzania?

hii isuzu ya toyota bei yake ipo juu sana.
Kumbe nimeeleweka[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Jamani kwa kweli kwa nilichokiona leo ni mwendelezo wa hujuma zinazofanywa na serikali ya Tanzania dhidi ya bidhaa za Kenya hapa nchini.

KWANINI?

Leo nimeingia famasi flani ambayo kila nikitoka kufanya vipimo ndo huwa nachukua dawa, sasa kilichonishangaza ni kupanda ghafla kwa bei ya dawa za Kenya. Kiukweli kuna PANADOL ya Kenya na ile ya Tanzania.

Zamani ile ya Kenya iliunzwa Tsh 1000(Tablet 1 yenye vidonge 10) huku ile ya Tanzania ikiuzwa Tsh 500(Tablet 1 yenye vidonge 10). Lakini cha kishangaza ni kwamba ile ya Kenya kwa sasa ni 1500 huku ya Tanzania ni 500 ileile. Hapo wateja lazima ile ya Kenya haitapata wateja.

MASWALI
(1)Je, hiyo ya kenya kupanda kwake bei ni kwasababu imeongezwa ubora kuliko ya Tanzania?

(2)Je,ni serikali ya Tanzania iliyoamua kuongeza ushuru wa bidhaa inayotoka Kenya ili kui-promote ile ya ndani?

(3)Au kuna sababu nyingine?

Naombeni wakenya na watanzania tutoe mawazo yetu ili tujue nini chanzo, binafsi mimi sielewi na imenibidi nichukue ile ya Tanzania-Uzalendo Kwanza. Na mpaka sasa niko fresh na namshukuru mungu
hapo hujuma inaingiajew? Mwenye famasi akipandisha bei ya dawa na watu wakishindwa kununua inakuwa hasara ya nani? Bila shaka jibu unalo kwamba ni hasara ya mwenye famasi.
 
Watu mmeacha kumfahamisha vizuri mleta uzi badala yake mnaleta mabishano mpk uzi umepoteza mvuto..
 
tablet 1 yenye vidonge 10 , nini hiki sasa? Ile ni blister 1 yenye tablets 10 .
Hivi huko shuleni huwa mnaenda kujifunza ujinga?
 
Tablet 1 yenye vidonge kumi=blister pack moja yenye vidonge(tablets) kumi
 
Nyinyi mnaingiza ujuwaji pasipo kabisa

Huyu mleta uzi yuko very clear....badala ya kujibu kero yake mnaanza uzushi

Haipendezi
Mleta mada au wewe ndio ulioleta na I'd tofauti.?
 
Misconception nyingine mtaani ni kwamba;
Panadol Extra (Nyekundu) = Ya Tanzania
Panadol Advance (Blue) = Ya Kenya.
Hizi ni brand names tu, kwa hio bei mara nyingi hutofautiana. GlaxoSmithKline ambao ndio watengenezaji wa dawa hizi ni waingereza ila wana kiwanda Kenya. Waafrika tumebaki kupambana kwa ajili ya mali ya wenzetu.
 
Back
Top Bottom