Kwa hili la Serikali kushindwana kauli na hospitali binafsi kwenye kitita cha NHIF, Waziri Ummy asaidiwe kuondoka wizarani

Kwa hili la Serikali kushindwana kauli na hospitali binafsi kwenye kitita cha NHIF, Waziri Ummy asaidiwe kuondoka wizarani

Wanajukwaa ninaungana na watanzania wote kuomboleza kifo cha mzee wetu Ali Hassan Mwinyi. Familia yake ijawe na faraja na subra katika kipindi chote kigumu. Mungu ailaze roho ya Babu mahala pema peponi tena huko Firdausi.... Aaamin.

Baada ya hapo hata sioni haja ya kutoa maelezo mengi mno.
Nimesikia kupitia vyombo vya habari kwamba eti serikali imeshindwana kauli na hospitali binafsi kwenye kitita Cha NHIF
Jambo lililonishangaza nikwamba eti hospitali binafsi wameshaweka mabango ya matangazo kwamba hawapokei wagonjwa wanaotumia bima (NHIF)

Eti wagonjwa mahututi watapokelewa sio kwa zaidi ya masaa 48. Unaweza ukajiuliza maswali mengi ila mimi najiuliza na sipati picha kama itakuaje unapopewa mgonjwa mahututi alievunjika vunjika au kuraruka mwili mzima umtoe wodini umpeleke unapopajua wewe. Je hiyo inakua rufaa au kitu gani? Haya ni mauaji yasiyo mithilika,ni aibu kubwa sana kwa taifa na nimaumivu makubwa sana siotu kwa wagonjwa lakini hata kwa wanafamilia. Ninapata hiyo picha kabisa

Pamoja na mambo mengi lakini ninaweza kusema serikali imeangalia maslahi yake kuliko kuvaa jukumu la kuwatibu wananchi wake na hospitali binafsi nao wameangalia maslahi yao ambapo kimsingi bila maslahi hata kidogo hawatoweza kuendesha taasisi kwasababu wananunua madawa na kulipa mishahara.

Waziri Ummy ameshindwa mambo makubwa mawili kwenye hili.
1: Ameshindwa kuangalia changamoto ya uendeshaji wa hospitali binafsi na kufikia nao muafaka.
2: Ameshindwa kuelewa kwamba serikali ndio inajukumu la kuwatibu wananchi wake ambao ndio walipa Kodi. Aelewe MATIBABU SIO FADHILA bali ni lazima. Hapo ndio alipoona kwamba hospitali binafsi zikwee mlima wake na serikali ikwee mlima wake. Huku nikufeli kukubwa sana kwa Ummy,hii ni aibu na alama mbaya sana katika wizara hiyo. Nikirejea maneno ya hayati mzee Mwinyi ninasema kwenye kitabu chako hili nalo tutaandika. Ninarudia hata ukijosahaulisha utakumbushwa na utaandikiwa TENA KWA WINO MZITO.

Nimalizietu kwa kusema Ummy acha ngonjera wewe umalize mwendo wizarani. Pisha akili na maarifa mengine vitumike kushawishi wawekezaji binafsi kwa manufaa ya nchi.
Mh. Rais kama waziri asipoona uungwana na aibu akaendelea kushupaza shingo yake, MSAIDIE KUONDOKA WIZARANI KWANI KUSHINDWA KWAKE NIKUAHINDWA KWAKO.
Hayo ni maoni yangu
Samia anagawa vyeo si kulingana na uwezo wa mtu bali kwa vigezo vyake binafsi. Serikali hii imejaa watu wasio na sifa kuanzia yeye mwenyewe
 
Mfupa wa afya unamshinda mMarekani na hata Muingereza mwenye socialized healthcare...

Healthcare is expensive na sisi ni nchi maskini.tunataka serikali na watu wenye uwezo wa-subscidize afya kwa watu maskini. Kama ndio hvyo either tukubali kuongezewa Kodi iende kwenye huduma za kijamii pamoja na afya au tukubali 55000 kwa mwaka haitoshi tena...

Pamoja na hayo ni kweli hospitali zina-cheat mifumo ya ku-submit mafao,madaktari Wana fanya double-consultation nk... Still kiasi Cha pesa kinachopotea kwenye hayo Mambo ni kidogo sana...

Zile tozo wangefanya hata 50% iende afya ingekuwa poa sana.

Watoto wote hakuna kulipia bima.
 
Wanaoumia ni watumishi wa umma ambao wanakatwa asilimia 2 ya mshahara wao kila mwezi.
Ifike mahali watumishi wa umma wapewe option ya kuchagua mfuko wanautaka.
Watumishi wa umma!? Hii sio kweli hapa labda mtu ambaye hana kazi maalumu ndio anaweza kukwepa hilo. Wafanyabishara wamelia mara ngapi kwa kodi limbikizo, kuna kodi mpaka zinafikisha unajiuliza hii nayo imekaaje.

Ukija tozo hiyo haina mfanyakazi wa umma wala Mlala hoi
 
Hakuna Mtumishi analipa Bima 55k kwa mwaka mkuu Labda bima za Vifurushi..
Na usisahau pia Bima wanaffanya ubadhilifu na Report ya CAG ilionyesha hayo
Watu tunasahau mapema sana
View attachment 2921053
Sijakataa ubadhirifu,nnacho-argue hata hizo bilioni kadhaa ingeokolewa,bado deficit inayotakiwa ku-subscidize vifurushi vingine vya bima ni Kubwa sana..
 
Sijakataa ubadhirifu,nnacho-argue hata hizo bilioni kadhaa ingeokolewa,bado deficit inayotakiwa ku-subscidize vifurushi vingine vya bima ni Kubwa sana..
Kama kipi watumishi wote wanakatwa si chini ya 200k na sio wote wanaugua hizo pesa zao zinaenda wapi???

Kwanini iwe ni NHIF na sio Bima zingine za Afya ambazo zipo kibao kuna AAR na zingine kibao hata Hiyo SHIB (ya NSSF) Sijawahi kuisikia ikiwa na ubabaishaji kama NHIF
 
Mfupa wa afya unamshinda mMarekani na hata Muingereza mwenye socialized healthcare...

Healthcare is expensive na sisi ni nchi maskini.tunataka serikali na watu wenye uwezo wa-subscidize afya kwa watu maskini. Kama ndio hvyo either tukubali kuongezewa Kodi iende kwenye huduma za kijamii pamoja na afya au tukubali 55000 kwa mwaka haitoshi tena...

Pamoja na hayo ni kweli hospitali zina-cheat mifumo ya ku-submit mafao,madaktari Wana fanya double-consultation nk... Still kiasi Cha pesa kinachopotea kwenye hayo Mambo ni kidogo sana...
Hivi mbona nchi hii hakuna waziri, mchumi, consultant wala mbunge ambaye akihojiwa anaongelea scale ya mshahara kwamba uko irerelevant and very informal.
Hakuna scale inayoelewela ya mishahara ya watu kuanzia watu wasio na elimu mpaka wenye elimu. Its about time waziri ummy akae ale pesa yake au ajiajiri maana huwa wepesi kuwaambia vijana mjiajiri. Apumzike wizara imemshinda
 
Mtengeneza tatizo ni NHIF na ameachiwa aoneshe kiburi chake kwa hospitali tunazoziamini kutoa huduma bora.

Ukimya wa Waziri wa Afya haumtoi kwenye kuwajibika. Na seems ana hamu kuona Watanzania wanakufa kwa kukosa huduma waliyoilipia bima NHIF.

Ni busara Waziri akawapisha wenye uwezo wa kuiongoza wizara
 
Sio kama hatoshitu bali hafai tena kwenye wizara hiyo. Changamoto zake zimemshinda
 
Kama ilivyo kwa biashara za mafuta na sukari, ambako waliozihodhi wanataka faida kubwa zaidi, kuna uwezekano mkubwa hata hospitali binafsi zinamilikiwa na wakora wanaotaka faida kubwa. Nimesikiliza taatifa ya kamati ya maboresho, sioni kama serikali haikuwasiliza hospital binafsi.

Cha muhimu zaidi kitita kipya kimezingatia vigezo kadhaa katika kuamua Bei ya Kila huduma. Sasa tatizo ni nini?
 
Kwenye nchi ambayo mzazi anagoma hata kununua sare za shule za mwanae kwa kisingizio cha umaskini na unyonge ni ngumu mno kuelewa gharama zilizopo kwenye matibabu. Ummy kujiuzulu haitasaidia chochote. Waziri ni kiongozi tu wa kisiasa ila chini yake kuna watendaji ambao baadhi wana nguvu za hatari kiasi cha kumvimbia Waziri. Ninashauri Rais atumie vyombo vyake kubaini tatizo liko wapi na kuchukua hatua haraka.
Kwamfano wewe ukiwa waziri ukavimbiwa na watumishi wa chini yako ukashindwa kuwadhibiti huoni kama utakua umepofuka na umevimbiwa madaraka? Hapo Ummy hanasuki kwenye hii lawama
 
Wanasema wenye hekima Heshimu baba na mama yako...


Je mdada wa Kitanga alimheshimu mama yake mzazi?
Malipo hapa hapa ulimwenguni
Ningehitaji ufafanuzi hapo kama hutojali
 
Back
Top Bottom