Kwa hili la Serikali kushindwana kauli na hospitali binafsi kwenye kitita cha NHIF, Waziri Ummy asaidiwe kuondoka wizarani

Kwa hili la Serikali kushindwana kauli na hospitali binafsi kwenye kitita cha NHIF, Waziri Ummy asaidiwe kuondoka wizarani

Kama ilivyo kwa biashara za mafuta na sukari, ambako waliozihodhi wanataka faida kubwa zaidi, kuna uwezekano mkubwa hata hospitali binafsi zinamilikiwa na wakora wanaotaka faida kubwa. Nimesikiliza taatifa ya kamati ya maboresho, sioni kama serikali haikuwasiliza hospital binafsi.

Cha muhimu zaidi kitita kipya kimezingatia vigezo kadhaa katika kuamua Bei ya Kila huduma. Sasa tatizo ni nini?
Pamoja na yote,tatizo ni wizara hivyo wizara hapo anatajwa Ummy
 
Kwamfano wewe ukiwa waziri ukavimbiwa na watumishi wa chini yako ukashindwa kuwadhibiti huoni kama utakua umepofuka na umevimbiwa madaraka? Hapo Ummy hanasuki kwenye hii lawama
Kujiuzulu ni kulinda tu heshima ila practically kuna watu ndo hutunga na kutekeleza mambo yote ya wizara. Yaani waziri kazi yake ni ndogo ndo maana wananenepa kama viboko.
 
Kujiuzulu ni kulinda tu heshima ila practically kuna watu ndo hutunga na kutekeleza mambo yote ya wizara. Yaani waziri kazi yake ni ndogo ndo maana wananenepa kama viboko.
Yeye alinde heshima yake. Kwamaelezo yako inamaanisha amejivunjia heshima yake mwenyewe maana ndio kapeleka mapendekezo bungeni ya huo upupu unao mkaanga leo
 
Ningehitaji ufafanuzi hapo kama hutojali
Story ni ndefu, to make it short alilazimishwa na rafikize kuhudhuria msiba wa mama yake.....


Hivyo wanasema the end justfy the means
 
Watumishi wa umma!? Hii sio kweli hapa labda mtu ambaye hana kazi maalumu ndio anaweza kukwepa hilo. Wafanyabishara wamelia mara ngapi kwa kodi limbikizo, kuna kodi mpaka zinafikisha unajiuliza hii nayo imekaaje.

Ukija tozo hiyo haina mfanyakazi wa umma wala Mlala hoi
Mkuu anayebeba mzigo wa kodi na tozo sio mfanyabiashara bali ni mlaji wa mwisho yaani mimi na wewe. Malalamiko ya wafanyabiashara ni kwa ajili ya manufaa yao na sio manufaa ya wananchi. Wakipigwa kodi na tozo huwa wanazihamishia kwenye bidhaa.
 
Wanajukwaa ninaungana na watanzania wote kuomboleza kifo cha mzee wetu Ali Hassan Mwinyi. Familia yake ijawe na faraja na subra katika kipindi chote kigumu. Mungu ailaze roho ya Babu mahala pema peponi tena huko Firdausi.... Aaamin.

Baada ya hapo hata sioni haja ya kutoa maelezo mengi mno.
Nimesikia kupitia vyombo vya habari kwamba eti serikali imeshindwana kauli na hospitali binafsi kwenye kitita Cha NHIF
Jambo lililonishangaza nikwamba eti hospitali binafsi wameshaweka mabango ya matangazo kwamba hawapokei wagonjwa wanaotumia bima (NHIF)

Eti wagonjwa mahututi watapokelewa sio kwa zaidi ya masaa 48. Unaweza ukajiuliza maswali mengi ila mimi najiuliza na sipati picha kama itakuaje unapopewa mgonjwa mahututi alievunjika vunjika au kuraruka mwili mzima umtoe wodini umpeleke unapopajua wewe. Je hiyo inakua rufaa au kitu gani? Haya ni mauaji yasiyo mithilika,ni aibu kubwa sana kwa taifa na nimaumivu makubwa sana siotu kwa wagonjwa lakini hata kwa wanafamilia. Ninapata hiyo picha kabisa

Pamoja na mambo mengi lakini ninaweza kusema serikali imeangalia maslahi yake kuliko kuvaa jukumu la kuwatibu wananchi wake na hospitali binafsi nao wameangalia maslahi yao ambapo kimsingi bila maslahi hata kidogo hawatoweza kuendesha taasisi kwasababu wananunua madawa na kulipa mishahara.

Waziri Ummy ameshindwa mambo makubwa mawili kwenye hili.
1: Ameshindwa kuangalia changamoto ya uendeshaji wa hospitali binafsi na kufikia nao muafaka.

2: Ameshindwa kuelewa kwamba serikali ndio inajukumu la kuwatibu wananchi wake ambao ndio walipa Kodi.
Aelewe MATIBABU SIO FADHILA bali ni lazima. Hapo ndio alipoona kwamba hospitali binafsi zikwee mlima wake na serikali ikwee mlima wake. Huku nikufeli kukubwa sana kwa Ummy,hii ni aibu na alama mbaya sana katika wizara hiyo. Nikirejea maneno ya hayati mzee Mwinyi ninasema kwenye kitabu chako hili nalo tutaandika. Ninarudia hata ukijosahaulisha utakumbushwa na utaandikiwa TENA KWA WINO MZITO.

Nimalizietu kwa kusema Ummy acha ngonjera wewe umalize mwendo wizarani. Pisha akili na maarifa mengine vitumike kushawishi wawekezaji binafsi kwa manufaa ya nchi.

Mh. Rais kama waziri asipoona uungwana na aibu akaendelea kushupaza shingo yake, MSAIDIE KUONDOKA WIZARANI KWANI KUSHINDWA KWAKE NIKUAHINDWA KWAKO.

Hayo ni maoni yangu
Haya majitu yanayojiita viongozi katika nchi yetu yanamuongoza nani? Bima imekuwa kama anasa kwa mtanzania.yenyewe yakiugua yanakwenda London. Mungu yachukue tu maana yameshindwa kutuongoza badala yake yanatuumiza
 
Mfupa wa afya unamshinda mMarekani na hata Muingereza mwenye socialized healthcare...

Healthcare is expensive na sisi ni nchi maskini.tunataka serikali na watu wenye uwezo wa-subscidize afya kwa watu maskini. Kama ndio hvyo either tukubali kuongezewa Kodi iende kwenye huduma za kijamii pamoja na afya au tukubali 55000 kwa mwaka haitoshi tena...

Pamoja na hayo ni kweli hospitali zina-cheat mifumo ya ku-submit mafao,madaktari Wana fanya double-consultation nk... Still kiasi Cha pesa kinachopotea kwenye hayo Mambo ni kidogo sana...
Kuna hela nyingi sana inavujia pasipostahili. Hispitali binafsi wako sahihi
 
kwa mwaka mzee maana kwa Mwezi ni kama 63k na ushee hivi
Ok, kama Makato ni 2% ya basic salary, anayeweza kuchangia kiasi hicho ni mwenye mshahara wa 2.5m na zaidi kwa makadirio.
Huko serekalini wenye mishahara hiyo ni wangapi?.
 
Mkuu anayebeba mzigo wa kodi na tozo sio mfanyabiashara bali ni mlaji wa mwisho yaani mimi na wewe. Malalamiko ya wafanyabiashara ni kwa ajili ya manufaa yao na sio manufaa ya wananchi. Wakipigwa kodi na tozo huwa wanazihamishia kwenye bidhaa.
Ahsante, ila walaji ndio hao hao mfanyabiashara, mtumishi wa umma, na raia wa kawaida

Kodi zingine hazihamishiki kirahisi isipokuwa kwa kiwango kidogo ,ingekuwa hivyo basi kungekuwa na hao kubwa kati ya wafanyabiashara na watu wengine
 
Ok, kama Makato ni 2% ya basic salary, anayeweza kuchangia kiasi hicho ni mwenye mshahara wa 2.5m na zaidi kwa makadirio.
Huko serekalini wenye mishahara hiyo ni wangapi?.
SIo wengi sana but wapo Kiasi kikubwa kwa nilipo
 
Harafu ale wapi? Hajiuzuru mtu hapa na mambo yataenda hivo hivyo. Asiyetaka ahamie Burundi
Kwa hiyo Ummy yupo kwenye uwaziri sababu ya kula? Na siyo kumsaidia Raisi na wananchi kuendesha sekta ya afya kwa weledi na manufaa. Ili kulinda siha za watanzania wote!?. Mawazo mgando Kama tope la mbugani.
 
Back
Top Bottom