Kwa hili la Serikali kushindwana kauli na hospitali binafsi kwenye kitita cha NHIF, Waziri Ummy asaidiwe kuondoka wizarani

Samia anagawa vyeo si kulingana na uwezo wa mtu bali kwa vigezo vyake binafsi. Serikali hii imejaa watu wasio na sifa kuanzia yeye mwenyewe
 

Zile tozo wangefanya hata 50% iende afya ingekuwa poa sana.

Watoto wote hakuna kulipia bima.
 
Wanaoumia ni watumishi wa umma ambao wanakatwa asilimia 2 ya mshahara wao kila mwezi.
Ifike mahali watumishi wa umma wapewe option ya kuchagua mfuko wanautaka.
Watumishi wa umma!? Hii sio kweli hapa labda mtu ambaye hana kazi maalumu ndio anaweza kukwepa hilo. Wafanyabishara wamelia mara ngapi kwa kodi limbikizo, kuna kodi mpaka zinafikisha unajiuliza hii nayo imekaaje.

Ukija tozo hiyo haina mfanyakazi wa umma wala Mlala hoi
 
Hakuna Mtumishi analipa Bima 55k kwa mwaka mkuu Labda bima za Vifurushi..
Na usisahau pia Bima wanaffanya ubadhilifu na Report ya CAG ilionyesha hayo
Watu tunasahau mapema sana
View attachment 2921053
Sijakataa ubadhirifu,nnacho-argue hata hizo bilioni kadhaa ingeokolewa,bado deficit inayotakiwa ku-subscidize vifurushi vingine vya bima ni Kubwa sana..
 
Sijakataa ubadhirifu,nnacho-argue hata hizo bilioni kadhaa ingeokolewa,bado deficit inayotakiwa ku-subscidize vifurushi vingine vya bima ni Kubwa sana..
Kama kipi watumishi wote wanakatwa si chini ya 200k na sio wote wanaugua hizo pesa zao zinaenda wapi???

Kwanini iwe ni NHIF na sio Bima zingine za Afya ambazo zipo kibao kuna AAR na zingine kibao hata Hiyo SHIB (ya NSSF) Sijawahi kuisikia ikiwa na ubabaishaji kama NHIF
 
Hivi mbona nchi hii hakuna waziri, mchumi, consultant wala mbunge ambaye akihojiwa anaongelea scale ya mshahara kwamba uko irerelevant and very informal.
Hakuna scale inayoelewela ya mishahara ya watu kuanzia watu wasio na elimu mpaka wenye elimu. Its about time waziri ummy akae ale pesa yake au ajiajiri maana huwa wepesi kuwaambia vijana mjiajiri. Apumzike wizara imemshinda
 
Mtengeneza tatizo ni NHIF na ameachiwa aoneshe kiburi chake kwa hospitali tunazoziamini kutoa huduma bora.

Ukimya wa Waziri wa Afya haumtoi kwenye kuwajibika. Na seems ana hamu kuona Watanzania wanakufa kwa kukosa huduma waliyoilipia bima NHIF.

Ni busara Waziri akawapisha wenye uwezo wa kuiongoza wizara
 
Sio kama hatoshitu bali hafai tena kwenye wizara hiyo. Changamoto zake zimemshinda
 
Kama ilivyo kwa biashara za mafuta na sukari, ambako waliozihodhi wanataka faida kubwa zaidi, kuna uwezekano mkubwa hata hospitali binafsi zinamilikiwa na wakora wanaotaka faida kubwa. Nimesikiliza taatifa ya kamati ya maboresho, sioni kama serikali haikuwasiliza hospital binafsi.

Cha muhimu zaidi kitita kipya kimezingatia vigezo kadhaa katika kuamua Bei ya Kila huduma. Sasa tatizo ni nini?
 
Bora kungekuwa na bima za Afya nyingi ili kuepo na ushindani wa huduma,
Wazo zuri sana. Ila hawatakubali watakomaa kama walivokakamaa na liTANESco lao. Aibu kubwaaaa
 
Kwamfano wewe ukiwa waziri ukavimbiwa na watumishi wa chini yako ukashindwa kuwadhibiti huoni kama utakua umepofuka na umevimbiwa madaraka? Hapo Ummy hanasuki kwenye hii lawama
 
Wanasema wenye hekima Heshimu baba na mama yako...


Je mdada wa Kitanga alimheshimu mama yake mzazi?
Malipo hapa hapa ulimwenguni
Ningehitaji ufafanuzi hapo kama hutojali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…