Kwa hili suala la RC Chacha Kanda ya Ziwa tumeitisha kikao cha Dharura siku ya Jumamosi

Kwa hili suala la RC Chacha Kanda ya Ziwa tumeitisha kikao cha Dharura siku ya Jumamosi

Sodoku Myebusi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,319
Reaction score
3,004
Sisi Wayebusi tumesikitishwa sana kusikia jambo hili na tumeshirikiana na Mwenyekiti wa Wanaume wa Kanda ya Ziwa kuitisha kikao siku ya Jumamosi kujadili hili jambo ambalo bwana Chacha amelianzisha.

Wadau wengi wamepiga simu wakiwa na maswali kadhaa kuhusiana na Bwana Chacha wanaume kwa wanawake wameoneshwa kusitikishwa sana kwa kitendo hicho na kumwonea huruma Bi Sophia.

Maswali yamekuwa mengi sana. Wengi wakiulize
1. Je huyu Chacha yupo sawa kweli kweli? Au kuna shida sehemu?
2. Je huyu Chacha kweli ni Mzaliwa wa Kanda ya Zima hasa Mkoa wa Mara au kuna Uzenji ndani yake?
3. Umri na Elimu ya Chacha?
4. Je wakati anazungumza alikuwa sober?
5. Uanaume wa Chacha umekuwa kwenye maswali sana.

Kumeonekana kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa wanaume. Haikuwahi tegemewa kuwa mwanaume tena wa kanda ya Ziwa atamdhalilisha mwanamke kiasi hicho.

Sisi Wayebusi huwa tuna kazi ya kulinda wanawake wasidhurike kimwili na kihisia. Inakuaje Chacha anaamua kumdhalilisha mwanamke ambaye alionesha hisia zake kiasi hicho? Ni mara ngapi wanaume tunabembeleza penzi? Na je kama angeamua tu kumblock ingekuwa na athari gani kwake? Kwa nini kumtangaza na kumwitia polisi kumkamata kama vile kafanya kosa la jinai?

Kumeonakena kuna tatizo limeanza kuingia kanda ya Ziwa. Tatizo ambalo zamani lilikuwa linapatikana tu Mikoa ya Pwani.

Hivyo Mwenyekiti wa Wanaume wa Kanda ya Ziwa ameitisha kikao siku ya Jumamosi kitakachofanyika Jijini Dar na Mwanza kwa wakati mmoja kikirushwa hewani. Lengo ni kuzungumza na wanaume Kanda ya Ziwa. Kuwa wameanza kupatwa na nini? Wamekula maharagwe ya wapi?

Wayebusi tumealikwa na kuamua kwa moyo wa dhati kutumia nafasi hiyo kutoa darsa kwa wanaume Tanzania na Dunia nzima. Waanze kuwa wanaume kweli kweli. Waishi Kiyebusi. Mimi Msodoku nimesikitishwa sana na tukio hilo.

Zamani wanaume Kanda ya Ziwa walikuwa wanasifika kuwa na vifua. Kutunza siri na kuhifadhi mambo. Siku hizi hali inabadilika. Chacha umekaa sana na watu wa Pwani. Unadiriki kumchamba mwanamke sababu amekutaka kimapenzi? Unamchamba mbele ya media nakutaka akamatwe?

Imesikitisha zaidi kuna watu walikaa kabisa kusikiliza maisha hayo binafsi ya Chacha. Akisimulia hayo mambo kama vile anatoa elimu ya suala la kiuchumi au kiafya. Ni aibu sana
 
Huyu mkurya wa mchongo,mambo haya tulizoea kuyaona kwa wanaume WA dar,sasa huyu bwana chacha daaah!
Tumfukuze huku uanaumeni
 
Sema aliona demu ni mbovu ingekuwa pisi ya kwenda mbona angeingia line. Namhurumia binti wa watu ametumika kujenga populality ya mtu
 
Back
Top Bottom