Kuna kitu naomba ninukuhu kwanza
Yohana 14:7-11
⁷ Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.
⁸ Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
⁹ Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
¹⁰ Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.
¹¹ Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.
Kwa mjibu wa biblia inaoneaha daima yesu hakutembea mwenyewe bali mda wote alikuwa natembea na uwepo wa Mungu ndani yake. Na aliposema "Mungu wangu mbona unaniacha" haikumanisha Mungu hamuoni tena bali Mungu alijiweka pembeni ili kuacha lengo la Yesu kuja dunian litimie. Kwann alisema roho yangu naikabidhi mikononi mwako hapo sijui sasa
Mojawapo ya maeneo ambayo yanamkanganyiko wa tafsiri(Siyo biblia imejikanganya hapana bali ni sisi tu na vichwa vyetu kutotaka kutumia akili zetu kung'amua kilichomaanishwa hapo)
Hii imepelekea kuzalishwa kwa imani na nadharia tofauti tofauti juu ya Mungu na Yesu ni kitabu hiki hiki cha Yohana ambacho nadhani kama ni mkristo unayefuata mafundisho ya Yesu Kristo basi unapaswa kukisoma kwa umakini nakujaribu kukielewa kwa binafsi yako kwanza pasipo kumhusisha yeyote kukuelezea au ku-apply nadharia yeyote unayohifamu kabla.
Binafsi yangu nimekielewa namna hii;
Yesu kavaa uhusika wetu hivyo ni binadamu mwenzetu na wakati akitufundisha maandiko, alikuwa akitumia nafsi ya kwanza kujielezea kama binadamu au mtoto wa Mungu (na mara kadhaa alilisisitiza hili kuwa tu wana wa Mungu au miungu inayoishi na akuonesha kujitenga nasi) lengo likiwa ni kuhubiri Neno (habari za uzima) kwa wana wa Mungu (akijijumuisha na yeye pia)
Unapojiuliza yu wapi Mungu au anafananaje Mungu? Jibu la Yesu hapo limejitosheleza;
Unapaswa kujiuliza kwanza kuwa kama Mungu ni Roho na ndani yangu alinipulizia pumzi ya uhai (Roho yake) nikaanza kuishi (yeye ndani yako na wewe ndani yake) huku sehemu ya roho yake inayoniunda mimi ikiwa ndani yangu, je huyo Mungu wahisi kwa umbo la kimwili anafananeje?
Hivyo hapa ni sawa na Yesu kama binadamu akuambie ukiniona mimi yaani binadamu mwenzio tiyari umeshamwona Mungu kwa kuwa kila aliye hai ndani yake anaishi Mungu (mwili wenu ni hekalu langu-ndiyo maana ya kuitaji kutukuzwa kupitia mwili huo) na Mungu ni Roho.
Yesu alinukuliwa pia akisema kuhusu yeyote hatourithi ufalme wa mbinguni pasipo kupitia kwake yeye au maombi yote yaelekezwe kwake naye baba atayajibu:- Kwa maana akuna atakaye enda kwa Baba ila kupitia kwangu kwa kuwa Mimi na Baba ni wamoja. Je, hapa Yesu anamaanisha nini? Je, anamaanisha kuwa yeye ni Mungu au sawa na Mungu?
Jibu ni hapana, Yesu (hapa anamwakilisha Neno au Sauti ya Mungu hivyo anapaswa kuwasilisha agizo lilivyo pasipo kubadili au kupindisha maana) hapa ni chombo kilichotumika kuwasilisha(hivyo tusidili na mwili, nafsi au mtu) au kinywa ambacho ndani yake ndipo linapotoka NENO LA UZIMA (Maagizo ya Mungu)
Hivyo anaposema hakuna atakayeurithi ufalme wa mbingu au maombi yake kujibiwa pasipo yeye, anamaanisha kuwa pasipo sisi kukiri na kupokea Neno la Mungu anavyotuambia nakulitekeleza hamna namna yoyote yakumfikia Mungu.
Hivyo Yesu akwambii umwabudu yeye bali Mungu wako na yeye anatwambia kuwa hakuna aliye mkamilifu ila Baba peke yake na kamwe hakuja kujitukuza bali kwa mapenzi ya aliyemtuma.
Nashukuruni mpaka hapo kwa waliosoma nilichoandika nina imani kwa kiasi chake wamenufaika kidogo na kile nilichookoteza kwenye kitabu hiki cha Yohana kwa ufupi. Na pia naruhusu kurekebishwa.