Kwa hoja za Babu Tale bungeni, ninakiri kuna ulazima wa marekebisho ya Katiba kwa sifa za mtu kuwa Mbunge

Kwa hoja za Babu Tale bungeni, ninakiri kuna ulazima wa marekebisho ya Katiba kwa sifa za mtu kuwa Mbunge

Ninawasalimu kwa jina la Chama Pendwa CCM.

Ninaandika nikiwa nina hasira kali sana dhidi ya mbunge aitwae Babu Tale kutokana na hoja zake zilizokosa weledi huko bungeni wakati akichangia bajeti ya wizara inayohusika na sanaa. Huyu babu kwa kukosa weledi alitaja majina ya wasanii katika hali iliyoonyesha kabisa ni chuki dhidi ya baadhi ya wasanii wakati alipaswa kuwa mwakilishi wa wasanii wote. Ni kauli ambazo sina haja ya kuzirudia hapa maana zinatrend kwa sasa.

Ninamkumbusha Babu Tale kujua kwamba anapokuwa bungeni anakuwa mwakilishi wa watanzania wote na sio mwakilishi wa WCB wala Tiptop. Kitendo cha kumtetea Kasim Mganga na kumponda Luludiva sio cha kiungwana. Pia ninamshauri mwaka 2025 atafute kazi nyingine za kufanya kwasababu wabunge mizigo hawatarudi bungeni.

Tunapaswa kubadili katiba ili angalau bungeni wasiingie vilaza kama kina Tale na kuchafua hadhi ya bunge.
View attachment 2254936
Mbunge Babu Tale akichangia bajeti ya wizara ya utamaduni​
HAYO NI MATOKEO YA CCM KUBAKA NA KUKOJOLEA KATIBA JMT
 
Babu Tale ni Mwakilishi wa Wasafi Bungeni!!!
 
Bila kupata utaratibu wenye vigezo vinavyo eleweka ikiwemo elimu vya kupata viongozi wa Kisiasa tutarajie kuja kupata kiongozi Mkuu wa Nchi ambaye ni wa ajabu na hovyo hovyo mno. Kwa nini uongozi wa kisiasa ndio uwekewe vigezo duni vya kielimu kumpata mhusika, Kwani siasa sio ajira? Ajira yenye hadhi na mapurupuru ya Kibunge eti imewekewa kigezo cha kielimu cha kujua kusoma na kuandika huu ni mzaha wa kiwango cha juu. Tanzania kama taifa wakati nwengine tuna mizaha sana kwenye mambo ya'msingi yanayo gusa maisha watu.

Sifa ya kiongozi muhimu na muwakilishi kwenye chombo nyeti cha uwakilishi wa wananchi bunge kwa ajili ya kutungua/kupitisha sheria na kuisimamia serikali kigezo cha kielimu iwe ni kujua kusoma na kuandika. We are not serious.
Halafu dereva wa mbunge lazima awe na cheti cha kidato cha 4 akamwendeshe mwenye kujua kusoma na kuandika hata kama alijifunzia mtaa bila kuingia ktkt jengo la darasa,
 
Waache wawepo Ili historia iandikwe.

Watoto na wajukuu zetu watapata reference.

Sikumuua Magufuli, LAKINI kifo chake kilikuwa Ni mipango wa Mungu Ili Tz ipone. Vuta picha angekuwepo mpaka leo.
 
Wa kulaumiwa ni huyo mnaemuita raisi wa wanyonge....chuki zake zilisababisha ajaze watu wa hovyo bungeni....mfano yule mama aliezungumza ishu za kunyonya maziwa wanawake....
Upo sahihi, aliyewaleta wabunge wa aina hiyo ndiye wakulaumiwa.
 
Mwenzio ana mshahara wa 13m per month, pensheni ya 400+m na sifa za kuteuliwa kuwa Waziri/Waziri Mkuu muda wowote. Pia, ana diplomatic passport
 
Back
Top Bottom