Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
HOTUBA YA SAA 1 NA DAKIKA 16 YA MHE RAIS NI TIBA YA MSONGO WA MAWAZO.
Na Elius Ndabila
0768239284
Leo hotuba ya Mh Rais inaendelea kujenga matumaini mapya katika Taifa letu. Ni hotuba nzito ambayo inajiegemeza kwenye misingi ya utawala bora na yenye kuleta mawanda mapya ya fikira juu ya nguvu ya mwanamke jasiri na shupavu. Mhe Rais ametoa suluhisho la mashaka mashaka juu ya hatima ya Taifa.
Nikiwa ninaendelea kuitafakari hotuba ya Mhe Rais Mama SAMIA, ninamkumbuka mwanamke jasiri na mwenye kujidhabihu ambaye anatajwa kwenye Biblia. Mwanamke huyu ni Debora.
Debora alikuwa ni nabii wa kike aliyetumiwa na Mungu wa Israeli, Yehova, kuwajulisha watu wake mambo aliyotaka wafanye. Pia, Mungu alimtumia kusuluhisha matatizo yaliyokuwa yakiendelea miongoni mwa Waisraeli (Waamuzi 4:4, 5).
Nabii huyo wa kike Debora aliwategemeza waabudu wa Mungu kwa ujasiri. Kwa mwongozo wa Mungu, alimwamuru Baraka aliongoze jeshi la Waisraeli likapigane na Wakanaani waliokuwa wakiwakandamiza. (Waamuzi 4:6, 7) Baraka alipomwomba Debora aende naye, alikubali kwa hiari bila woga, naye akatenda kulingana na ombi lake.—Waamuzi 4:8, 9.
Baada ya kupewa ushindi mkubwa na Mungu, Debora alichangia kutunga sehemu ya wimbo ambao waliuimba pamoja na Baraka kuhusu jambo lililotokea. Katika wimbo huo, alitaja sehemu iliyotimizwa na Yaeli, mwanamke jasiri, katika kuwashinda Wakanaani.
Fundusho tunalipata katika andiko hilo ni kuwa Debora alikuwa jasiri na mwenye kujidhabihu. Aliwatia moyo watu wafanye kile kilicho sahihi machoni pa Mungu. Walipofanya hivyo, aliwapongeza kwa ukarimu kwa Mambo waliyoyatimiza.
Nimeona nitumie huyu mtumishi Debora kwa kuwa alikuwa ni mwanamke wakati huo huo Mhe Samia ni Mwanamke tena jasiri ambaye analeta matumaini pale ambapo tumaini lilififia. Na huyu Mhe Samia ndiye amebeba ndoto na matumaini ya Watanzania wote kwa sasa.
Nimesema hotoba yake inatibu msongo wa Mawazo kwa sababu zifuatazo.
Mosi, Wafanyabiashara na Wajasiliamali walipoteza matumaini juu ya biashara zao kwa kuwa TRA waligeuka Miungu watu. Leo Rais anaposimama hadharani kuwakemea na kuagiza viongozi waliochini yake kuweka mazingira rafiki ya kukusanya kodi badala ya dhuluma basi hii inawafanya watu kurudisha morali iliyokuwa imefifia. TRA imewaumiza watu wengi na tunao ndugu wengi walifunga biashara na wengine walihamisha biashara zao kwenda nchi jirani.
Pili amegusia kilio cha Watanzania juu ya bei holela za bando ambazo zilipandishwa juzi. Mhe Rais amelikemea hili kwa kuwa nalo lilikuwa ni tishio kwa vyombo vingi vya habari ambavyo wanategemea internate ili kazi zao ziwafikie walaji.
Tatu amezungumzia represent ya Walimu zaidi ya 6000 ambao walistaafu, kuacha kazi au sababu zingine. Hili kwa tafsiri rahisi vijana wetu ambao wameshasomea Uwalimu na wako mtaani watapunguzwa kwenda kuziba mapengo hayo.
Nne, Uwajibikaji wa watumishi. Amesistiza kuwa kila mtu afanye kazi mahali alipo. Amesema watakakapo fanya ziara na kuona mabango ya Jambo ambalo DC na DED wangelishughulikia basi wote atawaondoa. Ni ukweli kuwa maeneo mengi nchini hawa watu hawafanyi kazi. Wengi ni watu wa kuzunguka kata zilizo jirani na makao Makuu na hawaendi Vijijini kusikiliza kero za wananchi. Ukiona wameenda basi tambua kuna ratiba ya ugeni Mwezi huo.
Pia amezungumzia Wizara ya Mambo ya nje kuwa amemchukua huyu Mama kwa kuwa ni mbobevu kwenye eneo hilo. Wiki liliyopita niliandika juu ya Diplomasia ya kiuchumi namna ambavyo Tanzania hatujaitumia. Kunapokuwa na mahusiano strong hata Uchumi inakuwa strong.
Mhe Rais amezungumzia juu ya kuunda tume ya kuangalia namna ya kupambana na Vovid 19. Amesema ni lazima Kama Taifa tuwe na msimamo, lakini msimamo utokane na tume kwani Tanzania siyo kisiwa.
Hotuba hii tiba ya msongo wa Mawazo kwa kuwa inamgusa kila mtu. Ni hotuba ambayo imejaa lugha ya ulezi kama ilivyo ada kwa akina Mama wengi, lakini ni hotuba ambayo inasimamia misingi ya Utawala bora.
Mama Samia ninamfananisha na Debora kwa kuwa amekuja wakati ambao Watanzania walikuwa na msongo wa Mawazo, Watanzania hawakujua hatima ya Uchumi wao wa kesho kutokana na kubambikiwa kesi na kuporwa fedha zao, Watanzania hawakujua kesho yao kwa kuwa vyombo vya habari vilifungwa mtu alivyojisikia, Watanzania waliona kama kuna mahali wanakosea.
Leo anapotokea mtu anatengeneza suluhu, tunahitaji kumuunga mkono na kumuombea.