ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
- Thread starter
- #121
Na hii ni ya mda? 👇👇Hii ni muda mrefu hapo mtaa wa mahakama kuu
View: https://www.instagram.com/p/DBQbkm3iagB/?igsh=M3c2a3l2eGh4dnhu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na hii ni ya mda? 👇👇Hii ni muda mrefu hapo mtaa wa mahakama kuu
Mkoa wa Mwanza ni Kati ya Mikoa ambayo Rais Samia amewapendelea sana Kwa kuimiminia miradi lukuki tena ya mabilioni Kwa mabilioni.
Miradi hiyo imegawanyika katika mafungu Makuu 3 ambayo ni
a)Miradi ya Urithi kutoka awamu ya 5,iliyokamilika na inayoendelea.
b)Miradi Mipya iliyoanza awamu ya 6 iliyokamilika na inayoendelea.
c)Na miradi ambayo Iko Mbioni kuanza wakati wowote .
Ifuatavyo ni miradi ambayo inatekelezwa na Rais Samia Mkoani Mwanza Kwa Kila kundi.
(a)MIRADI MIPYA
1.Ujenzi wa Barabara za Lami Mitaani mradi wa TACTIC Mwanza CC na Ilemela MC km 32 eg Buhongwa-Igoma
2.Ujenzi wa Soko La Kirumba na Soko la Samaki Mkuyuni Bilioni 25.
3.Upanuzi wa Kampasi ya TIA Usagara-Mwanza ,Bilioni 8
4.Ujenzi wa Soko Kuu la Jiji la Mwanza
5.Ujenzi wa Hospitali ya Jiji gorofa 6
6.Ujenzi wa Majengo Mapya ya Gorofa Chuo Cha Ufundi na Maendeleo Misungwi.
7.Ujenzi wa Jengo jipya la Mwanza Airport na kukarabati wa uwanja kuwa wa Kimataifa
8.Ujenzi wa Jengo la Kitega Uchumi la TBA Ghana Kota gorofa 7
10.Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu Cha Ardhi Mwanza (Sengerema)
11.Ujenzi wa Barabara za Mitaani chini ya TARURA eg Kisesa-Bujora,kiyungi road nk
12.Ujenzi wa Vyumba vya madarasa na shule Mpya zikiwemo za gorofa eg Kisenga ,Igudija nk katika Wilaya zote.
13.Ujenzi wa Vituo vya Afya, Hospital za Wilaya na ununuzi wa vifaa tiba Wilaya zote za Mwanza.
14.Mradi wa Maji Ukiriguru-Sumve Wilayani Misungwi Bilioni 32.
15.Ujenzi wa Barabara ya Hungumalwa-Ngudu-Magu km 71
16.Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Rufaa Ukerewe
17.Upanuzi wa Bandari za Mwanza South sanjali na ujenzi wa vivuko vipya.
18.Ujenzi wa Chuo Cha Michezo Malya (Malya Sports Complex and Training Centre).Zaidi ya Bilioni 40.
19.Ujenzi wa Barabara ya Mabuki-Jojiro-Ngudu
20.Ujenzi wa Barabara ya Mwanza Airport -Kayenze-Nyanguge
21.Ujenzi wa Barabara ya Nansio-Rugezi
22.Ujenzi wa Barabara ya Mwanangwa-Misasi-Salawe-Solwa-Kahama km 150.
23.Ujenzi wa Barabara ya Bukokwa-Nyakalilo
24.Ujenzi wa Barabara ya Ilalila-Shibula
25.Ujenzi wa Barabara ya Sengerema -Nyehunge km 54.4 (Bilioni 73).
26.Ujenzi wa Daraja Kubwa la Simiyu lenye mita 150 pamoja na Barabara Unganishi.
27.Ujenzi wa Daraja Kubwa la Sukuma lenye urefu wa mita 70 na barabara Unganishi km 4.
media="media="instagram:C89677rNdfd"]
View: https://www.instagram.com/p/C89677rNdfd/?igsh=ZTdkNml4YTQwa2V0[/URL]
View: https://youtu.be/Aq7AGgVXaxQ?si=fb9L7WED3YEdNVdb
(b)Miradi ya Urithi
1.Ujenzi wa daraja la JPM
2.Ujenzi wa Sgr ya Mwanza-Isaka
3.Ukamilishaji wa Stendi za
Nyegezi na Nyamhongolo
4.Ukamilishaji wa mradi wa Maji Butimba
5.Ukamilishaji wa Jengo la OPD Sekou Toure gorofa 6
6.Ukarabati wa Meli kubwa ya MV Mwanza Hapa kazi tuu.
7.Ukamilishaji wa Chuo Cha Ufundi na Teknolojia DIT Mwanza Campus
8.Ukamiloshji wa Tawi la Chuo Cha Mipango Vijijini Mwanza Centre
View: https://youtu.be/n97F4rAuoPs?si=tmTMNkcjX_nX7z3r
(c)Miradi ambayo Iko Mbioni kuanza ni
-Upanuzi wa Barabara ya njia 4 kutoka Mwanza CBD Hadi JPM bridge (lot 1 km 25),CBD-Usagara Jnct km 25.
-Ujenzi wa mgodi mkubwa wa Madini ya Dhahabu Nyanzaga
-Upanuzi wa Barabara kuu ya Musoma kuwa njia 4
-Upanuzi wa Barabara kuwa njia 4 kutoka Usagara-Shinyanga Border
-Kamanga-Katunguru-Sengerema km 3.
-Upanuzi kuwa njia 4 wa Barabara ya Mwanza-Nyanguge km 35.
-Mwanza Airport-Igombe-Kayenze-Nyanguge km 46
-Mkuyuni-Mahina-Nyakato km 10
-Nyakato(VETA)-Buswelu-Mhonze km 18.
View attachment 3127876
My Take
Hiyo ni Baadhi tuu ya miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Samia huko Mwanza.
Kiufupi Samia ameiheshimisha Mwanza kushinda Shujaa waliyedai Anapendelea Kwao.
Kazi Iendelee.CC Nyanduzy , @feke b kidume
[URL unfurl="true" media=
View attachment 3128482View attachment 3128483View attachment 3128484View attachment 3128485View attachment 3128486
Imewakata.Nitaendelea kuwaonesha kazi nzuri ya Samia Kila Kona ya Nchi hii.Wabongo wanasubiri afanye mambo kinyume na matamanio yao waanzishe uzi wa kuhoji uzanzibari wake!. Tuna akili za kipuuzi sana.
Kanifurahisha sana kufufua hicho chuo cha Malya cha michezo.
Kwa hiyo wewe uko site ya Kila mradi hapo Juu au siyo?Mimi nipo site Huku Mwanza na miradi yote imesimama.
Hata huo mradi wa daraja la Busisi umesimama pia?.Mimi nipo site Huku Mwanza na miradi yote imesimama.
Hakuna kilichosimama ,hater tuu huyoHata huo mradi wa daraja la Busisi umesimama pia?.
Ndio kazi anayofanya Samia na Tulia hapo MbeyaZiongezwe zaidi jiji la Mbeya liboreshwe hadi kufikia ku-compete na majiji kama Mwanza, Arusha na ikiwezekana ata Dar.
Ni bahati mbaya unaropoka Kwa sababu wewe sio msukuma ila ungekuwa msukuma ungejua kwamba machifu wao ni wanawake na wamekuwa wanawaongiza.wasukuma
hawaongozwi
na mwanamke
tuone mbeya ikipiga hatua maana Jiji letu lipo nyuma sana.Ndio kazi anayofanya Samia na Tulia hapo Mbeya
Huna Akili 💔Sitaki vingi nitajie kimoja tuu ambacho kilianzishwa na kutekelezwa na Serikali zilizopita.
Watu kama nyie msiotumia akili Huwa nawapenda sana,nitajie hicho kimoja.
Wewe mwenye akili nitajie miradi ya awamu ya 5 kwenye orodha hapoHuna Akili 💔
Kamanga- katunguru- sengerema km 3? Una Manisha 300 au 3?Kwa hiyo wewe uko site ya Kila mradi hapo Juu au siyo?
Ni hivi mliyegemea SSH ashindwe Sasa amewaumbua kaweza kuzidi mliozani wanaweza.
Km 3 ndio zinaanza ujenziKamanga- katunguru- sengerema km 3? Una Manisha 300 au 3?
eti mwanza imeachwa nyuma na Dodoma na arusha😂😂😂😂 chawa buana! kama kigezo ni airport kwani hizo airport za arusha na dodoma zinazidi nini ya mwanza?! mbona husemi mwanza ina stand mbili za mabasi za kisasa huku arusha kuna open space ndo wanaita stand😂😂Kwa muda mrefu maendeleo mwanza iliachwa nyuma. 2005 Mwanza lilikua Jiji la pili Kwa ukubwa TANZANIA ikiacha nyuma Arusha na Dodoma lakini hivi sasa Arusha na Dodoma wako mbele ya Mwanza Kwa ukubwa na maendeleo. Airport ya Mwanza ilikua kituko, Barabara ni vituko.
Kuona uthubutu aliofanya mama, kwangu Mimi nimefajirika na licha ya Kwa muda mrefu kutomkubali, Kwa maendeleo haya Mimi nafikiria kumpa kura yangu ya NDIO
Mwanza Mko nyuma sana,hapa mshukuruni mama ameamua kuwahwshumishaeti mwanza imeachwa nyuma na Dodoma na arusha😂😂😂😂 chawa buana! kama kigezo ni airport kwani hizo airport za arusha na dodoma zinazidi nini ya mwanza?! mbona husemi mwanza ina stand mbili za mabasi za kisasa huku arusha kuna open space ndo wanaita stand😂😂
Sawa ndugu wasemaji,ila akili za wengi zinawaambia huu ni msimu wa chaguzi,hivyo ni vyema kuamka mara kwa mara ili kuthibitisha kama kweli kumekucha ama tu ni ndoto za msimu wa chaguzi?30% ya Wapiga Kura wanatoka Kanda ya Ziwa
Inifwakti Kanda ya Ziwa ndio huchoose prezidenti 😂😂