Pre GE2025 Kwa huu utitiri wa miradi aliyomwaga Rais Samia mkoa wa Mwanza, angekuwa anatokea kanda ya Ziwa wapinzani wangesema anapendelea kwao

Pre GE2025 Kwa huu utitiri wa miradi aliyomwaga Rais Samia mkoa wa Mwanza, angekuwa anatokea kanda ya Ziwa wapinzani wangesema anapendelea kwao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkoa wa Mwanza ni Kati ya Mikoa ambayo Rais Samia amewapendelea sana Kwa kuimiminia miradi lukuki tena ya mabilioni Kwa mabilioni.

Miradi hiyo imegawanyika katika mafungu Makuu 3 ambayo ni

a)Miradi ya Urithi kutoka awamu ya 5,iliyokamilika na inayoendelea.

b)Miradi Mipya iliyoanza awamu ya 6 iliyokamilika na inayoendelea.

c)Na miradi ambayo Iko Mbioni kuanza wakati wowote .

Ifuatavyo ni miradi ambayo inatekelezwa na Rais Samia Mkoani Mwanza Kwa Kila kundi.

(a)MIRADI MIPYA
1.Ujenzi wa Barabara za Lami Mitaani mradi wa TACTIC Mwanza CC na Ilemela MC km 32 eg Buhongwa-Igoma

2.Ujenzi wa Soko La Kirumba na Soko la Samaki Mkuyuni Bilioni 25.

3.Upanuzi wa Kampasi ya TIA Usagara-Mwanza ,Bilioni 8

4.Ujenzi wa Soko Kuu la Jiji la Mwanza

5.Ujenzi wa Hospitali ya Jiji gorofa 6

6.Ujenzi wa Majengo Mapya ya Gorofa Chuo Cha Ufundi na Maendeleo Misungwi.

7.Ujenzi wa Jengo jipya la Mwanza Airport na kukarabati wa uwanja kuwa wa Kimataifa

8.Ujenzi wa Jengo la Kitega Uchumi la TBA Ghana Kota gorofa 7

10.Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu Cha Ardhi Mwanza (Sengerema)

11.Ujenzi wa Barabara za Mitaani chini ya TARURA eg Kisesa-Bujora,kiyungi road nk

12.Ujenzi wa Vyumba vya madarasa na shule Mpya zikiwemo za gorofa eg Kisenga ,Igudija nk katika Wilaya zote.

13.Ujenzi wa Vituo vya Afya, Hospital za Wilaya na ununuzi wa vifaa tiba Wilaya zote za Mwanza.

14.Mradi wa Maji Ukiriguru-Sumve Wilayani Misungwi Bilioni 32.

15.Ujenzi wa Barabara ya Hungumalwa-Ngudu-Magu km 71

16.Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Rufaa Ukerewe

17.Upanuzi wa Bandari za Mwanza South sanjali na ujenzi wa vivuko vipya.

18.Ujenzi wa Chuo Cha Michezo Malya (Malya Sports Complex and Training Centre).Zaidi ya Bilioni 40.

19.Ujenzi wa Barabara ya Mabuki-Jojiro-Ngudu

20.Ujenzi wa Barabara ya Mwanza Airport -Kayenze-Nyanguge

21.Ujenzi wa Barabara ya Nansio-Rugezi

22.Ujenzi wa Barabara ya Mwanangwa-Misasi-Salawe-Solwa-Kahama km 150.

23.Ujenzi wa Barabara ya Bukokwa-Nyakalilo

24.Ujenzi wa Barabara ya Ilalila-Shibula

25.Ujenzi wa Barabara ya Sengerema -Nyehunge km 54.4 (Bilioni 73).

26.Ujenzi wa Daraja Kubwa la Simiyu lenye mita 150 pamoja na Barabara Unganishi.

27.Ujenzi wa Daraja Kubwa la Sukuma lenye urefu wa mita 70 na barabara Unganishi km 4.

media="media="instagram:C89677rNdfd"]
View: https://www.instagram.com/p/C89677rNdfd/?igsh=ZTdkNml4YTQwa2V0[/URL]

View: https://youtu.be/Aq7AGgVXaxQ?si=fb9L7WED3YEdNVdb

(b)Miradi ya Urithi
1.Ujenzi wa daraja la JPM
2.Ujenzi wa Sgr ya Mwanza-Isaka
3.Ukamilishaji wa Stendi za
Nyegezi na Nyamhongolo
4.Ukamilishaji wa mradi wa Maji Butimba
5.Ukamilishaji wa Jengo la OPD Sekou Toure gorofa 6
6.Ukarabati wa Meli kubwa ya MV Mwanza Hapa kazi tuu.
7.Ukamilishaji wa Chuo Cha Ufundi na Teknolojia DIT Mwanza Campus
8.Ukamiloshji wa Tawi la Chuo Cha Mipango Vijijini Mwanza Centre

View: https://youtu.be/n97F4rAuoPs?si=tmTMNkcjX_nX7z3r

(c)Miradi ambayo Iko Mbioni kuanza ni

-Upanuzi wa Barabara ya njia 4 kutoka Mwanza CBD Hadi JPM bridge (lot 1 km 25),CBD-Usagara Jnct km 25.
-Ujenzi wa mgodi mkubwa wa Madini ya Dhahabu Nyanzaga
-Upanuzi wa Barabara kuu ya Musoma kuwa njia 4
-Upanuzi wa Barabara kuwa njia 4 kutoka Usagara-Shinyanga Border
-Kamanga-Katunguru-Sengerema km 3.
-Upanuzi kuwa njia 4 wa Barabara ya Mwanza-Nyanguge km 35.
-Mwanza Airport-Igombe-Kayenze-Nyanguge km 46
-Mkuyuni-Mahina-Nyakato km 10
-Nyakato(VETA)-Buswelu-Mhonze km 18.
View attachment 3127876

My Take
Hiyo ni Baadhi tuu ya miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Samia huko Mwanza.

Kiufupi Samia ameiheshimisha Mwanza kushinda Shujaa waliyedai Anapendelea Kwao.

Kazi Iendelee.CC Nyanduzy , @feke b kidume
[URL unfurl="true" media=

View attachment 3128482View attachment 3128483View attachment 3128484View attachment 3128485View attachment 3128486

Wabongo wanasubiri afanye mambo kinyume na matamanio yao waanzishe uzi wa kuhoji uzanzibari wake!. Tuna akili za kipuuzi sana.

Kanifurahisha sana kufufua hicho chuo cha Malya cha michezo.
 
Wabongo wanasubiri afanye mambo kinyume na matamanio yao waanzishe uzi wa kuhoji uzanzibari wake!. Tuna akili za kipuuzi sana.

Kanifurahisha sana kufufua hicho chuo cha Malya cha michezo.
Imewakata.Nitaendelea kuwaonesha kazi nzuri ya Samia Kila Kona ya Nchi hii.
 
wasukuma
hawaongozwi
na mwanamke
Ni bahati mbaya unaropoka Kwa sababu wewe sio msukuma ila ungekuwa msukuma ungejua kwamba machifu wao ni wanawake na wamekuwa wanawaongiza.

Back kwenye topic,hiyo ya kuongozwa inahusianaje na Samia kumwaga miradi huko Mwanza?
 
Kwa muda mrefu maendeleo mwanza iliachwa nyuma. 2005 Mwanza lilikua Jiji la pili Kwa ukubwa TANZANIA ikiacha nyuma Arusha na Dodoma lakini hivi sasa Arusha na Dodoma wako mbele ya Mwanza Kwa ukubwa na maendeleo. Airport ya Mwanza ilikua kituko, Barabara ni vituko.

Kuona uthubutu aliofanya mama, kwangu Mimi nimefajirika na licha ya Kwa muda mrefu kutomkubali, Kwa maendeleo haya Mimi nafikiria kumpa kura yangu ya NDIO
eti mwanza imeachwa nyuma na Dodoma na arusha😂😂😂😂 chawa buana! kama kigezo ni airport kwani hizo airport za arusha na dodoma zinazidi nini ya mwanza?! mbona husemi mwanza ina stand mbili za mabasi za kisasa huku arusha kuna open space ndo wanaita stand😂😂
 
eti mwanza imeachwa nyuma na Dodoma na arusha😂😂😂😂 chawa buana! kama kigezo ni airport kwani hizo airport za arusha na dodoma zinazidi nini ya mwanza?! mbona husemi mwanza ina stand mbili za mabasi za kisasa huku arusha kuna open space ndo wanaita stand😂😂
Mwanza Mko nyuma sana,hapa mshukuruni mama ameamua kuwahwshumisha
 
30% ya Wapiga Kura wanatoka Kanda ya Ziwa

Inifwakti Kanda ya Ziwa ndio huchoose prezidenti 😂😂
Sawa ndugu wasemaji,ila akili za wengi zinawaambia huu ni msimu wa chaguzi,hivyo ni vyema kuamka mara kwa mara ili kuthibitisha kama kweli kumekucha ama tu ni ndoto za msimu wa chaguzi?
 
Back
Top Bottom