Uchaguzi 2020 Kwa janja hii ya CCM kutumia ugeni wa kitaifa kuomba kura NEC semeni jambo

Uchaguzi 2020 Kwa janja hii ya CCM kutumia ugeni wa kitaifa kuomba kura NEC semeni jambo

Kwanza umemuita Rais na tambua Urais haukomi mpaka Hapo atakapoaapishwa Rais Mwingine na Ili kuweka kumbukumbu sawa Rais huyo mwingine Ni Dkt John Joseph Pombe Magufuli, Yaani kwa akili zako mgando na kwa kuwa ulikuwa na vyeti feki basi unataka wakati wa kampeni miezi miwili nchi ilale kisifanyike chochote.....hata USA wakati wa Kampeni kazi zinaendelea.....Pia Tambua kiuhalisia kupambana na Wenye vyeti feki Ni suala jema Sana ulitakiwa kumshukuru Rais wetu mpendwa Kuwa kafanya Kitu kizuri.
 
Lazima shughuli ziendelee kwa manufaa ya nchi jamani tatizo liko wapi kufanya shughuli za kiserikali
 
Nakushangaa sana Mtoa hoja . JPM bado ni Rais wa JMT kwa hiyo anafanya kazi pia , hawezi kuacha kazi ya Urais kwa kuwa yupo kwenye kampeni.

Wacha propaganda za ovyo.

Amekuja Rais wa Nchi jirani sasa Lissu ndio ampokee? Umemuona huyo Mgeni kwenye kampeni? Tulia watu wafanye kazi , hakuna sheria iliyovunjwa. JPM piga kazi achana na hawa wajeuri wasiotambua kuwa wewe ni Rais.
 
Wacha waombewe hizo kura tu, watanzania hawawasikilizi hao marais, alianza wa Burundi kumuombea kura kule Kigoma lakini hamna kitu, amefuata huyo nae hamna kitu.

Hata wakamlete Trump CCM hawapati kitu.
 
Mpuuzi ni wewe usiyejua kwamba kampeni hazitakiwi kwenye shughuli za kiserikali.
Nani alikutuma ukimbie mchakato wa katiba mpya pale bungeni?

Vyeo vya mheshimiwa vipo hata kama na yeye mgombea au hujui kama bado ni rais,Amir jeshi mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, mwenyekiti wa chama tawala na vile vile anateua na kutengua pia.
 
Kumbuka kuwa anakofia mbili.

Ndio maana pamoja na kofia zote hizo bado anatakiwa kufata sheria za NEC

Kwa maana hiyo basi Kuna siku jpm atafanya kampen Mpaka saa Sita usiku just because Ana kofia mbili
 
CCM kupitia mgombea wake wa urais Sasa wanatumia janja janja ziara na ugeni wa kitaifa kufungua miradi na kuomba kura. Ratiba ya Magufuli inasema ana pumziko kwa muda wa siku 10 na kuendelea baadaye. Lakini leo hii na muda huu anatumia nafasi yake Kama rais kufungua miradi na hapo hapo kuomba kura.

Balance ya fairness iko wapi, hawa wenzake kina Lissu wanawekewa barrier kila Kona. Hawatakiwi hata kutembelea mashina yao na kudhibitiwa kila wakionekana kujumuika katika shughuli either kiuchumi au kijamii. Ni Lini katika kipindi chote viongozi wa nje ndio wawe wanatuwekea jiwe la msingi kwenye miradi yetu? Na kwa Nini atumie nafasi hiyo kuwaombea kura wagombea wake na yeye kujiombea kura.

Wito kwa NEC, kwa kuwa huyu anayo advantage hiyo Basi wengine nao mazingira yawaruhusu m
 
Upuuzi mtupu kudhani shughuli za kiserikali zina ukomo kipindi cha kampeni.
Acha uzuzu wewe!
Hakuna anayelalsmika kuhusu shughuli za kiserikali hapa! HOJA NI KWA NINI MGOMBEA WA CCM ANATUMIA ZIARA YA UGENI WA MARAIS TOKA NJE KUJIPIGIA KAMPENI KINYUME CHA SHERIA YA UCHAGUZI!!!
Alichofanya Magufuli pale ni Matumizi mabaya ya Madaraka, Matumizi mabaya ya Raslimali za Serikali! Pale kaenda na magari ya Serikali siyo ya CCM. Upo??
 
CCM kupitia mgombea wake wa urais Sasa wanatumia janja janja ziara na ugeni wa kitaifa kufungua miradi na kuomba kura. Ratiba ya Magufuli inasema ana pumziko kwa muda wa siku 10 na kuendelea baadaye. Lakini leo hii na muda huu anatumia nafasi yake Kama rais kufungua miradi na hapo hapo kuomba kura.

Balance ya fairness iko wapi, hawa wenzake kina Lissu wanawekewa barrier kila Kona. Hawatakiwi hata kutembelea mashina yao na kudhibitiwa kila wakionekana kujumuika katika shughuli either kiuchumi au kijamii. Ni Lini katika kipindi chote viongozi wa nje ndio wawe wanatuwekea jiwe la msingi kwenye miradi yetu? Na kwa Nini atumie nafasi hiyo kuwaombea kura wagombea wake na yeye kujiombea kura.

Wito kwa NEC, kwa kuwa huyu anayo advantage hiyo Basi wengine nao mazingira yawaruhusu kutumia fursa itakayojitokeza.
NEC ni hovyo sana na maafisa wote wa NEC ni wa kutia kitanzi.
 
Swali ni Je, leo JPM alikuwa na ratiba ya kampeni Kibamba?

Kama hakuwa na ratiba hiyo then why ameomba kura akiwa kwenye eneo ambalo kiratiba za NEC hakupaswa kuwa hapo?
That's why tunataka Tume Huru ya NEC ya CCM imchukulie Hatua Magifuli! Tunajua Lissu tu KAZUIWA kwenda kutembelea matawi ya Chama kwa madai anafanya Kampeni....!!!
Huu ndo ujinga wa "Double Standards" tunaotakiwa kuukemea na kuulaaniwa kwa nguvu zote!!
 
Acha uzuzu wewe!
Hakuna anayelalsmika kuhusu shughuli za kiserikali hapa! HOJA NI KWA NINI MGOMBEA WA CCM ANATUMIA ZIARA YA UGENI WA MARAIS TOKA NJE KUJIPIGIA KAMPENI KINYUME CHA SHERIA YA UCHAGUZI!!!
Alichofanya Magufuli pale ni Matumizi mabaya ya Madaraka, Matumizi mabaya ya Raslimali za Serikali! Pale kaenda na magari ya Serikali siyo ya CCM. Upo??
Hahah

Zuzu wewe uliyekimbia mchakato wa katiba mpya pale bungeni halafu unajifanya hujui kwamba vyeo vyake bado anavyo hadi sasa mbali ya kuwa mgombea, pia ni rais, Amiri jeshi wa vyombo vya ulinzi na usalama, mwenyekiti wa chama tawala, na vile vile anateua na kutengua.

Umeona uzuzu wako wa kukimbia vitu muhimu kipindi cha bunge la katiba?
 
That's why tunataka Tume Huru ya NEC ya CCM imchukulie Hatua Magifuli! Tunajua Lissu tu KAZUIWA kwenda kutembelea matawi ya Chama kwa madai anafanya Kampeni....!!!
Huu ndo ujinga wa "Double Standards" tunaotakiwa kuukemea na kuulaaniwa kwa nguvu zote!!
Siku zote mnakaa kimya ila ikifikia kipindi cha uchaguzi ndio mnajua umuhimu wa TUME HURU?
 
Hahah

Zuzu wewe uliyekimbia mchakato wa katiba mpya pale bungeni halafu unajifanya hujui kwamba vyeo vyake bado anavyo hadi sasa mbali ya kuwa mgombea, pia ni rais, Amiri jeshi wa vyombo vya ulinzi na usalama, mwenyekiti wa chama tawala, na vile vile anateua na kutengua.

Umeona uzuzu wako wa kukimbia vitu muhimu kipindi cha bunge la katiba?

Nguvu nyingiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii na ujibu Hoja yoyote
 
JPM atashinda kwa kishindo hilo halina ubishi.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Back
Top Bottom