Kwa jicho la 3 ndoa za Kikristo ni mzigo kwa waume

Kwa hiyo unataka kusemaje labda? Kwamba unafikiri Babu zako waliyavuka hayo yote kiwepesi tu!!!!?

Timiza wajibu wako acha visingizio, vinginevyo utazidi kuona mambo ni magumu. Maisha hayajawahi na hayatawahi kuwa rahisi.

Naona hatuelewani mkuu, nimeelezea kinachoendelea kwa misingi ya kiuchumi....... Sasa katika kushupaza shingo na kuvumilia "majukumu" hiyo story nyingine tofauti kabisa maana kuna alieumbwa kubeba kilo 50 na kuna anayeweza kwenda kilo 200
 
They're delusional ndoa sio lelemama
 
Ndoa ya kikristo ingekuwa paradiso kama Biblia ingezingatiwa, lakini wanawake wa kikristo wengi huwanyanyasa waume wakijua hawawezi kuwapa talaka. Mwisho inatimiza usemi kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake hivyo, mletee mke mwenza atulie
 
Ndoa ni scam tu ndugu ukiona ni mkataba wa maisha ni perception yako tu ya kukaririshwa na wakoloni! Subiri ukatwe kichwa ndio ujione hujui. Wazungu waliowaletea ukatoliki wanazivunja na kuoa upya kila siku we umebeba gunia la misumari kichwani unateseka unaogopa vitu vya kufikirika? Wake upo broda
 
Utamchunguza mwanamke lakini nakwambia hutomaliza sifa zake za ndani, labda uishi nae kabla ya ndoa, umjue ndio uamue.
 
Kwa hiyo unataka kusemaje labda? Kwamba unafikiri Babu zako waliyavuka hayo yote kiwepesi tu!!!!?

Timiza wajibu wako acha visingizio, vinginevyo utazidi kuona mambo ni magumu. Maisha hayajawahi na hayatawahi kuwa rahisi.
Sema ww mada huaielewa. Rudia kusoma tena
 
Unanitia moyo kimtindo...
 
Oa wake watatu, utaishi kama mfalme, maana wanakuwa wanashindana kupata favor zako
Hao watatu ni wangapi wana uwezo wa kuwatunza wakaridhika wote?kumbuka kuishi na mwanamke kuna kuongeza familia pia sasa ndiyo kila mmoja amekuletea watoto watatu utawalisha vipi utawasomesha vipi?

Ni kuongeza umaskini tu bora kama mtu anajijua ana udhaifu fulani asiikaribie kabisa hii taasisi aiache kwa wenye uwezo
 
Hii plan ya kuwa na backup ni nzuri ila nawaza migogoro au mtoto kukosa malezi ya pande zote, hapo najikuta nakomaa kwanza
 
Inasemekana mwanamke ana masikio matatu... Usipolizibua SIKIO LA CHINI VIZURI kamwe hato kusikiliza..

Learn or perish.
🤣🤣🤣🤣utazubua sana ila haiwezekani kila wakati ukawaza jambo ilo ilo... Kwenye mengine sasa ndio mnaanza kuona mna mitazamo tofauti na itikadi tofauti na malezi tofauti mapendezi tofauti. Hatari
 
Kwani lazima uufutae huo ukristo,angalia faida na hasara za kufuata huo ukristo katika jambo lako.
 
Hakuna agizo la Mungu kuhusu kuoa. Unaweza oa au usioe ni uchaguzi wako.
 
Uzuri na unafuu kwa mwislamu ni ruhusa yakuoa mke zaidi ya mmoja,ni hivi mwanamke wa kwanza anaweza jirekebisha ukimwolea mke mwingine,ushahidi wa hilo upo,lkn upande wa uislamu napo kuna kaugumu kidogo kumwacha mkeo,labda hadi we mwanaume uzushe vitimbi dhidi ya mkeo,mfano kumpiga mara kwa mara,kutomtunza hasa kwa chakula,na we mwanaume wala huna sababu yakufanya hivyo,nk nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…