Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vizuri, kwa kuzingatia maoni yako ikiwa mabingwa wa msimu husika ndio unataka washiriki AFL basi haina tofauti na michuano ya champions league na hakuna haja ya mashindano mapya.Mkuu kuna mada hapo nime attach pia mtu anaweza soma nimesoma mi bado sijaelewa maana Team iwe imeshiriki hayo mashindano ya CAF.
Na tunajua kwenye kila team ikishiriki kila hatua hua ina vuna points.
Sa swali langu je zile Team zimepanda saiv ligi mfano ilivokuaga Leicester kule EPL ndio iwe Bongo ipande ibebe unaambiwa hio haiend kule AFL maana haina points kule so itatakiwa iende champions league iwe inakusanya kule points ina maana gani sasa hio mkuu?
Yan Man united amalize wa 7 na chesii then waahiriki UEFA?
Ukubwa unaupima kwa kushuka kiwango msimu mmoja au miwili? Haiendi hivyo. Man u au Liverpool zingekuwa timu ndogo sana kwa hiki kipimo chako. Ukubwa wa timu una mambo mengi na kubwa ni mashabiki, wafuasi na usisahau kuwa mpira ni biashara na biashara ni watu.Nadhani haiko fair
Kuna team Africa zishapoteza ubora kama hizo Wydad, Simba,na Kaizer ambazo zinapewa upendeleo kisa historia tulitaka tuone team imara na tishio kwa sasa kama FAR Rabat, Pyramid, Yanga n.k
One of the best Reply ever wanatengeneza madaraja ambayo Azam na Team za kawaida kuja kuyafikia ni ngumu sana.Kibaya zaidi, hao wenye ranking za juu wanaposhiriki ndio wanazidi kujiongesea ranking kwa maashindano hayo hayo.., maana yake hutoi nafasi kwa ushindani ili timu ndogo nazo zikuwe..
Mkuu watu hawajengi hoja wanataka utani usiokua na faida mda wote.Kiongozi nilikua na shauku kujua ulicho uliza ila kwa majibu haya...ndio maana nasemaga humu kwanza kuna watanzania ni wajinga wa kutupwa ,pia kuna umbumbumbu
AFL ni kombe la kibiashara zaidi jamaa wamelenga kupata pesa maana izo timu zenye rank kubwa ndio vigogo wa miaka mingi kwenye nchi zao wana mashabiki wengi kwaiyo muitikio utakua mkubwa. CAF wamepuyanga hajafikiria ile passion na legacy ya soka ambayo hauwezi kuinunua kwa pesa. Mashindano lazima yapande ngazi kwa mpangilio wa numerical order, yaani timu zipambane kufika nafasi za juu premier league halafu ulete mambo ya point sijui ranks ni upumbavu, sasa kuna maana gani ya kuwa na bingwa wa ligi kuu kama iyo title haitoshi kumpa sifa ya kwenda mbele zaidi.Inafikirisha sana kaaa kwa jicho la kimpira halaf tumia akili ya kawaida kabisa kuliwaza hili,
Usitumie hata Akili yako ya Form 4 wala form 6 tumia ile akili ya kuvukia Barabara tu Mkuu.
Waza Mpira ulibuniwa kwa hoja gani?..unahisi wazungu walikua malofa kuipinga Super League kwao?
Jiulize tu leo kuna shindano mtu anaenda kwa Ranks za CAF ndio linaitwa shindano kubwa Afrika na lenye thaman hivi jiulize tu itokeee FIFA waseme World Cup Team ziende kwa FIFA Ranking unahisi Afrika tutapeleka team ngapi?
Jiulize hivi leo inatokea Team A ambayo ipo juu kwenye Ranks za CAF ukanda flani ina maliza kwenye Ligi ya 4 halaf kuna Team C imepanda league currently ni mpya ila imeweka investment ya kutosha imemaliza nafasi 3 za juu kwa Ligi na remember haina historia yoyote kule CAF, kwahio hii Team ya nafasi ya 3 haitoenda popote maana unakuta Caf champions League anaenda yule wa 2 halaf hapohapo hii ya nafasi ya 4 itaenda super League?
Nachanganyikiwa kabisa na hii Afrika!!
Au sijaelewa maana wanaangalia points!!
Naomba mtu asitumie lugha ya kunikebehi au kunidhalilisha kama unanielewesha unieleweshe taratibu nipo tayar kuelewesha na wale ambao hawajaelewa kama mimi nao wataelewa.
Nielewavyo mimi Mpira ni mchezo wa kushangaza ndio Mpira huo...ukifanya Makosa una shangazwa, na Team iliyokua inachukuliwa ya kawaida ina take over.
Jiulize Team kama FAR RABAT,AZAM,PYRAMID,FUTURE Zitapata lini hio nafasi?
Wydad amepigwa juzi ikawa Rasmi hatoshiriki kombe lolote Msimu unaokuja kesho yake inakuja taarfa kuna kombe hilo ndilo Baba Lao na Taarfa inasema Kombe litahusisha Team zenye Points nyingi Kwenye ranks za CAF.
KUNA MCHEZO HAPA UMECHEZWA.
Halaf nawaza hata itokee Azam abebe Kombe Bongo ila ni Simba na Yanga ndio zitakua na Chance ya kwenda AFL na Azam ataenda Champions League?? au kule Morocco ni Wydad ndie ana chance zaidi ya FAR RABAT kucheza AFL!!
AFRIKA! AFRIKA!
Tulia nirudi kulala!
Soma pia👇
CAF Confederation Cup yafutwa. Msimu ujao kutakuwa na mashindano mawili tu
Msimu wa 2024/2025 kutakuwa na mashindano ya African football league na CAF champions league. African football league itahusisha timu 24 ambazo zitatoka kwenye zone tatu kulingana na rank zao za CAF. Zone 1) North Africa Zone 2) West / Central Africa Zone 3) South / East Africa Kwa sheria...www.jamiiforums.com
Ni kweli kabisa..hoja yako ni nzito.na si wewe tu ..mitandao ya zambia nayo inahoji km hv ? Hii JF ya sasa haina wale GT wa kipindi kile..sasa kuna maandazi tu humu..mmebaki wachache kama wewe..Mkuu watu hawajengi hoja wanataka utani usiokua na faida mda wote.
Ukiwaambia wajenge hoja waanza kukutukana.
Hivi kwanini hua unajiona una akili sana kuliko wengine?Isivyokuwa Bahati JF imejaza watu wa ajabu.
Nitarudi kukujibu kwa Hoja tunduizi.
Karibu sana.
Mbumbumbu wakishazamia mahali basi ni shida tupu, Europe wataendelea kututawala nasi tutaendelea kuwa Shit hole countries in the dark continent maana hatujifunzi kwa waishio dunia ya kwanza.Kuna muda jaribu kushiriki ubongo unapochangia mada. Sio muda wote ni kuhusu Chama na Pacome.
Utadhani akina Wydad Casablanca, Orlando Pirates, Keizer Chiefs, Asante Kotoko n.k hazikupenda kuendelea kuwa bora miaka yote kumbe hata Ulaya AC Millan, Juventus, Barcelona, FC Porto nazo zilikuwa bora zaidi ila siku hizi zimekuwa zilipendwa maana soka huwa lina kupanda na kushuka duniani kote.Wakati ulaya tunaona kina FC Copenhagen wanawekwa kundi moja na Bayern Munich huku kwetu wanatenganisha mchele na pumba
Copenhagen anawekwa kundi moja na Man United na bayern anasonga sisi huku!!Wakati ulaya tunaona kina FC Copenhagen wanawekwa kundi moja na Bayern Munich huku kwetu wanatenganisha mchele na pumba
Bora kuto kuwemo kuliko kuishia mashindano yanapo anziaYanga hammo![emoji2]
AFLNgoja hapa na mm nitie neno,kwa mfano young African no bingwa NBC pl na kwenye rank ni nambari 11 atashiriki shindano lipi kati ya Hays mawili??? AFL au CAFCL? Au atashiriki yote kwa pamoja