Kwa Jicho la kimpira kuifuta Confederation Cup, CAF wamepuyanga, Motsepe unaharibu soka la Afrika

Vizuri, kwa kuzingatia maoni yako ikiwa mabingwa wa msimu husika ndio unataka washiriki AFL basi haina tofauti na michuano ya champions league na hakuna haja ya mashindano mapya.

Kuwa kwenye nafasi za juu kwenye ranking za caf inamaanisha consistency so mi nadhani hii AFL inatakiwa iangalie hiyo na si katimu kanaibuka ka uyoga nako kanashiriki AFL ikiwa hivyo kutakuwa hakuna utofauti wa radha katika mashindano.
 
Nadhani haiko fair

Kuna team Africa zishapoteza ubora kama hizo Wydad, Simba,na Kaizer ambazo zinapewa upendeleo kisa historia tulitaka tuone team imara na tishio kwa sasa kama FAR Rabat, Pyramid, Yanga n.k
Ukubwa unaupima kwa kushuka kiwango msimu mmoja au miwili? Haiendi hivyo. Man u au Liverpool zingekuwa timu ndogo sana kwa hiki kipimo chako. Ukubwa wa timu una mambo mengi na kubwa ni mashabiki, wafuasi na usisahau kuwa mpira ni biashara na biashara ni watu.
 
Kibaya zaidi, hao wenye ranking za juu wanaposhiriki ndio wanazidi kujiongesea ranking kwa maashindano hayo hayo.., maana yake hutoi nafasi kwa ushindani ili timu ndogo nazo zikuwe..
One of the best Reply ever wanatengeneza madaraja ambayo Azam na Team za kawaida kuja kuyafikia ni ngumu sana.
 
naona shauku ya Motspe ni kuifanya hii ligi iwe ya kuvutia kupitia hawa wakubwa waliokuwa dominant ila pia je hawatatumia new records?sababu miaka 5 nazani ya hesabu za points imeshapita..au bdao?
 
Kiongozi nilikua na shauku kujua ulicho uliza ila kwa majibu haya...ndio maana nasemaga humu kwanza kuna watanzania ni wajinga wa kutupwa ,pia kuna umbumbumbu
Mkuu watu hawajengi hoja wanataka utani usiokua na faida mda wote.

Ukiwaambia wajenge hoja waanza kukutukana.
 
AFL ni kombe la kibiashara zaidi jamaa wamelenga kupata pesa maana izo timu zenye rank kubwa ndio vigogo wa miaka mingi kwenye nchi zao wana mashabiki wengi kwaiyo muitikio utakua mkubwa. CAF wamepuyanga hajafikiria ile passion na legacy ya soka ambayo hauwezi kuinunua kwa pesa. Mashindano lazima yapande ngazi kwa mpangilio wa numerical order, yaani timu zipambane kufika nafasi za juu premier league halafu ulete mambo ya point sijui ranks ni upumbavu, sasa kuna maana gani ya kuwa na bingwa wa ligi kuu kama iyo title haitoshi kumpa sifa ya kwenda mbele zaidi.
 
Mkuu watu hawajengi hoja wanataka utani usiokua na faida mda wote.

Ukiwaambia wajenge hoja waanza kukutukana.
Ni kweli kabisa..hoja yako ni nzito.na si wewe tu ..mitandao ya zambia nayo inahoji km hv ? Hii JF ya sasa haina wale GT wa kipindi kile..sasa kuna maandazi tu humu..mmebaki wachache kama wewe..
 
Kuna muda jaribu kushiriki ubongo unapochangia mada. Sio muda wote ni kuhusu Chama na Pacome.
Mbumbumbu wakishazamia mahali basi ni shida tupu, Europe wataendelea kututawala nasi tutaendelea kuwa Shit hole countries in the dark continent maana hatujifunzi kwa waishio dunia ya kwanza.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Wakati ulaya tunaona kina FC Copenhagen wanawekwa kundi moja na Bayern Munich huku kwetu wanatenganisha mchele na pumba
Utadhani akina Wydad Casablanca, Orlando Pirates, Keizer Chiefs, Asante Kotoko n.k hazikupenda kuendelea kuwa bora miaka yote kumbe hata Ulaya AC Millan, Juventus, Barcelona, FC Porto nazo zilikuwa bora zaidi ila siku hizi zimekuwa zilipendwa maana soka huwa lina kupanda na kushuka duniani kote.
 
Wakati UEFA wameongeza Europa conference league Ili timu nyingi zipate nafasi zaidi kushiriki mashindano mkubwa, CAF wenyewe wanapunguza, hovyo kabisa.
 
Ngoja hapa na mm nitie neno,kwa mfano young African no bingwa NBC pl na kwenye rank ni nambari 11 atashiriki shindano lipi kati ya Hays mawili??? AFL au CAFCL? Au atashiriki yote kwa pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…