Kwa kamasi na chafya hizi, ugoro umeshawaingia. Watoto wapendwa shikilieni hapo hapo.

Kwa kamasi na chafya hizi, ugoro umeshawaingia. Watoto wapendwa shikilieni hapo hapo.

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
581
Hadithi hadithi. Hadithi njoo, uongo njoo, utamu kolea.

Wale watoto wawili kwa nyakati tofauti wiki hii wameendelea kutema nyongo dhidi ya mkulu na kundi linalomzunguka ambalo inadaiwa ndilo linachafua hali ya katika kijiwe cha wadanganyika walio hoi bin taaban Kiuchumi na kiusalama pia.

Pamoja na watoto wawili Hawa ambao inadaiwa kuwa wamevua marapu rapu ya maguo waliyokuwa wamevaa hapo awali na kuvaa nguo mpya, kupuliza pumzi ya moto kwa walioshika mpini, bado kelele zao zinaonekana kutomzuia ng'ombe kunywa maji.

Washika mpini wanaendelea na mikakati yao ya namna bora ya kuendelea kujihomolea vyote vilivyomo kwenye ardhi ya wadanganyika.

Hata hivyo katika siku za karibuni, washika mpini na wengine waliowazunguka wameanza kujibu 'vihoja' vya wale watoto wapendwa ambao pia zamani walikuwa wavaa marapurapu.

Hii ni dalili ya uoga, lakini pia kwa chafya, na kamasi hili zito bila shaka vijiugolo vinawaingia vizuri.

Wadanganyika wote waitikie Amen.

Hadiithi yangu inaishia hapa.
 
Jamaa press Moja tu leo...watu Wana ropoka tu...mara kufa mara sjui nini...
 
Back
Top Bottom