Kiturilo
JF-Expert Member
- Sep 27, 2021
- 708
- 2,859
Nimesikitishwa sana baada ya kutonywa na mtu kwamba eti wote waliokuwa kwenye top positions kwenye serikali ya awamu ya tano wanatakiwa kuondolewa!
Lakini nawahakikishia wote wenye hiyo mipango ovu kuwa watafanikiwa kuwatoa kwenye nafasi zao lakini kamwe hawatafanikiwa kuwatoa ndani ya mioyo ya watanzania na pia hawatafanikiwa kamwe kufuta kazi zao walizowafanyia watanzania.
Ni kweli Dk Kalemani siyo waziri tena lakini si Bwawa la nyerere lipo na linaendelea kujengwa kule Rufiji?
Nani hajui kuwa enzi ya Dk Kalemani majenereta yalikosa soko? Nani hajui kuwa enzi zake wananchi waliacha kuuziwa nguzo za umeme?
Ni kweli Dk Tito Mwinuka siyo MD wa Tanesco tena lakini si ndiyo ameifanya Tanesco iache kuagiza nguzo nje ya nchi na kuanzisha kiwanda cha kutengeneza nguzo zao wenyewe za zege,? pia na kuacha kutegemea ruzuku serikalini?
Ni kweli Dk Chamriho hayupo wizara ya ujenzi ,lakini si ndiyo amesaini na kutujengea flyover kila sehemu? Ina maana ukimtoa wananchi watasahau kuwa Mfugale na Kijazi flyovers zimesimamiwa na yeye?
Tunawaonya tu watoeni wote alafu tuone hizo kura za kuwafanya mshinde mtaenda kuomba wapi.
Kinachombeba mtu ni utendaji wa kuwafanyia kazi wananchi na siyo porojo zenu.