Kwa kasi hii ya Azam Wachina wa StarTimes wajiandae kufungasha virago?

Kwa kasi hii ya Azam Wachina wa StarTimes wajiandae kufungasha virago?

Kwa kasi hii ya Azam wachina wa Startimes wajiandae kufungasha virago?

Naona Azam media wanazidi kuja kwa kasi leo hii wamezindua minara ya bilioni 50 mikoa 21

Baada ya Dish wamekuja na vya Antenna, hawa jamaa wapo vizuri sana naona kwa sasa Wachina wa Startimes wajiandae kisaikolojia tu maana sidhani kama kuna mtu timamu atatumia vile vidubwashwa vyao.

Kongole Azam media sasa huku kwa vya Antenna ndo mnaenda kusepa na nyomi ya kijiji.
Hao Azam ukicha league ya bongo hawana jipya kabisa
Start time wapo vizuri sana kwa kila idara
Hata rejea piatakwimu za TCRL king'amuzi kinachoongoza kuwa na wateja wengi ni kipi kama sio Startime..

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Natumia Azam nyumbani wanatumia DStv na dukani kuna startimes Azam hana content kabisa ukiondoa mechi za ligi kuu za Simba na Yanga hakuna kinachobakia
Imagine vipindi ni vya kina Bin Zubery na labda hizo tamthiliya ambazo hata sijui zinatoka wapi zinaenda wapi
Imagine game za uefa,Europa,Seria A zote huoni Wala zile za Spain labda waboreshe
Movie ndio kabisa Kila siku utaangalia Colombiana na Sicario
Unafananisha Azam na mikebe yenu are you serious??
 
Hao Azam ukicha league ya bongo hawana jipya kabisa
Start time wapo vizuri sana kwa kila idara
Hata rejea piatakwimu za TCRL king'amuzi kinachoongoza kuwa na wateja wengi ni kipi kama sio Startime..

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Kilibebwa na serikali na tcra kwa sababu ya kuhamia digital mwaka 2013 but kinyume na hapo hamna kitu
 
Kama huna uhakika wa milo mitatu nunua STARTIMES, ksm una uhakika wa milo mitatu nunua AZAM kama unahela amabzo hazina matumizi nunua DSTV


Azam ukiondoa tu NBC PL, hana contents kabisa na nikiwa home naanagalia mpira NBC PL na Taarifa ya Habari Basii!

Azam TV akiboresha baadhi ya Vitu kama Contents akapunguza yale matamthilia wanoweka sauti akina MBOTO, akaajaza Documentary, Music akapunguza yale Machannels kila ukiweka unakuta watu wanazunguka lile dude la mraba pale MAKA


Angechangamka akaweka na Championship basi atakamata soko sana!!
 
Ana hoja kubwa tu..contents nyingi za hicho kisimbuzi zipo upande wa Muslims hata tamthilia zao maudhui ya vipindi na hata watangazaji..hiko wazi kabisa
Kuna kipindi Fulani Cha kuchambua michezo Kila jumapili asubuhi, Sasa timu ya Tanzania ikiwa inacheza kimataifa baada ya kipindi wanatoa Dua , du!! hata hawajishtukii kuwa nchi ni mchanganyiko wa wasio na dini na dini tofauti kwao ni full kiarabu utadhani wapo masjid
 
Jamiiforums ni sehemu ndogo sana ya maisha yetu. Hiko kisimbuzi cha Star times mnavyokisakama kila siku humu mpaka juzi nikaona takwimu ndio kinachoongoza kwa mbali sana kuwa na watumiaji wengi Tanzania.
Hata mimi nashangaa kwa kweli. Ishu ni bei ya kifurushi na channeli.

Siyo Watanzania wote wanapenda mpira, hivyo wanunue sijui Azam. Wapo Watanzania wameridhika na Startimes kwa sababu ya channel zao na bei ya chini ya kifurushi ambacho kinaanzia elfu kumi.

Kisimbuzi ambacho kitamfungashia virago mwenzake ni kile ambacho kitapunguza bei ya vifurushi.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Ukitoa DSTV king'amuzi kinachofuata kwa ubora ni startimes, kwa upande wa football wako vizuri, series za kizungu, kihindi kichina, kikorea na kituruki wako vizuri kwa upande wa Tamthilia zilizotafsiriwa ingawa mimi sio mpenzi nazo ila The Brothers hainipiti, kwa upande wa michuano ya kimataifa star times inaonyesha ligi nyingi zaidi ya Azam huku mpaka Ronaldo anaonekana,kwa upande wa soka la Africa, wanaonyesha michuano yote inayosimamiwa na caf, Tunaangalia ligi ya kenya, tunaangalia ligi ya Uganda na kwa upande wa Tanzania wameanza na champioshp,
Hiyo brothers inasawiri maisha ya baadhi ya nchi za ulimwengu wa tatu Tanzania ikiwemo.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Anzisheni na nyie cha kwenu mrushe upako siku nzima hakuna atakaekuzuia ilimradi unalipa Kodi.
Tusipangiane maisha.
Acha makasiriko ostadh ,bila shaka uta kua una linda pale.Tv imani
 
Jamiiforums ni sehemu ndogo sana ya maisha yetu. Hiko kisimbuzi cha Star times mnavyokisakama kila siku humu mpaka juzi nikaona takwimu ndio kinachoongoza kwa mbali sana kuwa na watumiaji wengi Tanzania.
Inabidi pia ujue wingi wa watumiaji wa Startimes umeletwa na wao kuwa wakwanza kwanza kuwa agressive pindi mabadiliko yalipofanywa kutoka analog kwenda digital..kimsingi soko lilikuwa bado halina competition kama sasa,Dstv walikuwepo lakini walikuwa wanafanya mambo kimbwenyenye..

Naamini growth rate yake imepungua compared to Azam as of now..
 
Wanaume tunanunua decoder kwaajili ya mechi. Ikatokea hawa Canal + wakaingia Tz hizo decoders zingine zote zitapunguza mauzo.

Niliona Canal + wamepigwa marufuku hata kwa uchache wao wa sasa. DSTV ni bei rahisi South kuliko hapa at some point ilikua kulipia kifurushi cha juu kabisa South ni sawa na elfu 50 ya hapa.

Ila hapa kifurushi hicho hicho kinatafutana na mshahara wa kima cha chini.
 
Usifananishe Startimes Na Vitu Vya Hovyo Hovyo Tshs 15000/= Unaona Mwezi Mzima
Kifurushi Kikiisha Local Channels Zote Bure, Sasa Azam Hakuna Ikiisha Wanazima
Acha upotoshaji hata usipolipa local channels zote zinakuwepo tu.Halafu kwenye contents azam yupo vizuri zaidi na channels nyingi ni nzuri kiasi chake,wewe kisimbusi gani hakina hata channels za KENYA?!!Hiyo startimes inaongoza kuwa na wateja wengi kutokana na wakati ule huduma hii inaanza ndio kilikuwq kisimbusi bora kuliko vingine(zuku,continental,digiteck,na ting)ila baada ya azam kuingia ni suala la muda tu atahama na kijiji,na sasa ambapo huduma ya antenna imeanza kusambazwa nchi nzima!!
 
Bilioni 50 kusambaza antena? Badala ya kulipia EPL??

Azam bado sana...hawana channels za maana kabisa ...hata channels za South Africa Tu hawana hata moja
Sijui kama hamuongei lugha 2 tofauti.
Jamaa anaongelea minara zaidi na antena ni moja kupanua wigo kwa wateja wengi sambamba na hiyo minara.
Ikiwa ataonyesha EPL na huku mikoa mingi aifikiwi kuna faida gani?
Bora wapanue wigo wa watazamaji ili wakianza kuonyesha EPL watawafikia wateja wengi
 
Ni kweli kinaongoza ,sbb wao ndo walikuwa waanzilihi, lakini muda unavyozidi kwenda ,dstv na dish ya kawaida yanashika Kasi mikoani
 
Kuna kipindi Fulani Cha kuchambua michezo Kila jumapili asubuhi, Sasa timu ya Tanzania ikiwa inacheza kimataifa baada ya kipindi wanatoa Dua , du!! hata hawajishtukii kuwa nchi ni mchanganyiko wa wasio na dini na dini tofauti kwao ni full kiarabu utadhani wapo masjid
Kipindi Cha hovyo sana hasa akiongoza Zubery kinakuwa kama kijiwe Cha kahawa anamuhoji mtu huku yeye anasoma sms kwenye simu wako live mwenzake anatoa uchambuzi ye anakupa taarifa za Le Mutuz kufariki yani jamaa kile kipindi amuachie angalau kabombe ndie huwa anakimudu vema
 
Back
Top Bottom