Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Walewale kama .mh nkamia. Tusiwe na akili fupi kiasi hicho kwa ushabiki tu..hadi washindwa chambua mambo kwa weredi. Nchi yenyewe bhado msimamo wa taifa haujulikani . Hata ujinga sio hivyo, kwani alietufikisha hapa tulipo sasa nani au hatumjui. Tuamke na tujitambue kama taifa .tufuate sheria na taratibu tulizojipangia kwani ndo mwongozo wetu.

But bongo shida kubwa ni elimu na kujitambua tu...kwani wasomi wachache na wasio soma wengi hadi wamepitiliza ... it means wajinga wengiiiiiiiiiiiiiii.....
Mfano mdogo shuleni wanafunzi wanafanya mtihani 200. Then wanaofaulu kuendelea ni wanafunzi 5 au 10. Hawa waliofeli wanaenda wapi..tujitambue bhanah hata kama njaa kali co kwa shit hizo......

team. Uzalendo wa kweli........
 
d66e5324c7f69eda58417abbd809baa6.jpg
 
uchaguzi mwingine wa rais tufanye 2035 aongoze kwa miaka 20 mfululizo.
Nadhani uchaguzi hufanywa kwa matakwa ya kikatiba na si kwa kiwango gani Rais aliyeko madarakani katekeleza ahadi zake. Vionjo vya mafanikio yake hufanya uchaguzi kuwa rahic kwa aliyeko madarakani au chama tawala hats hivyo si jambo jema kufikiria kwa namna yoyote ile na kuanza kujenga mazingira ya uvunjifu wa katiba. Tumpongeze kwa kasi nzuri ya kuwafikia watanzania waliowengi na mipango mizuri ya maendeleo.
 
Unaandika mambo mengi mazuri ila unaweza ukaandiaka kitu kingine ambacho hakihusiani na MAGUFULI.kila siku thread zako ni predictable.MAGU ameshasema hahitaji praise singers amekuja kuafanyakazi.
 
Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sasa, sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja kweli ya kufanya tena uchaguzi wa rais?, si tumwache tuu aendelee mpaka pale tutakaapoona tumetosheka?.

1. Pamoja na ukanyagaji wake wa katiba ya nchi, lakini kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuinyoosha nchi hii iliyopinda kupindukia kwa rushwa, uzembe na ufisadi, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya uchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tuu aendelee mpaka 2025? na kama bado anatosha, aendelee tuu?.

2. Jee hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, na kumwacha Magufuli kupita bila kupingwa, ili kuokoa muda, pesa na mali?, hivyo Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025 and beyond?.

3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike kwa mujibu wa katiba, hata kama uchaguzi huo ni wastage of time, money and resources?!. Kwani katiba ndio nini hata iheshimiwe hivyo?.

4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.

5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, ingekanyagwa kirahisi rahisi na kupuuzwa, huku watu wakiangalia tuu?, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.

6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.

8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, , Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?.

9. Na baada ya katiba kukanyagwa, kwa mikutano ya siasa kuzuiwa, jee kuna ubaya wowote kama wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, haswa kwa kuzingatia the playing field is not level, na badala yake CCM tuu ndio iwe pekee inatoa mgombea urais siku zote kufuatia long eksipirience ya uzoefu wa muda mrefu wa CCM wa kumtoa rais ambaye siku zote huchaguliwa kwa ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huru na wa haki?.

10. Na kufuatia somo la demokrasia ya Kiafrika, na mfano hai wa matokeo ya urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea urais wa kushindana na mgombea wa chama dola, CCM?, yaani by now tumeishajua mgombea wa CCM kwa 2020 ni Magufuli?, kuna chama kiko tayari kumteua mgombea wake kushindana na Magufuli ambaye ni a sitting president, huku kutakuwa ni kugombea au kujifurahisha tuu?!, au hata ikitokea huyo mgombea wa upinzani ameshinda atatangazwa?!.

Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.

Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Paskali
Point namba tatu umesema wastage of time, money and resources. Kwa hiyo time and money it's not a part of resources .????
 
Swali jepesi.
Je, kila mtu anadhani hivyo?
Kama sio, basi uchaguzi ni muhimu kwa ajili ya kupata chaguo/mtizamo wa wengi...
Kwa maana huo ni mtizamo wako.
 
Mkuu Jeki, kiukweli kauli hizi ni tatizo!, nimezifanyia psychoanalysis kauli hizo nikagundua zinatokana na some deep rooted neurosis zinazompa inferiority complex na lack of confidence hivyo hizi kauli na matendo ya superiority complex ni matokeo tuu.ĺĺl

Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Paskali
Kwa maana hiyo ni lazima watanzania tuwe na huruma kwa mwenzetu, 2020 tumsaidie ili apumzike tu asiendelee kujitesa bure maana walio tayari kuongoza bila kulalamika wapo.
 
Siku Pascal uliyoalikwa kwenye Press Conference pale Ikulu na kupata nafasi ya kuuliza swali sisi wengine tulipata tafsri rasmi ya jina lako MAYALA na tafsri hii ilitolewa na Mkulu.

Labda kwa kuweka kumbukumbu sahihi na tujikumbushe tafsiri hiyo. MAYALA kwa Lugha ya Kisukuma ni NJAA.
 
Toa ndoto zako za mchana Paskali, hivi siku hizi unataka kuwa mwehu, au ugumu wa maisha unakusukuma huandike hii. Hakika tutasoma namba wote.
 
Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sasa, sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja kweli ya kufanya tena uchaguzi wa rais?, si tumwache tuu aendelee mpaka pale tutakaapoona tumetosheka?.

1. Pamoja na ukanyagaji wake wa katiba ya nchi, lakini kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuinyoosha nchi hii iliyopinda kupindukia kwa rushwa, uzembe na ufisadi, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya uchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tuu aendelee mpaka 2025? na kama bado anatosha, aendelee tuu?.

2. Jee hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, na kumwacha Magufuli kupita bila kupingwa, ili kuokoa muda, pesa na mali?, hivyo Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025 and beyond?.

3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike kwa mujibu wa katiba, hata kama uchaguzi huo ni wastage of time, money and resources?!. Kwani katiba ndio nini hata iheshimiwe hivyo?.

4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.

5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, ingekanyagwa kirahisi rahisi na kupuuzwa, huku watu wakiangalia tuu?, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.

6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.

8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, , Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?.

9. Na baada ya katiba kukanyagwa, kwa mikutano ya siasa kuzuiwa, jee kuna ubaya wowote kama wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, haswa kwa kuzingatia the playing field is not level, na badala yake CCM tuu ndio iwe pekee inatoa mgombea urais siku zote kufuatia long eksipirience ya uzoefu wa muda mrefu wa CCM wa kumtoa rais ambaye siku zote huchaguliwa kwa ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huru na wa haki?.

10. Na kufuatia somo la demokrasia ya Kiafrika, na mfano hai wa matokeo ya urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea urais wa kushindana na mgombea wa chama dola, CCM?, yaani by now tumeishajua mgombea wa CCM kwa 2020 ni Magufuli?, kuna chama kiko tayari kumteua mgombea wake kushindana na Magufuli ambaye ni a sitting president, huku kutakuwa ni kugombea au kujifurahisha tuu?!, au hata ikitokea huyo mgombea wa upinzani ameshinda atatangazwa?!.

Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.

Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Paskali

NINA WASIWASI NA UWEZO WAKO WA KUELEWA MAMBO, UNAANDIKA SANA HUMU ILA MAMBO MENGINE UNAJIABISHA, MWANDISHI HURU ILA MAWAZO YAKO HAYAKO HURU. JIFUNZE KUTAFAKARI KWANZA KABLA YA KUANDIKA, PASCAL UNAPOTOKA MNO, HUJUI BIASHARA ZINAENDAJE, HUJUI HALI YA WATANZANIA WENGI MAISHA YAO YAMEFIKA WAPI, HUJUI DIRA YA NCHI, HUJUI FOCUS YETU NA PRIORITY NI ZIPI, HUJUI DEMOKRASIA INAVYOFINYWA NADEMOGRASIA INAVYOUISHWA, KAMA UNATAFUTA TEUZI ALL THE BEST ILA KAMA UNATUMIA IBARA YA 18 YA KATIBA YETU KUTUHABARISHA BASI UNATAKIWA UHABARISHE KICHWA CHAKO KWANZA NA KIELEWE SOMO ALAFU NDO UTAHABARISHE.
 
Back
Top Bottom