Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja ya kufanya tena uchaguzi wa rais?, si tumwache tuu aendelee?.

1. Kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya kchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tuu aendelee mpaka 2025?.

2. Jee hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, kwa Magufuli kupita bila kupingwa, na badala yake , ili kuokoa pesa, mali na muda?, na Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025?!.

3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike hata kama ni wastage of time, money and resources?!.

4. Na hiyo 2025 tukimuona bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili katiba yetu tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.

5. Kwani katiba ni nini?,si ni kipande tuu cha karatasi?!, nini muhimu kati ya kipande cha karatasi na umuhimu wa Magufuli kwa taifa?!.

6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, tukimtaka Magufuli, si tunaweza kuiweka tuu katiba pembeni tukaendelea na Magufuli wetu?!.

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu?!,

8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Jee kuna ubaya kama Magufuli akipatiwa muda wa kutosha kama Kagame, Museveni au kama Mugabe?.

9. Na jee kuna ubaya wowote wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, na badala yake CCM tuu ndio iwe inatoa rais siku zote kufuatia long eksipirience ya CCM na uzoefu wa muda mrefu kwa CCM kwenye urais?.

10. Na kufuatia somo la urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea kushindana na Magufuli?! 2020?, kutakuwa ni kugombea au kujifurahisha tuu?!, au hata ikitokea huyo mgombea wa upinzani ameshinda atatangazwa?!.

Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.

Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Paskali

Kuna wengine labda watakuona queer, lakini sio Mimi:
1. Katiba haiandikwi kwa ajili ya MTU mmoja au kizazi kimoja tu. Katiba lazima izingatie maslahi ya nchi ambayo ni mapana zaidi ya uchaguzi mmoja uliomweka rais madarakani.

2. Uchaguzi huru na wa haki hatujawahi kuushuhudia hapa kwetu, wewe wajua. Na hili so lawama au credi kwa mtu au chama bali kwa mfumo mzima.

3. Katiba sio "kipande cha karatasi" kama wewe unavyoelewa! Katiba ni sheria, tena ni mama wa sheria zote, ni falsafa, ni mwongozo, ni mila etc. na si lazima iwe written eg.: (UK constitution)
Ukiiona katiba kama kipande cha karatasi kamwe hutaiheshimu na hutaheshimu sheria nyingine zote.

4. Rais ni taasisi, sio MTU. JPM ni binadamu, na we we unajua maumbile ya binadamu; hatuko perfect. Inaonekana mwenzetu hutofautishi vitu hivyo viwili kwa sababu zako.

5. Sio busara kubadili au kufuta Katiba kwa faida ya MTU mmoja au kikundi kimoja cha watu (chama). Katiba ndio msingi wa Mihimili mitatu ya Utawala (DOLA). Katiba ndio kielelezo cha mipaka ya mamlaka ya Bunge, Mahakama na Serikali. Katiba ya nchi ni zaidi ya vitu mnavyoita "TUNU" kmf. Kiswahili. Leo nikisema kiswahili kimedumaza elimu yetu mtasemu siheshimu tunu za taifa! lakini Katiba ya nchi mnaiita "kipande cha karatasi" Hiki ni kiroja.

6. Kwahiyo ukibadili au kufuta Katiba kwa faida ya MTU mmoja (sio taasisi)!!! matokeo yake umefuta mamlaka ya mihimili mitatu ya DOLA. Maana yake unasimika UDIKTETA. Na kuna udikteta wa MTU mmoja na wa kikundi cha watu, vyote ni haramu.

7. Mfano: Huwezi kumfanya jaji wa mahakama asifuate tena sheria, eti kwasababu umeshinda kesi au alifuta kesi yako!
Huwezi kusema eti: 'Kwasababu Bunge limetunga sheria nzuri tusiwe na uchagizi wabaki wabunge hawahawa mpaka lini sijuwi!! Dunia itawashangaa.

9. Swali unalowauliza wapinzani ungewauliza CCM kwanza kama wako tayari kuendesha uchaguzi ulio huru na wa haki na kuwapa wapinzani Serikali iwapo watashinda kihalali? Kwasababu wapinzani hawatumii polisi ili washindwe kila uchaguzi. Bali siku zote mwenye nguvu ya dola ( incumbent); asiyeheshimu katiba, akiona mambo yake hayaendi anavyotaka yeye hutumia nguvu.

Kwa hayo machache naishia hapo. Umeleta mada nzuri, ila kama lugha yangu imekukwaza kwa namna yoyote niwie radhi baba.
 
Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja ya kufanya tena uchaguzi wa rais?, si tumwache tuu aendelee?.

1. Kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya kchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tuu aendelee mpaka 2025?.

2. Jee hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, kwa Magufuli kupita bila kupingwa, na badala yake , ili kuokoa pesa, mali na muda?, na Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025?!.

3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike hata kama ni wastage of time, money and resources?!.

4. Na hiyo 2025 tukimuona bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili katiba yetu tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.

5. Kwani katiba ni nini?,si ni kipande tuu cha karatasi?!, nini muhimu kati ya kipande cha karatasi na umuhimu wa Magufuli kwa taifa?!.

6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, tukimtaka Magufuli, si tunaweza kuiweka tuu katiba pembeni tukaendelea na Magufuli wetu?!.

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu?!,

8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Jee kuna ubaya kama Magufuli akipatiwa muda wa kutosha kama Kagame, Museveni au kama Mugabe?.

9. Na jee kuna ubaya wowote wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, na badala yake CCM tuu ndio iwe inatoa rais siku zote kufuatia long eksipirience ya CCM na uzoefu wa muda mrefu kwa CCM kwenye urais?.

10. Na kufuatia somo la urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea kushindana na Magufuli?! 2020?, kutakuwa ni kugombea au kujifurahisha tuu?!, au hata ikitokea huyo mgombea wa upinzani ameshinda atatangazwa?!.

Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.

Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Paskali
Acha ukabila paskali, au unajipendeza upate udc?
 
Ukisoma haraka huwezi kuelewa hili bandiko.
Kipengele namba kumi kinaweza kuwa na maana sana kuliko vipengele vyote.

Maudhui na dhima ya bandiko ni zaidi ya uchaguzi, ubora wa rais bali umuhimu na matakwa ya kikatiba
 
Paskali nadhani usomi wako umejaa kujipendekeza na unafiki.
Kama unajua matakwa ya katiba kwa nini uandike hewa.
Mkuu tunaona anayofanyia nchi na wana nchi wanaona hakuna haja ya kuvunja katiba au kuibadili sanduku la kura ndo litakalo amua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli generation hii imejaa wanafiki,waoga na watu ambao wapo tayari kuvunja sheria ili mradi matakwa yao yafikiwe,with my high respect kwa mtoaji hii mada sikutegemea kuwa naye atakuwa mmoja wa watu ambaye pamoja matatizo tuliyokuwa nayo kuhusu katiba yetu atashauri katiba ivunjwe kwa masilahi ya our no 1,elewa katiba ndio sheria mama na inaelekeza kuwa uchaguzi mkuu wa Rais utakuwa unafanyika kila baada ya miaka mitano,sasa our own great thinker halioni hili,Watanzania ipo siku wataamuka na kutambua haki zao;mtoaji uzi huu anaelewa kuwa our no 1 ana madaraka makubwa mno including to over run mihimili mingine ya utawala bora;Mr.Mayala unaelewa kuwa NEC yetu haipo huru(na hii sio rocket science kutambua hilo);Mr.Mayala unaelewa kuwa human rights ndani ya nchi yetu haipo(refer uchangiaji wako kuhusu watuhumiwa kudhalilishwa wakati bado ni suspects);Mr.Mayala unatambua kuwa wanasiasa wana nguvu mno kuliko mahakama our own RC wa DSM amelithibitisha hili few hours ago kwa kusimamisha ubomoaji wa nyumba na amri yake watu wametii ILA ile ya mahakama pale Kimara ilipuuzwa;tatizo kubwa kwetu tunapokuwa kwenye ofisi zetu zenye AC,fridge,computers etc etc tunasahau wenzetu pale LINGUSENGUSE muda huu wengi wao hawajui what time they will have their next meal,its a sad day kwangu kwa mmoja wa role model wangu kuja na mada kama hii,but history always itakuja kurekebisha haya na kutuhukumu.SHAME ON US labda MUNGU katupa too much mpaka tunajisahau tunaishi kwenye nchi yenye changamoto nyingi mno,angalia haya ya AJIRA YA TRA NI HUZUNI KUBWA MNO.
 
Kuna wakati ukimsilikilza pasco unaweza jua ana upeo mkibwa wa kufikiri , huku kwetu watu wa aina hiyo tunawaita wenye GB kubwa . Lakn kumbe mayalla uwezo wake ni kb tu kichwani. Kitendo cha katika kuita kipande cha karatas kimeondoa mazuri yoote kwangu. Anasahau katika iko badala ya watu million 50. Mawazo yao ndio yakazalisha hicho anachokiita kikaratas. Katika ikisimama limesimama Taifa zima. Usipotii katiba hujawatii unaowaongoza.

Pls jitambue unapoandika
 
Pasco,
Kwanza nikiri wazi kwamba huwa naheshimu sana maoni ya watu. Pili huwa nafuatilia na kuvutiwa na hoja zako nyingi hapa jukwaani! Ila niseme ukweli leo umeongea kijinga sana kwenye hii hoja! Nasema kijinga kwa sababu bado unaweza kujielimisha,kuelimishwa na ujinga wako ukaondoka!
Tanzania hatufanyi uchaguzi eti kwa sababu Nchi haina uongozi mzuri ama kwa sababu hakuna kiongozi shupavu. Mpaka sasa anachokifanya magufuli sio kitu kigeni,kiliwahi kufanywa huko nyuma na waliomtangulia lkn bado tulilazimika kuingia ktk uchaguzi! Tulikuwa tunafanya uchaguzi tukiwa na mfumo wa chama kimoja, leo tunao mfumo wa vyama vingi unakuja na mawazo ya kijinga namna hii?
Kati ya wakati huu na wakati wa uongozi wa Mwl Nyerere ni wakati upi ulikuwa muafaka wa kufuta uchaguzi?
Mawazo yako nayaona kama ni matokeo ya athari za uongozi mbovu wa CCM ya baada ya Mwl Nyerere! Watu walikuwa wamepoteza aina ya uongozi shupavu wa Nchi unavyopaswa kuwa! Leo Magufuli anaoneka kama katoka peponi!
Pasco umesahau kwamba Magufuli anatoka katika mfumo ule ule ulioyalea matatizo tuliyonayo? Hivi sio Rais wetu huyu aliyekuwa anasimamia Wizara iliyokuwa inanunua vivuko vibovu? Umesahau nini? Nashauri tusijisahu.
Unafahamu kwamba kwenye dunia hii kuna Nchi hazijui maana ya ufisadi,hazijui watu wanaokwepa kodi,hazijui kama kuna watu wanaolala chini hospitalini, hazijui kama kuna sehemu watu wanashindia mlo mmoja kwa siku, hazijui kama kuna watoto wanakaa chini shuleni n.k, lkn bado Nchi hizo zinafanya uchaguzi kama takwa muhimu katika kukuza Demokrasia na kuleta Maendeleo ya kweli katika Nchi zao?
Tanzania tuna nini cha kujivunia mpaka sasa? Dakika 10 tu za Magufuli Ikulu watu mnakuja na mawazo ya kutaka tuondoe uchaguzi wa Rais?
Umeandika hoja zako ukiwa na akili timamu ama una mihemko ya kutoujua ukweli?
Umefanya makusudi ama ndo akili yako imekuongoza hivyo leo? Siamini kama ni wewe!
Tanzania Tunaizidi nini Nchi ya Norway? Tunawazidi nini Denmark? Hizi ni Nchi zilizo na kila kitu anachohitaji kuwa nacho Raia katika Nchi yake! Ni Nchi ambazo hazina ujinga wa ufisadi! Mpaka sasa wao wanatupatia misaada kibao lkn still wanafanya uchaguzi kila inapofika wakati!
Sisi tuna nini?
Jisahihishe uache ujinga!
Tumpongeze Rais Magufuli kwa kufanya kile walichoshindwa kukifanya wengine, hata kama nae alikuwa sehemu ya uongozi mbovu uliopita, lkn tuache mawazo ya kijinga na hatari kwa ustawi wa Nchi yetu!
Ubarikiwe ndugu yangu . . , inaelekea wewe ni Mwalimu . . [emoji106] [emoji106] [emoji106]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wengine labda watakuona queer, lakini sio Mimi:
1. Katiba haiandikwi kwa ajili ya MTU mmoja au kizazi kimoja tu. Katiba lazima izingatie maslahi ya nchi ambayo ni mapana zaidi ya uchaguzi mmoja uliomweka rais madarakani.

2. Uchaguzi huru na wa haki hatujawahi kuushuhudia hapa kwetu, wewe wajua. Na hili so lawama au credi kwa mtu au chama bali kwa mfumo mzima.

3. Katiba sio "kipande cha karatasi" kama wewe unavyoelewa! Katiba ni sheria, tena ni mama wa sheria zote, ni falsafa, ni mwongozo, ni mila etc. na si lazima iwe written eg.: (UK constitution)
Ukiiona katiba kama kipande cha karatasi kamwe hutaiheshimu na hutaheshimu sheria nyingine zote.

4. Rais ni taasisi, sio MTU. JPM ni binadamu, na we we unajua maumbile ya binadamu; hatuko perfect. Inaonekana mwenzetu hutofautishi vitu hivyo viwili kwa sababu zako.

5. Sio busara kubadili au kufuta Katiba kwa faida ya MTU mmoja au kikundi kimoja cha watu (chama). Katiba ndio msingi wa Mihimili mitatu ya Utawala (DOLA). Katiba ndio kielelezo cha mipaka ya mamlaka ya Bunge, Mahakama na Serikali. Katiba ya nchi ni zaidi ya vitu mnavyoita "TUNU" kmf. Kiswahili. Leo nikisema kiswahili kimedumaza elimu yetu mtasemu siheshimu tunu za taifa! lakini Katiba ya nchi mnaiita "kipande cha karatasi" Hiki ni kiroja.

6. Kwahiyo ukibadili au kufuta Katiba kwa faida ya MTU mmoja (sio taasisi)!!! matokeo yake umefuta mamlaka ya mihimili mitatu ya DOLA. Maana yake unasimika UDIKTETA. Na kuna udikteta wa MTU mmoja na wa kikundi cha watu, vyote ni haramu.

7. Mfano: Huwezi kumfanya jaji wa mahakama asifuate tena sheria, eti kwasababu umeshinda kesi au alifuta kesi yako!
Huwezi kusema eti: 'Kwasababu Bunge limetunga sheria nzuri tusiwe na uchagizi wabaki wabunge hawahawa mpaka lini sijuwi!! Dunia itawashangaa.

9. Swali unalowauliza wapinzani ungewauliza CCM kwanza kama wako tayari kuendesha uchaguzi ulio huru na wa haki na kuwapa wapinzani Serikali iwapo watashinda kihalali? Kwasababu wapinzani hawatumii polisi ili washindwe kila uchaguzi. Bali siku zote mwenye nguvu ya dola ( incumbent); asiyeheshimu katiba, akiona mambo yake hayaendi anavyotka yeye hutumia nguvu.

Kwa hayo machache naishia hapo. Umeleta mada nzuri, ila kama lugha yangu imekukwaza kwa namna yoyote niwie radhi baba.
Mkuu Shoctopus, kwanza asante kwa objectivity yako kwenye bandiko hili.
Thanks nitazingatia hoja zako.
P
 
1. Watu wanabadilika. Madaraka hulevya haswa yanapo kosa ukomo, Kama ambavyo pesa tu hubadilisha watu. Mugabe, Museveni, Iddi Amin, na viongozi wengi waliogeuka kuwa madikteta walianza kwa kupendwa sana na wananchi.

2. Binadamu wote tumeumbwa tukiwa na madhaifu, sheria zipo kwa ajili ya kutulinda na madhaifu yetu. Na sheria kuu kiliko zote ni katiba. Katiba ndo imeweka mipaka inayo mfanya kila mtu aishi kwa kujiamini kwamba utu wake, haki zake na mali zake zinatambulika na kulindwa. Haya ndo kiini cha ubinaadamu na utofauti wetu na wanyama. Mnyama hana mke, mtoto, mali, wala haki yoyote anayoweza kuitetea. Katiba inatupa utu wetu.

3. Afrika kusini na marekani enzi za ubaguzi wa rangi waliendelea sana kiuchumi. Barabara zilikuwa nzuri, hospitali nzuri, shule nzuri...lakini utu wa mtu mweusi haukuwepo. Watu weusi walionekana sawa na wanyama tu na wala hayo maendeleo hayakuwanufaisha. Bila utu wako maendeleo hayana maana. Tetea utu wako kwanza, kwa kutetea katiba inayo linda utu huo, kabla ya kutetea maendeleo.

4. Wananchi wanaojitambua hawawezi kuruhusu katiba inayo linda haki zao kukanyagwa, maana kufanya hivyo ni kuruhusu utumwa tena.

5. Leo tunamshangilia Raisi Magufuli kwa mazuri anayoyafanya, kama waZimbabwe walivyomshangilia Mugabe akitwaa mashamba ya wazungu na kuwagawia wazawa. Ni vema kuwapongeza na kuwashangiliwa. Lakini tujiulize, je raisi akija kubadilika asiwe huyu tunaye mjua leo, je na sisi tutahama nchi kama wanavyofanya waZimbabwe.

6. Ndio maana upo umuhimu wa ukomo wa kutawala. Kabla mtu hajalevya na madaraka, anaachia ngazi na kutawala mwingine. Na kwa kubadilishana huko madaraka, hata raisi anavyo tawala, anatawala akijua mamlaka yake yana ukomo.

7. Tusitake miungu wa duniani. Tusikubali kuamini kwamba mtanzania mzalendo mwenye uwezo wa kuongoza yupo mmoja tu, na hatokuja kutokea mwingine. Hizo ni fikra za kitumwa na kikoloni. Hizo ni fikra za kuuza utu wetu wenyewe, na kujiacha uchi kama wanyama pasipo na kinga ya sheria yeyote.

8. Namkubali sana mh. Raisi John Pombe Magufuli kwa utendaji wake mzuri na namuombea aweze kuongoza vizuri kwa mda anaoruhusiwa kikatiba. Napinga kwa nguvu zote, kuikanyaga katiba, wala kujiweka juu ya katiba, wala kuidharau, au kuibadilisha kwa lengo la kujipa mamlaka zaidi au kujiongeza mda wa kutawala. HAKUNA MWANADAMU ALIE JUU YA SHERIA.
 
damu itamwagikaaa haitawezekana mwizi aharibu katibaaa patachimbikaaaaaaaaaaa hapaaaaaaa wasituone tumenyamaza
 
Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sasa, sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja kweli ya kufanya tena uchaguzi wa rais?, si tumwache tuu aendelee mpaka pale tutakaapoona tumetosheka?.

1. Pamoja na ukanyagaji wake wa katiba ya nchi, lakini kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuinyoosha nchi hii iliyopinda kupindukia kwa rushwa, uzembe na ufisadi, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya uchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tuu aendelee mpaka 2025? na kama bado anatosha, aendelee tuu?.

2. Jee hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, na kumwacha Magufuli kupita bila kupingwa, ili kuokoa muda, pesa na mali?, hivyo Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025 and beyond?.

3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike kwa mujibu wa katiba, hata kama uchaguzi huo ni wastage of time, money and resources?!. Kwani katiba ndio nini hata iheshimiwe hivyo?.

4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.

5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, ingekanyagwa kirahisi rahisi na kupuuzwa, huku watu wakiangalia tuu?, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.

6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.

8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, , Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?.

9. Na baada ya katiba kukanyagwa, kwa mikutano ya siasa kuzuiwa, jee kuna ubaya wowote kama wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, haswa kwa kuzingatia the playing field is not level, na badala yake CCM tuu ndio iwe pekee inatoa mgombea urais siku zote kufuatia long eksipirience ya uzoefu wa muda mrefu wa CCM wa kumtoa rais ambaye siku zote huchaguliwa kwa ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huru na wa haki?.

10. Na kufuatia somo la demokrasia ya Kiafrika, na mfano hai wa matokeo ya urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea urais wa kushindana na mgombea wa chama dola, CCM?, yaani by now tumeishajua mgombea wa CCM kwa 2020 ni Magufuli?, kuna chama kiko tayari kumteua mgombea wake kushindana na Magufuli ambaye ni a sitting president, huku kutakuwa ni kugombea au kujifurahisha tuu?!, au hata ikitokea huyo mgombea wa upinzani ameshinda atatangazwa?!.

Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.

Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Paskali
Habari za wakati huu mkuu pascal?

Ningependa kukwambia kuwa haja ya kufanya uchaguzi mwaka 2020, IPO. .

Sababu ni hizi hapa

1. Uchaguzi wa kila baada ya miaka mitano upo kikatiba. Hautafanyika endapo katiba itabadilishwa

2. Tanzania ni nchi ya demokrasia. Mnamo mwaka 1992, walikubaliana kuachana na Sera ya ujamaa na kuamua kutumia Sera ya ubepari. Na wakaamua kujiwekea awamu ya uongozi bila kupima uwezo wa uongozi

Kwahiyo napenda kukwambia kuwa haja ipo kwakua Tanzania inaendeshwa kwa katiba. Kwahiyo hayo yote anayoyafanya mh rais, anayafanya kwa mujibu wa katiba na si utashi wake
 
Tatizo kwa miaka zaidi ya 30 tulilia mtu wa aina hii ya Magufuli, issue itakuwa kupata mbadala wa kuendeleza
 
Hili swala lipo kila baada ya miaka mitano walioliamua hilo hawakuwa wajinga waliiona sababu.

Yeye mwenyewe ameshasema hii kazi ni ngumu au imekuwa tamu kwake.

Mimi naona kuna watu anawahofia huku chamani kwa huu hiyo anafanya hivyo ili aoteshe mizizi vizuri lakini atafanikiwa kwa hili naona ngumu
 
Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sasa, sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja kweli ya kufanya tena uchaguzi wa rais?, si tumwache tuu aendelee mpaka pale tutakaapoona tumetosheka?.

1. Pamoja na ukanyagaji wake wa katiba ya nchi, lakini kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuinyoosha nchi hii iliyopinda kupindukia kwa rushwa, uzembe na ufisadi, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya uchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tuu aendelee mpaka 2025? na kama bado anatosha, aendelee tuu?.

2. Jee hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, na kumwacha Magufuli kupita bila kupingwa, ili kuokoa muda, pesa na mali?, hivyo Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025 and beyond?.

3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike kwa mujibu wa katiba, hata kama uchaguzi huo ni wastage of time, money and resources?!. Kwani katiba ndio nini hata iheshimiwe hivyo?.

4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.

5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, ingekanyagwa kirahisi rahisi na kupuuzwa, huku watu wakiangalia tuu?, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.

6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.

8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, , Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?.

9. Na baada ya katiba kukanyagwa, kwa mikutano ya siasa kuzuiwa, jee kuna ubaya wowote kama wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, haswa kwa kuzingatia the playing field is not level, na badala yake CCM tuu ndio iwe pekee inatoa mgombea urais siku zote kufuatia long eksipirience ya uzoefu wa muda mrefu wa CCM wa kumtoa rais ambaye siku zote huchaguliwa kwa ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huru na wa haki?.

10. Na kufuatia somo la demokrasia ya Kiafrika, na mfano hai wa matokeo ya urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea urais wa kushindana na mgombea wa chama dola, CCM?, yaani by now tumeishajua mgombea wa CCM kwa 2020 ni Magufuli?, kuna chama kiko tayari kumteua mgombea wake kushindana na Magufuli ambaye ni a sitting president, huku kutakuwa ni kugombea au kujifurahisha tuu?!, au hata ikitokea huyo mgombea wa upinzani ameshinda atatangazwa?!.

Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.

Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Paskali
Sasa najua una maoni tofauti
 
Ni hapa tu nawashangaa Watanzania wenzangu na hasa wewe mtoa mada...eti akiendelea Hivi, Mnaweza Kushangaa 2020 Watanzania Wakaamua Kuokoa Gharama na 2025 Tukabadili Katiba Kuondoa Ukomo. Bila shaka umesahau kwamba Katiba yetu kwa sasa inategemea Magufuli kaamkaje, kama kaamka na kisirani ole wetu, hamna cha Katiba, hamna cha sheria...ni wananchi kuumia, kutekwa, kuteswa na kupigwa risasi zisizo na hesabu.

Pascal Mayalla, naomba nikuulize, ni Katiba gani hiyo unayoiongelea? Hivi kweli unao ujasiri wa kusema tuna Katiba! Siyo wewe uliyedai kuwa kwa nia yake nzuri kwa taifa unamsamehe hata akivunja Katiba! Katiba inayovunjwa jinsi kiongozi anavyopenda si Katiba. Hakuna kinachomzuia Magufuli kuondoa ukomo na usitudanganye kwamba eti hadi Katiba ibadilishwe...I am sure you are not serious, unatuvika tu kilemba cha ukoka.

Hatuwezi kushangaa ukomo kuondolewa kama ambavyo hushangai Katiba ikivunjwa na wewe Pascal Mayalla huoni tatizo. Mimi msimamo wangu uko pale pale na hautetereki...kiongozi akishavunja Katiba sina cha kupongeza, kupongeza ni kubariki uhalifu na hakuna popote kwenye Katiba uhalifu umeruhusiwa. Kwa kuamua kumsifia sina la nyongeza, hauko peke yako, mko wengi ambao kwenu Katiba si chochote si lolote...nawatakia heri!
Mkuu Mag3, baadhi ya hoja zako zimejibiwa humu.
P
 
Serious!!!!??? Mayala huyu huyu aliyetajwa na Mhe. Sikuile? Kwa hiyo hata katiba ikikanyagwa kwa mwamvuli wa kurekebisha mambo ni sawa tu? Kwa kauli yako hiyo mbona rais aliyepita na wengine walikuwa zaidi yake kiuchapakazi na yeye akiwa ndani yake? Eti aachwe tu apite mwaka 2020, kwani ni yeye tu pekee ndiye mwenye akili za kuongoza Tanzania, wengine hawana uwezo? Kwanini tukubali kuwa na mtu anayekanyaga katiba na kuitia mfukoni mihimili mingine halafu tushangilie kuwa ni mchapakazi wakati tunaoathirika ni wananchi wengi kwa vitendo vyake? Mayala haupo serious sana, labda na wewe uwe unajipigia debe ukumbukwe. Tumia kalamu yako kwa manufaa ya wengi, acha ubinafsi
 
Back
Top Bottom