Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Hili ni bandiko la swali na swali hili bado liko valid, hata baada ya hili la kikokotoo, bado 2020 kunahitajika uchaguzi wa rais, au Magufuli aendelee tuu hadi 2025?, and may be more?.
P
Uchaguzi nilazima kk tena waanze na kura zao zamaoni tuone ccm kama wanapenda udhulumati wa kudhulumu wavuvi ziwa tanganyikal na wakulima wa korosho kama ccm wengine hawapendi dhuluma wamchomoe haraka 2020 aondoke
 
Mkuu Mbazi TZ, hata kama ulikuwemo kwenye cabinet for the past 20 years, kwa mfumo wa katiba yetu, the role of cabinet ni advisory body and not decision making body, hivyo cabinet inamshauri tuu rais, lakini kufikia maamuzi, rais ataamua yeye mwenyewe bila kushurutishwa kufuata ushauri wa yeyote, maamuzi ya rais toka ndani ya cabinet, huchukuliwa as a collective responsibility, hivyo hata kama waziri fulani alikataa jambo fulani ndani ya cabinet, likiishapitishwa, ni wote wamekubali na majadiliano ya cabinet ni confidential, hivyo msimtegemee rais Magufuli ajitokeze aseme alipinga nini ndani ya miaka hiyo 20, ila wenye uelewa mpana, wanamuongalia jinsi anavyofumua madudu, then unajua hata alipokuwa mmoja wao, msimamo wake ulikuwaje.

Wengi wamejikita kwenye la kikokotoo tuu, lakini kubwa jingine ni kurejesha fao la kujitoa.

P.
 
Swali la kujiuliza ni kuna haja gani ya kuwa hata na chaguzi ilhali tunajua kabisa mwisho wa siku CCM ndo atatangazwa mshindi?

Una maanisha kua USHINDI hautokani na wapiga kura ila watakaohesabu ?
Lkn kumbuka tuna wabunge wengi wa upinzani Bungeni[emoji4]
 
Uchaguzi ufanyike kwa mujibu wa katiba hata kama atarudi yeye ila isiwe kwa kukiuka katiba inayoelekeza chaguzi kila baada ya miaka mitano. Hatuongozwi na malaika hivyo ni lazima misingi ya katiba ilindwe na kuheshimiwa
 
Duh aisee unazeeka vibaya!
 
Tena nashauri miaka yake kumi ikiisha wananchi waulizwe,wakikubali apewe vipindi vingine viwili vya miaka mitano mitano.Tunataka kizazi cha mafisadi kibadilishwe mindset.
Mkuu areafiftyone, katika bandiko hili nilishauri kitu kama hiki, leo tumeshuhudia jiwe la msingi la mradi wa Stigler, SGR inaendelea, Flyover zinaendelea, midege ndio hiyo inapaa kuzunguka dunia, mabarabara ndio usiseme, madini mkataba unasainiwa anytime from now, etc etc, kweli 2020 kuna haja ya kufanya uchaguzi wa rais?.

P
 

Wasomi wa sheria wanafahamu zaidi umuhimu wa yaliyomo kwenye katiba na sheria. Ukiona wasomi hao ghafla wanashadadia matendo tofauti na matakwa ya katiba na sheria, jua kuna dosari tayari-usomi ushahamia tumboni au kwenye maslahi mengine. And they don't care how they sound or look any more. Pity!
 
Sio kuwa hamna haja ya uchaguzi tu ikiwezeka kizazi chake chote kiongoze Tanzania mapaka yesu arudi
 
Usitutafutie ban humu ndani nitakupa kubwa kuliko
 
Bila unafiki kutoka rohoni apige kama baba wa taifa hili naona nia njema aliyonayo ya kutupereka tunakotajia naunga mkono hoja.
Hili ni bandiko la swali na swali hili bado liko valid, hata baada ya hili la kikokotoo, bado 2020 kunahitajika uchaguzi wa rais, au Magufuli aendelee tuu hadi 2025?, and may be more?.
P
 
Kuna watu wanaitwa mafarisayo, masadukayo na kuna watu wa mataifa. Mafarisayo na masadukayo hawa ni watu wanaoishi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, halafu watu wa mataifa, wao wanaishi kwa kufuata ukweli halisi wa kile kilichopo.

Ni kweli katiba, sheria, taratibu na kanuni zinaelekeza uchaguzi wa rais ufanyike kila baada ya miaka 5. Lakini uzoefu unaonyesha haijawahi kutokea a sitting president akashindwa kwenye uchaguzi wa awamu yake ya pili, kwasababu ni uchaguzi wa kugombea kisu huku mmoja ameshika kwenye mpini, kitu kinachoufanya uchaguzi huo kuwa ni igizo tuu la uchaguzi.

Sisi watu wa mataifa tumeuliza why do we have to spend all this money kufanyia igizo la uchaguzi wakati rais bora tayari tunaye and he does wonders?.

Kwa mtu anayeelewa the political dynamics za siasa zetu, 2020 kuna mtu wa kushinda na Magufuli?.



2020 kwenye urais, lets save, time, money and resources, Magufuli aendelee tuu
P
 
haina haja kusema kweli, mtu kama Magufuli utamsimamisha na nani ambaye anaweza akawa na nguvu ya ushawishi hata kufikia robo ya kura zake?
jamaa kazi anafanya hata wanaopinga ni viletu wamezoea kuongea ila hata roho zao nina imani zina wasuta
 

Hivi kwa nini mkuu hakumwana pascal? Nafikiri bado teuzi zinaendelea, mkuu mkumbuke pascal kwenye ufalme wako, maana yawezekana akaja mkuu mwingine hasiyefahamu umuhimu wake kwako.
 
Sio kuwa hamna haja ya uchaguzi tu ikiwezeka kizazi chake chote kiongoze Tanzania mapaka yesu arudi
Mkuu Lendila, sio kizazi chake maana Tanzania sio nchi ya kisultani au kifalme ila ni ukweli usiofichika kuwa kuna makabila ya majembe kazi, wenye bidii na wachapa kazi na kuna makabila ni wavivu na wapiga soga, hivyo nimeisha pendekeza rais wa JMT atokane na makabila wachapa kazi.


P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…