Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Hivi Hiujiulizi kitu gani kilimzuia Nyerere kujenga flyover ? Ni kitu gani kilimzuia kubomoa jengo la Tanesco ? Ni kitu gani kilimzuia mkapa kujenga Double road hadi kusini ;akajenga single ! Ni kitu gani kilimzuia Mwinyi kujenga daraja la salenda akajenga Single road nyingi mikoa mbalimbali ! NI KITU GANI KILIMDANGAYA JAKAYA Akaanza kuunganisha kwanza Makao makuu ya mikoa na wilaya kwa Barabara; badala ya kuanza na Kijiji kwa kijii ?.Kila mtu akajenga juu ya msingi wa mwenzake ! Acheni kumchafua Mheshimiwa aonekane chema Chajiuza kibaya chajitembeza,;Ni kitu gani kiliwamzuia kutokwepa Uchaguzi ? Tumsaidie aongoze Nchi na kutawala Taifa; badala ya kutawala nchi na kuongoza taifa; hiyo ndiyo tofauti ya awamu zingine
 
Hata kama rais magufuli ameleta maendeleo makubwa vipi,hatuwezi kumshindanisha na mtanzania mwingine kwa kuleta maendeleo pia?
 
Mkuu areafiftyone, katika bandiko hili nilishauri kitu kama hiki, leo tumeshuhudia jiwe la msingi la mradi wa Stigler, SGR inaendelea, Flyover zinaendelea, midege ndio hiyo inapaa kuzunguka dunia, mabarabara ndio usiseme, madini mkataba unasainiwa anytime from now, etc etc, kweli 2020 kuna haja ya kufanya uchaguzi wa rais?.

P
Pascal I support you 100%.Rais wa aina ya JPM is what we needed,what else.Referendum ipite,wananchi wakiafiki,kitu ambacho sidhani kama kuna mtu "in his own mind"(ambaye hakushikiwa akili) atakaye kataa.Mimi nasema hata ikibidi katiba ibadilishwe,ingawa this is going a little bit too far.Mwanadamu ni mwanadamu anaweza kubadilika.
 
Hakuna haja ya kuharibu pesa ambazo zingefanya maendeleo mengine kwa kufanya uchaguzi mwingine wakat huyu aliepo anatufaa kuendelea naunga mkono Magufuri aendelee kuwa rais wa nchi yetu kwa miaka 30 mbele ili nchi inyooke na ipige hatua kimaendeleo na kuufikia uchumi wa kati na usiotegemea msaada ya mabeberu wanatuibia mali zetu kama walivofanya kwenye awamu ya 5 na 4 kama kupandisha wanyama wetu kma twiga, nk. Labda tufanye uchaguzi wa madiwani na wabunge tu rais mh Magu anatosha sana.
 
Mkuu Lendila, sio kizazi chake maana Tanzania sio nchi ya kisultani au kifalme ila ni ukweli usiofichika kuwa kuna makabila ya majembe kazi, wenye bidii na wachapa kazi na kuna makabila ni wavivu na wapiga soga, hivyo nimeisha pendekeza rais wa JMT atokane na makabila wachapa kazi.


P

🤣🤣🤣🤣


Kwani mkuu wewe ni wa kabila lipi?

Kusema kabila flani ndo wachapa kazi kwa hiyo wapewe madaraka ilhali anaedai hivyo ni mmoja wa makabila hayo, ni namna fulani ya kutetea au kuunga mkono hoja flani haramu.

Kwanza si kweli kwamba makabila hayo mengine siyo wachapakazi at all. Ila ni mtizamo wa watu flani na "naked" conclusions zao ambazo haziko dressed na tafiti zozote ya kisayansi (social or otherwise).

Walio wengi haijawahi kumaanisha wote, na walio wachache haijawahi kumaanisha hawapo kabisa hata mmoja. Hivyo basi kusema atoke kabila flani tuu kwa sababu wengi wao ni wachapa kazi, equates to reckless generalization. Na pili, mtu atawezaje kutofautisha mtizamo huu na mwanzo wa ukabila na au mwendelezo wa kuuchagiza? Na la kustaajabisha kwenye karne hii, to what end?
 
Mkuu areafiftyone, katika bandiko hili nilishauri kitu kama hiki, leo tumeshuhudia jiwe la msingi la mradi wa Stigler, SGR inaendelea, Flyover zinaendelea, midege ndio hiyo inapaa kuzunguka dunia, mabarabara ndio usiseme, madini mkataba unasainiwa anytime from now, etc etc, kweli 2020 kuna haja ya kufanya uchaguzi wa rais?.

P
Nilicho gundua kwako Pascal ni kuwa unapoona unawaudhi watu basi ndio roho yako inaburudika sana!
Mumefanana sana kwa hilo na kaka yako.
 
Kuna watu wanaitwa mafarisayo, masadukayo na kuna watu wa mataifa. Mafarisayo na masadukayo hawa ni watu wanaoishi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, halafu watu wa mataifa, wao wanaishi kwa kufuata ukweli halisi wa kile kilichopo.

Ni kweli katiba, sheria, taratibu na kanuni zinaelekeza uchaguzi wa rais ufanyike kila baada ya miaka 5. Lakini uzoefu unaonyesha haijawahi kutokea a sitting president akashindwa kwenye uchaguzi wa awamu yake ya pili, kwasababu ni uchaguzi wa kugombea kisu huku mmoja ameshika kwenye mpini, kitu kinachoufanya uchaguzi huo kuwa ni igizo tuu la uchaguzi.

Sisi watu wa mataifa tumeuliza why do we have to spend all this money kufanyia igizo la uchaguzi wakati rais bora tayari tunaye and he does wonders?.

Kwa mtu anayeelewa the political dynamics za siasa zetu, 2020 kuna mtu wa kushinda na Magufuli?.



2020 kwenye urais, lets save, time, money and resources, Magufuli aendelee tuu
P


Mkuu kwa thinking behind hoja yako hii ya a sitting president, the moment ukiielekeza kwenye chaguzi zote since the dawn of multipartism, hajawahi kushinda mgombea wa chama chochote cha tofauti. Then utarealize may be we have had a much bigger problem. Kumbe hakukuwa na haja ya chaguzi za vyama vingine kushiriki... So siyo tatizo la kuelekea 2020, unless mtu au watu wanataka kulitumia now kama tatizo jipya, kwa maslahi flani.

Chanzo cha tatizo hilo ni nini? Ni kukubalika kwa chama X na vyama vingine kutokukubalika? Au design ya system na process ya uchaguzi haviko "democratic" to begin with, ili kuweza kutoa democratic outcome? Ni vyama havina resources shindani? Maswali ni mengi.
 
Wakati wa mwalimu uchaguzi ni kila baada ya miaka mitano ingawa mgombea alikuwa ni yeye mwenyewe...ili kutimiza matakwa ya katiba.
Wasomi wa sheria wanafahamu zaidi umuhimu wa yaliyomo kwenye katiba na sheria. Ukiona wasomi hao ghafla wanashadadia matendo tofauti na matakwa ya katiba na sheria, jua kuna dosari tayari-usomi ushahamia tumboni au kwenye maslahi mengine. And they don't care how they sound or look any more. Pity!
 
Wanabodi.


2. Jee hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, na kumwacha Magufuli kupita bila kupingwa, ili kuokoa muda, pesa na mali?, hivyo Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025 and beyond?.

3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike kwa mujibu wa katiba, hata kama uchaguzi huo ni wastage of time, money and resources?!. Kwani katiba ndio nini hata iheshimiwe hivyo?.

4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.

5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, ingekanyagwa kirahisi rahisi na kupuuzwa, huku watu wakiangalia tuu?, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.

6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.

Paskali
Naona waweza kuwa una nia njema na nchi hii, ila
Tujihadhali na kutengeneza katiba ya mtu na tusifurahie watu waliosigina katiba. Hivi tukibadili katiba kwa kuwa tunaye rais safi JPM, je akikaribia kuondoka tunatunga nyingine au tunamwangalia kwanza atakayefuata then tunaamua kuibadili tena?, Kama kunaweza kuwa na maandalizi ya yeye kuondoka then akatusaidia tukabadili katiba kabla hajaondoka then ni vizuri. Lakini je ikitokea mwenyezi Mungu akamwita ghafla akaja mwingine akakuta katiba iliyompa rais madaraka makubwa akamua kuyatumia vibaya, tutakuwa wageni wa nani? Kumbuka madaraka tuliyompa Nyerere mtu muadilifu, waliomfuata waliyatumiaje? Kumbuka madaraka tulimpatiga Gavana wa benki kuu Nyirabu - waliofuatia waliyatumiaje?
Mimi nadhani ni muhimu hivi anavyotenda JPM viwekewe misingi ya kikatiba kiasi kwamba yeyote atakayekuja kutawala asiweze kuvuruga. Cheki Marekani Trump anavyodhibitiwa!
Katiba haitamtaja JPM bali itamtaja rais - iweze kumbana yeyote atakayepata title hiyo afanye kama JPM kikatiba. Atajenga viwanda na kununua madege atakuja mwingine ataviuza kwa fedha kiduchu (walifanya hivyo hivyo baada ya Nyerere). Atajenga reli ya kisasa, hata baada ya miaka 50 atakuja mwingine atajiuzia! nk.
 
Vitu ambavyo raisi wa sasa anavifanya ni kutekeleza ilani ya CCM, isipokuwa ule upendeleo pekee anaoufanya kwa kuindeleza Chato, vile vile nao wanastahiki maendeleo kwa kuwa ni watanzania pia. Kwa kweli uchaguzi ni lazima kwa kuwa ni jambo la kisheria, kama tungetaka kuokoa pesa tungetafanya wakati ule wa chama kimoja na myombea mmoja wa uraisi, lakini bado tulikuwa tuna piga kura. Huo uoga wa raisi kuendelea kutawala bila ya uchaguzi usiwepo, ikiwa ni kweli utawala wake unakubalika na watanzania wengi basi atapita kwa utawala wa awamu nyingine na kama hakubaliki basi atatutwe mwenye kukubalika ambaye atapata ridhaa ya watanzania katika kuwapeleka katika hali bora ya maisha. Watanzania wengi tunakubali kuwa raisi Magufuli ameleta maendeleo na anajitahidi kusimamia rasilimali za nchi, lakini mpaka sasa tunaona maendeleo yenyewe ni ya VITU na si ya WATU, hapo ndipo kwenye mashaka je aendelee kuleta maendeleo ya vitu lakini watu tuwe hatuna maendeleo kwa miaka mitano ijayo??????
 
Mjomba Pascal! Mimi Napenda Kukuitaga Mj Pasco Mbona Unaenda Lesi Sana Vipi Nawe Unataka Ukuu Wa Wilaya Au Mahaba Yako Maana Duh Mpaka Unataka Uchaguzi Usiwepo Tena Ha Ha Ha Ha Ha Shikamoo Njaa
 
Hakuna haja ya kuharibu pesa ambazo zingefanya maendeleo mengine kwa kufanya uchaguzi mwingine wakat huyu aliepo anatufaa kuendelea naunga mkono Magufuri aendelee kuwa rais wa nchi yetu kwa miaka 30 mbele ili nchi inyooke na ipige hatua kimaendeleo na kuufikia uchumi wa kati na usiotegemea msaada ya mabeberu wanatuibia mali zetu kama walivofanya kwenye awamu ya 5 na 4 kama kupandisha wanyama wetu kma twiga, nk. Labda tufanye uchaguzi wa madiwani na wabunge tu rais mh Magu anatosha sana.
Mkuu Bujoro, haya ndio maneno ya wazalendo wa kweli wa nchi yetu wenye uchungu na umasikini wetu, hivyo kuokoa fedha japo kidogo kuliko kuzitumia kufanyia maigizo.

P
 
Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sasa, sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja kweli ya kufanya tena uchaguzi wa rais?, si tumwache tuu aendelee mpaka pale tutakaapoona tumetosheka?.

1. Pamoja na ukanyagaji wake wa katiba ya nchi, lakini kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuinyoosha nchi hii iliyopinda kupindukia kwa rushwa, uzembe na ufisadi, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya uchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tuu aendelee mpaka 2025? na kama bado anatosha, aendelee tuu?.

2. Jee hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, na kumwacha Magufuli kupita bila kupingwa, ili kuokoa muda, pesa na mali?, hivyo Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025 and beyond?.

3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike kwa mujibu wa katiba, hata kama uchaguzi huo ni wastage of time, money and resources?!. Kwani katiba ndio nini hata iheshimiwe hivyo?.

4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.

5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, ingekanyagwa kirahisi rahisi na kupuuzwa, huku watu wakiangalia tuu?, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.

6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.

8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, , Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?.

9. Na baada ya katiba kukanyagwa, kwa mikutano ya siasa kuzuiwa, jee kuna ubaya wowote kama wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, haswa kwa kuzingatia the playing field is not level, na badala yake CCM tuu ndio iwe pekee inatoa mgombea urais siku zote kufuatia long eksipirience ya uzoefu wa muda mrefu wa CCM wa kumtoa rais ambaye siku zote huchaguliwa kwa ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huru na wa haki?.

10. Na kufuatia somo la demokrasia ya Kiafrika, na mfano hai wa matokeo ya urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea urais wa kushindana na mgombea wa chama dola, CCM?, yaani by now tumeishajua mgombea wa CCM kwa 2020 ni Magufuli?, kuna chama kiko tayari kumteua mgombea wake kushindana na Magufuli ambaye ni a sitting president, huku kutakuwa ni kugombea au kujifurahisha tuu?!, au hata ikitokea huyo mgombea wa upinzani ameshinda atatangazwa?!.

Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.

Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Paskali

Mayalla wewe ni Msukuma kwa hiyo sishangai kuona unaleta hoja ya kipuuzi namna hii.
 
Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sasa, sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja kweli ya kufanya tena uchaguzi wa rais?, si tumwache tuu aendelee mpaka pale tutakaapoona tumetosheka?.

1. Kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuinyoosha nchi hii iliyopinda kupindukia kwa rushwa, uzembe na ufisadi, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya uchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tuu aendelee mpaka 2025? na kama bado anatosha, aendelee tuu?.

2. Jee hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, na kumwacha Magufuli kupita bila kupingwa, ili kuokoa muda, pesa na mali?, hivyo Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025 and beyond?.

3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike kwa mujibu wa katiba, hata kama uchaguzi huo ni wastage of time, money and resources?!. Kwani katiba ndio nini hata iheshimiwe hivyo?.

4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.

5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.

6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.

7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.

8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, , Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?.

Paskali
Leo kulikuwa na kikao cha halmashauri kuu mkoa cha kupokea taarifa za utekelezaji wa ilani ambao mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christine Mndeme alikuwa anawasilisha, Katika kikao hicho kilichorushwa moja kwa moja na Chanel Ten, wajumbe wa haashauri kuu mkoa wa Ruvuma wamekubaliana Rais Magufuri aendelee KUONGOZA kwa miaka 20 zaidi.

Kama mawazo hayo yataungwa mkono na mikoa mingine ina maana inawezekana Magufuli ndiye Rais atakayekaa madarakani miaka mingi Ikulu kuliko hata Nyerere
Harakati zimeanza.
P
 
Back
Top Bottom