Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwani hawezi kutokea a better person than him? Watu walisema haya haya kwa Mwinyi wakataka aendelee, isingekuwa mwalimu huenda Mwinyi angekuwa rais hadi leo, akaja Mkapa tukasema hayahaya, akaja JK watu wakata akae hadi katiba mpya ipatikane, uzuri JK ni mwanasiasa alijua amani ya Tanzania inasimama kwasababu ya term limit watu wakimchoka rais matumaini yanayobaki ni kusubiri muda wake uishe. Hivi tumeshawahi kujiuliza Mwinyi angeamua kubaki leo tungekuwa na JPM? Who knows what God has in stock for our nation? Huenda ajaye atakuwa bora zaidi ya huyu. Na kiongozi mzuri hufanya yale mazuri katika muda wake wa uongozi na kuwaacha wengine watende mengine mazuri, kiongozi mbovu huamini hakuna binadamu wengine wenye akili ila yeye tu, Na hupenda kung’ang’ania madarakani na mwisho wake huwa sio mzuri. Rais wetu keshatukumbusha mara nyingi tu kuwa hana mpango wa kuendelea muda wake ukiisha, wacha wapiga ramli waendelee ila yeye keshasema. Ikitokea akayageuka maneno yake na msimamo wake basi hatufai. Maana kiongozi mzuri ni yule anayesimamia maneno yake, a man of his words.
 
Mkuu Gerald Magembe, kwanza naunga mkono hoja yako hii na kitu kama hiki niliwahi kukishauri humu katika uzi huu. Ili Tanzania tufanikiwe kweli na kuweza kusonga mbele, huyu mtu anahitaji kupatiwa muda wa kutosha, the minimum ya angalau miaka 20 kuinyoosha Tanzania.

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

P
 
Wanabodi,
Hili ni swali la 5 years ago na sasa mwaka wenyewe wa uchaguzi ndio huu.

Hivi na hii Corona, huu ni mwezi May, uchaguzi ni October, kweli bado tunahitaji kufanya uchaguzi wa rais?.

P
 
Wanabodi,
Hili ni swali la 5 years ago na sasa mwaka wenyewe wa uchaguzi ndio huu.

Hivi na hii Corona, huu ni mwezi May, uchaguzi ni October, kweli bado tunahitaji kufanya uchaguzi wa rais?.

P
Mkuu P uko vizuri upstair na ni mwandishi kwa taaluma ila wakati mwingine unashangaza sana. Uko serious na ulichokiandika? na kama hauko serious kwa nini unaandika ulichokiandika. Kama uko serious basi kazi ipo kwelikweli.
 
Wanabodi,
Hili ni swali la 5 years ago na sasa mwaka wenyewe wa uchaguzi ndio huu.

Hivi na hii Corona, huu ni mwezi May, uchaguzi ni October, kweli bado tunahitaji kufanya uchaguzi wa rais?.

P
Uchaguzi ni takwa la Kikatiba, tukiangalia mtu akae madarakani kwa vigezo flani flani haiwezi kuleta maana wala ufumbuzi, mfano wewe umemuona kafanya vizr sekta flani, Je sekta ambazo kafeli atafutwe Rais mwingine awe msaidizi ili afanye hizo sekta nyingine? TUHESHIMU KATIBA NA TUWEKE MAPENZI BINAFSI KANDO, MAZURI YOTE ANAYOFANYA NDO LENGO LA YEYE KUOMBA KUONGOZA NA WALA SI HISANI, VP MABAYA ANAYOFANYA TUKITUMIA KIGEZO CHAKO ANAPASWA KUONDOLEWA?
 
Mkuu P ni mwandishi unashangaza sana. Uko serious na ulichokiandika?. Kama uko serious basi kazi ipo kwelikweli.
Mkuu Focal, niko very serious!.
Haya ni maoni yangu, pia humu jf ni rukhsa kushangaa!. Endelea kushangaa...
P
 
Mkuu Focal, niko very serious!.
Haya ni maoni yangu, pia humu jf ni rukhsa kushangaa!. Endelea kushangaa...
P
Nimekuelewa mkuu P, lakini uchaguzi ni takwa la kikatiba hata kama huyo Raisi kafanya makubwa kiasi gani. Tukianza haya mambo ya aendelee tu huko ni kuisigina katiba. Ni lazima uchaguzi ufanyike ili kama kawafanyia wananchi mazuri basi wampe kipindi kingine. Hayo ya propaganda tuwaachie wanasiasa kwa taaluma yao..
 
Wanabodi,
Hili ni swali la 5 years ago na sasa mwaka wenyewe wa uchaguzi ndio huu.

Hivi na hii Corona, huu ni mwezi May, uchaguzi ni October, kweli bado tunahitaji kufanya uchaguzi wa rais?.

P
Mungu akiamua lake Mwanadamu hawezi kulizuia. Najua kuna wale wala fedha za Bungeni hawautaku ukweli huu lakini muda ndio huo tena.

Na hata ikafanyika Uchaguzi tutawasikia Puppets wa mabeberu huko majukwaani wakisema "Kufanya uchaguzi ni kufuja hela bora bajeti ingeenda kwenye kuokoa Uchumi uliotetereka na janga la korona n bla bla km walivyozoea"
 
Wanabodi hili ni bandiko la 2015

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Wanabodi, kwanza angalieni tarehe ya bandiko hili, kisha angalia hoja No. 4, 5, 6, 7 na 8 za bandiko hili, kisha sikiliza kilichozungumzwa jana Bungeni Dodoma kuhusu hoja hii.


P
 
Hili andiko linashusha heshima yako
Mkuu Screpa, it's true, linashusha heshima yangu kwa wasomaji wa viwango vyao, lakini kwa wenyewe wenye uwezo to read in between the lines, tunaelewa vizuri sana tuu.
P
 
Vijana wa CCM mnatumika vibaya sana, kama KONDOMU. Mwishowe mtatupwa huko kama GAMBO na MULONGO. Shauri yenu.
 
Mkuu Elius Ndabila, naunga mkono hoja

P
 
Nani kakuambia rais atakuwa John Magufuli?
Mtajinyonga bure baada ya kujua kuwa 28/10 ndio mwisho wa Giza la nchi hii maana mwanga, furaha, amani na heshima vinarudi tena.
Mkuu Chakaza, umeona hiyo sentence kwenye bold?.

2020 ni Magufuli 5 tena!.
P
 
Mkuu Chakaza, umeona hiyo sentence kwenye bold?.

2020 ni Magufuli 5 tena!.
P
Mkuu nimeiona, lakini kumbuka maneno aliyosema Tundu Lissu mgombea wa Chadema. Kuwa "tukishinda lazima tutatangazwa"
Hayo sio maneno mepesi kutoka kwa mgombea kaliba ya Lissu.
Angetamka Rungwe au Lipumba yangekuwa mepesi lakini sio Lissu.
Nakushauri kama mwandishi unayesomwa na hata hao wakubwa (tofauti na sie makapuku) andika makala za kuonya kuhusu hatari ya mgombea Y kushinda na kutangazwa X katika TZ ya Leo.
Pia matokeo ya jambo hilo ni vurugu na kusababisha vifo. Na jambo hilo katika dunia ya Leo halikubaliki ndio mwanzo wa safari ya The Hague sio kwa mkuu mwenyewe tuu bali hata kina Sirro, Mabeho (kama atajihusisha) na wengine wengi tuu
 
Hata Lisu Mwenyewe na Chadema yao wanajua fika Magufuli kawaacha mbali na ushindi kwa CCM safari hii sio wa Mashaka Mashaka km ilivyozoeleka huko Nyuma. Hii ndio sababu tunashuhidia Kampeni za furaha na kiaina sherehe Fulani sababu Umma unamfurahia na kumpongeza Mgombea wa CCM kwa kazi nzuri zinazoonekana alizofanya ktk awamu Yake ya kwanza.

Narudia ushindi kwa CCM Mwaka huu sio wa Mashaka Mashaka sababu ile nguvu ya Umma ndio imemkubali Magufuli na ndiyo inayomtaka aendelee.
Hoja dhaifu aliyokuja nayo Lisu (km mesia wa kuikomboa Chadema toka shimo ilulokua inazama) ni kutafuta huruma ya Tatizo alilopata yeye kama yeye na Uchochezi ambao ndio unaomuangisha vibaya)

Naamini Mbowe na wenzake wanachofanya ni kumtumia Lisu kuokoa jahazi lililokwisha anguka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…