Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Narudia tena kuonya, CCM Kwa mambo Mazuri yaliyotapakaa karibu Kila Kona ya nchi yetu yaliyofanywa Chini ya Uongozi mahiri wa JPM, isingewezekana Kwa Chama, ama Kwa mtu yeyote maarufu kushinda uchaguzi huu never!

Na hata hivyo, bado ni mapema, waachane na Kampeni za Urais ili kuokoa hata hicho kidogo walichonacho mkononi, itawaletea heshima

Waweke nguvu kwenye ubunge wasije kuanguka kotekote, angalau kwenye ubunge wanaweza kuambulia wawili watatu........ Hivi
 
Mataga
 
Sheria Inasemaje?
Ina Maana JPM Kapita Bila Kupingwa
Acha Vyama Vyote Vifanye Campaign Hadi Mwisho
JPM Anasema Wazi Wananchi Wakapige Kura
Tume Ndiyo Itangaze Nani MSHINDI
 
Mtoa mada naona kama ulikuwa unatumia hadubini kuona yale yanayokuja kutokea.
 
Mgombea wa CCM John Pombe Joseph Magufuli amesema kwa kipindi cha miaka 5 ametengeneza ajira milioni 6.

Nyie waimba sifa wake mwambieni labda waliojiriwa walitangaziwa ajira Ikulu, wakafanyiwa interview Ikulu,wakaajiriwa Ikulu. Lakin Huku mtaani kwetu vijana hawana ajira,walimu hawana ajira.Hali ni ngumu Mzee.
 
Kuna swali niliuliza kwenye last line ya bandiko hili, leo ndio nimejibiwa
Mkuu Gerald .M Magembe , kuna kitu kikubwa sana unakizungumza hapa kuhusu uchaguzi, kushinda kura na kukabidhiwa nchi.

Kule Zanzibar kuna dhana kuwa kila siku kuna mtu anashinda lakini hapewi!. Kuna mtu akasema "Zanzibar ni nchi ya kimapinduzi, mtu hawezi kukabidhiwa nchi kwa kipande cha karatasi ".

Mimi kabla ya uchaguzi wa 2015 nikawashauri kama ni kweli kuna mtu huwa anashinda lakini hapewi, lazima kuna sababu inayofanya hapewi, nikawashauri, waitafute hiyo sababu ili kabla hawajaingia kwenye uchaguzi Mkuu mwingine wahakikishe hiyo sababu inayofanya asipewe imeshughulikiwa ili akishinda apewe, hakuna aliyejishughulisha kutafuta sababu.

Na kweli kwenye uchaguzi wa 2015 kule Zanzibar, CUF ilikuwa inaelejea kushinda ila kabla ya ushindi kutangazwa, meza ikapinduliwa!.
Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Sasa uchaguzi huu wanajaribu tena bila kujua hizo sababu.

Kwa upande wa uchaguzi wa huku bara, hata mimi niliwahi kuuliza suppose CCM imeshindwa, huyo mshindi atapewa?, atatangazwa?.

Kwenye bandiko hili, kwenye last line, kuna kitu niliuliza
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Jee Systems ziliandaliwa kuweza kumsarve a different master?. Suppose Chadema ndio ishinde, TL awe CinC?!, can you imagine?. Jee nchi inakabidhiwa kwa votes or vetting?.

Hebu tuelimishe kwa uchaguzi wetu electro collage zetu ni zipi zitakazo fanya hata Chadema ikishinda electro votes bado haiwezi kupewa nchi kwasababu haijaonenyesha maturity, ability, capacity na capabilities, ili kuwa entrusted na Ikulu yetu?.

P
 
 

Uongozi wa juu kabisa sio rahisi hivyo kama wengi wanavyo dhani.
 
Maskini magufuli alikuwa anazxubaoshwa na thread kama hizi za mapambio na masifa toka kwa mabazazi wa kisiasa ambao walipotaka kugombea ubunge L awe walidharilishwa na kuonekana kaa taka taka magufuli will nevrr win for second term ni fisadi mwizi mkabila he must go
 
Kwa sababu tarehe 28 October, Watanzania tunakwenda kufanya uamuzi, sasa muda huu kabla ya uchaguzi, najifanyia tathmini nilisema nini kuhusu uchaguzi huu, na baada ya matokeo, nitarejea na kupima kilichotokea na nilichokiona kabla.
Natoa wito kwa Watanzania wenzangu, tujitokeze kwa vingi kupiga kura na kuchagua chama, viongozi tunaowataka ambao watatuletea maendeleo ya kweli. Kwa wanaotaka maendeleo ya kweli, watachagua chama na maendeleo ya kweli, lakini kwa wanaotaka porojo tuu, rukhsa kuchagua porojo ni haki yako ya kidemokrasia kuchagua chama chochote, kiongozi yoyote.
Paskali.
 
Siamini Paskali Mzee umekuwa mweupe namna hii, heshima yako kidogo iliyobaki kwangu acha niihifadhi hadi wakati mwingine.

Njaa yako ni mbaya na inatafuna ubongo, chunga itakufanya vibaya.
 
Ukweli ni kwamba, uchaguzi haujafanyika na matokeo hayajajulikana
Zaidi ya hapo, kuongelea matokeo ya uchaguzi huu kabla haujafanyika ni kupiga ramli tu.
Usirahisishe habari kwa kuotea nani atashinda.
 
Swali langu ni dogo tu
Why tumetumia gharama nyingi kuendesha uchaguzi wakati kila kitu tayari kipo planed?

Ndio maana wazungu huwa wanatufananisha na masokwe

Hayo maela yote si bora yangeenda kulipa pession kwa wazee wetu?
Mkuu hp4510 , huu ndio ulikuwa ushauri wangu wa kwanza kabisa, angalia tarehe ya bandiko hili
Uchaguzi ni takwa la kikatiba, sheria, taratibu na kanuni, lazima ufanyike na hata kama baadhi ya sehemu ni igizo tuu la uchaguzi.

P
 
Baadhi ya wana jf ni watu wa ajabu sana, eti wanashangazwa na matokeo ya uchaguzi huu na wamekuwa surprised as if they didn't know hiki kingetokea.
Angalia tarehe ya bandiko hili, uone tulisema nini kuhusu uchaguzi huu wa 2020,
kinachowashangaza ni kipi?.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…