Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Wanabodi.

Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli

Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.

Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.

Paskali
Inawezekana ila tatizo ni zile kauli zake za kujutia uteuzi, kwamba najuta kuomba nafasi hii, mimi nilikuwa nabip tu kuchukua fomu. Kauli hizi zinaonesha hatuna sababu ya kumlazimisha mpendwa wetu, aachwe apumzike. Na mimi naamini hata awamu ijayo anaweza kujiengua mwenyewe, hana tamaa ya madaraka kabisa.
 
Hatufanyi uchaguzi kwa sababu kuna kasi au hakuna kasi. Hii inaonyesha kwa Tanzania, waliosoma na wasiosoma wote kapu moja..
 
Kilaga

Tatizo la Pasco ni njaa na unafiki.

Ugali wa unafiki anautaka,ila kukabidhi ufunguo wa akili zake pale Lumumba anaogopa.

Kuudhi watu makini kichwani hataki,ila udenda unamtoka kila ainapo minofu anayoifadi Makonda kwa kujipendekeza kwa Magufuli.

Pasco anataka kotekote,heshima ya watu makini humu JF anaitaka,na kushiba makombo ya unafik anataka!

Atapasuka msamba shauli lake"
 
HAYA NI MAWAZO YA KITUMWA!!!

Kuamini maendeleo yanaletwa na Rais kukaa mda mrefu madarakani, kunyoosha wananchi kwa kukiuka utawala wa Sheria ama kubadili katiba kwa kisingizio cha maendeleo.

Hizi sio Zama za "Devine rights and power of Kings"

Kaka Paschal Mayalla nakufahamu vizuri sana wewe sio muumini wa hoja nyepesi,imani yangu inanituma haya maswali umeuliza wewe kama njia ya kuwapatia majibu wenye hoja zao.

Kwa Taswira ya mabadiliko na Maendeleo ya kweli Rais Magufuli bado anatapatapa.Anajitahidi sana lakini kiukweli kwa mwenendo wake sina Shaka Hata aongoze miaka 32 kama Museven Bado ataiacha Tanzania maskini.

Maendeleo ya nchi sio zao la raisi kukaa madarakani mda mrefu Ipo mifano lukuki ya viongozi wa Africa waliokaa Madarakani miaka mingi,wengine waliingia kwa Mapinduzi ya kijeshi,wengine walichaguliwa na wananchi badae wakavuruga na kubadili katiba lakini mpaka Leo nchi zao ni Maskini.

Kwa mfano:
Robert Mugabe-ameitawala Zimbabwe kwa miaka 35,Yoweri Mseven ameitawala Uganda miaka 31 na Paul Kagame ameitawala Rwanda kwa miaka 17.

Umewataja kuzinyoosha nchi zao(sijui ulimaanisha kuwanyoosha kwa kuishi kama mashetani au malaika)

Lakini ukweli ni kwamba Kati ya nchi maskini Duniani Zimbabwe,Uganda,Rwanda na Tanzania ni Kati ya nchi 47 Maskini zaidi(Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya UN Least developed countries-LDC's ya Mwaka huu)Tembelea website ya UN usome Data sheet..hizi nchi hazija-graduate.

Tanzania:
J.K.Nyerere(Baba wa Taifa-Rais mwenye Busara na Hekima,rais aliemfukuza mkolon,mwanafalsafa,mtakatifu bado kutangazwa) aliongoza miaka 23 akaiacha Tanzania maskini.

Mwinyi a.k.a Mzee Rukusa:
Aliongoza miaka 10 akaicha Tanzania Maskini

Mkapa:
Alianza vizuri kama Mr.Clean akaongoza miaka 10,lakini bado akaicha nchi maskini na kashifa lukuki za ufisadi.

Mhe. Jakaya Kikwete a.k.a Chaguo la MUNGU alianza vizuri kwa Ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya lakini wapii bado ameiacha Tanzania Maskini na na kashifa lukuki za ufisadi.

Magufuli JPM a.k.a Brudozer,Mzee wa HAPA KAZI TUU!!:
only two yrs +,pamoja na kukiri haheshimu utawala wa Sheria mnataka aongezwe mda na kufuta uchaguzi atawale kama chifu kweliii!!?..

Kasi ya utawala wa Rais Magufuli ni kasi ya utumbuaji,matamko,kubeti,na kasi ya maisha kuzidi kuwa magumu!!

Watu kukosa mahitaji,kukosa ajira,kukonda,kuishi kama mashetani,
Chuki,visasi,biashara kufa kila uchao,hofu na mashaka,n.k

Tuombe uzima Bada ya miaka mi8 Tukutane hapa Tutoe ushuhuda!
 
Mkuu Jeki, kiukweli kauli hizi ni tatizo!, nimezifanyia psychoanalysis kauli hizo nikagundua zinatokana na some deep rooted neurosis zinazompa inferiority complex na lack of confidence hivyo hizi kauli na matendo ya superiority complex ni matokeo tuu.ĺĺl

Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Paskali
 
Sasa Pasakali labda mm niulize,je unapofanya kazi nzuri huku ukikanyaga katiba na kuwatenda wenye nchi ndivyosivyo hapo nani MNUFAIKA??
Pili kuna sababu gani ya kumwongezea JPM muda?kwani tunahitaji ushupavu wake tu au tunataka ungangari wake uimarishe taasisi zetu? Maana hata akitawala miaka 100. Bila taasisi imara tutarudi kulekule. Si unajua alivyokua Nyerere na waliomfuatia ni mbingu na dunia!!?

Paskali maendeleo si kukanyaga haki za watu hata wasiwe huru ktk nchi yao. Hapo nakataa
 
Magufuli HAAMINIKI!!
Hata miaka mitano sijui kama tutaimaliza Salama.

Rais hata Hotuba tuu zinamshinda.

*Kuna siku anahutubia kama nabii/mchungaji

*Siku nyingine kama Mkuu wa Alshabaab

*Siku nyingine Kama Meneja wa Kampuni binafsi

*Siku nyingine kama Rais

*Siku nyingine hadi Ving'amzi vinazima anatoa speech kama mgonjwa wa Mirembe!

Hata wasaidizi wake anawapa kazi ngumu ya kumsafisha (hotuba zake nyingi serikali tuu ndo inazielewa) mpaka amalize kuhutubia jopo likae kutafsiri mf.hotuba ya ALAT hamjui tuu lakini nyuma ya pazia kuna mengi.

Juzi kwenye mbio za mwenge na Nyerere day Zanzibar ikabidi asome hotuba angalau jamaa wakapumua nae akazungumza kama rais.

Kiufupi tukiacha ushabiki JPM ni haaminiki kabisa!!!

Kuna mda huwa natamani BoraX10 Mama Samia Suluhu ndo angekuwa Rais Kassim awe makam pengine busara za mama samia zingesaidia!

Magufuli alitakiwa awe waziri mkuu!!!
Urais Badoo ana wenge sanaaaa!!!
 
Kwa nafasi ya urais tusifanye uchaguzi.
Kwa nafasi za udiwani na ubunge wachukuliwe wale walioshika nafasi za pili 2015.
Alafu tuuunde serikali ya mseto.
 
Njaaaaaa
 
Walewale kama .mh nkamia. Tusiwe na akili fupi kiasi hicho kwa ushabiki tu..hadi washindwa chambua mambo kwa weredi. Nchi yenyewe bhado msimamo wa taifa haujulikani . Hata ujinga sio hivyo, kwani alietufikisha hapa tulipo sasa nani au hatumjui. Tuamke na tujitambue kama taifa .tufuate sheria na taratibu tulizojipangia kwani ndo mwongozo wetu.

But bongo shida kubwa ni elimu na kujitambua tu...kwani wasomi wachache na wasio soma wengi hadi wamepitiliza ... it means wajinga wengiiiiiiiiiiiiiii.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…