Kwa kasi hii ya Rais Magufuli nashindwa kuelewa mzee Mwinyi alifeli wapi hadi viwanda na mashirika ya umma yakafa!

Mradi wa mabasi ya mwendo kasi ulianza wakati huu wa Magufuli, leta mrejesho wa kasi ya mradi.
Kwenye mwendokasi shukuru sana awamu hii mana bila wao kwa hali yako ungekuwa unatembea kwa miguu wewe ungekuwa unaishia kuyaona kwenye taarifa ya habari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwinyi hakufeli, angefeli JPM leo asingekuwa rais. Unasema maendeleo hayana vyama husemi kweli. Tumeona viongozi wakiwanyima watu huduma kwa sababu kura za CCM zilikuwa chache huko. Pia pale Arusha mkuu wa mkoa alijaribu kukwamisha ujenzi wa hospitali ya kisasa kwa sababu tu ni juhudi za Lema kutika chadema.
Kwa sasa barabara za vumbi nchini ni mbaya kuliko hata zilivyokuwa baada ya vita ya Idd Amin.
Zahanati vijijini hazina watumishi kabisa au zina mhudumu moja tu. Shule za msingi hazina waalim wa kutosha.
Idadi ya watoto wanaopata mikopo ni ndogo mno.
Dah.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vita ipi mkuu wakati mmepata Uhuru without arm struggle bali ni constitution or negotions.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani siku moja ushirikishe ubongo kidoho badala ya kucha, natamani muanze kujenga hoja shawishi na sio hizi harufu za uchama
Tumwache Mzee Mwinyi apumzike hata km aliteleza yaneshapita hayo, hatuwezi kuyarudisha nyuma

Ili mradi tumepata Rais Mzalendo kila kitu kitakaa sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawawezi kufikiri haya, hawajui kuwa JPM anavuna asichokipanda?
Amekuta hazina inacheka na akiishiwa anawabana mafisadi na kuwakwuda wakiri walipe au wabane wafie gerezani.
Duh mkuu ina maana hujui nyerere alimkabidhi mwinyi nchi haliyakuwa imemshinda...? That we were in survival mode...? Nchi hata kujinunulia chakula ilikua tabu ndo iwe hayo mambo mengine..?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ikawa ili kupata hela ya kununua chakula lazima tu uze na kuuwa baadhi ya viwanda vyetu, so as to maintain and manage our survival mode.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kipindi hicho hakuwa na option. Wananchi aliwakuta masikini na pesa hawana, kodi asingeweza kukusanya kikamilifu. IMF na jumuiya za kifedha zilikataa kuikopesha nchi kutokana na sera za nchi za wakati huo.

In short jamaa ilibidi ajitoe kafara ili mambo yawe kama yalivyo leo. Bora hata huyu wa sasa anakopesheka na anakopa kwelikweli, pia kodi anakusanya za kutosha kutoka kwa wananchi ambao amewakuta na ukwasi walioachiwa na j.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kumbe ulituhumu bila utafiti?
Mnayemwita mzalendo anatembelea nyota za Ben na Mkwere.
Amekuta hazina inacheka, huku akiishiwa anawakwida wafanyabiashara wakiri kuwa wahujumu uchumi walipe au wakane wafie gerezani.
Kuna wakati utabadilisha ID kwa kuogopa sifa hizi.
Kwani huyu mnayemsifia mtayajua madhara ya maamuzi yake baadae sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie mgojeni tu tutasikia na Tume ya uchaguzi nayo imetoa gawio hahaa
 
Mchumi heshima yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaelewa maana ya ?!
 
Wewe lazima utakua ni mkatoliki viwanda mashirika ya umma yalikufa enzi za nyerere hali ikawa mbaya sana kila kitu foleni.
Mzee mwenye akaleta neema bidhaa zote zikawepo ila imported tv zikaanza barabara za lami zikaanza kujengwa ya kwanza kariakoo kisha ya kawawa palikua pananuka
Mkapa akaja ufisadi ukaanzia kwake akauza viwanda mashirika mabenki mashamba na hata kufikia akafungua kampuni binafsi ikulu akajiuzia kiwira mbaya zaidi nyumba za serikali kodi zetu nyumba ya 1bn ikauzwa 9m tena ulipe ndani ya miaka 20.
Shule zilijengwa
Kikwete akajenga barabara kilimo kwanza umeme vijijini etc safari nyingi sana kwa watendaji semina za hovyo hovyo
Magufuli anajenga vitu lakini sii ustawi wa wa wananchi ataua kilimo elimu kisha akiondoka kutakua na kesi nyingi sana za madai ufisadi miradi maana yeye hafuati bajeti ya bunge
 
Hapa tunaangalia changamoto.......mambo ya kuchafuana ni ya kwako wewe na ufahamu wako!
Changamoto
Nadhani haufahamu utawala wa Mwinyi vizuri na changamoto alizokutana nazo.
Yawezekana hauna lengo la kumchafua ila Uzi wako unafanya hivo. Kwan uzi unaonesha kuwa Taifa lipo Nyuma kimaendeleo sababu Mwinyi alishindwa kusimamia viwanda.
Swali:
Hivyo viwanda alikabidhiwa vikifanya kazi ya uzalishaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…