isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,143
- 6,560
Huu ndio ukweli wa wazi kabisa ambao hausemwi ilhali ipo wazi nyerere anatakiwa kushtakiwa kwa kuhujumu uchumi, taifa na watu wake kwa sera za hovyo.Mfumo wa uchumi wa kimashariki (Kijamaa) kupitia Azimio la Arusha uliopora viwanda na Mali nyingi za matajiri na serikali kujimilikisha na kuviendesha.
Bahati mbaya viliendeshwa kwa kupangiwa bei na serikali bila kujali gharama za uzalishaji (Production cost) Vingi vilifeli mikononi mwa Nyerere mwenyewe! Na ilibidi vipewe ruzuku toka kwenye kodi.
Njaa ya miaka ya mwisho Sabini na Vita ya Uganda na Tz vilifirisi kabisa nchi. Nyerere akaenda kwa mabeberu kuomba mkopo
Walimpa masharti yafuatayo;
i. Kujiondoa serikali kuzalisha,kuagiza na kuingiza bidhaa. Iwe inakusanya Kodi tu.
ii.Kuwepo na soko huria. Bei za bidhaa zitokane na ushindani na mahitaji ya soko. (Serikali ijiondoe kupanga bei)
iii. Ashushe thamani ya shilingi
iv. Kuwepo uchangiaji katika huduma za kijamii baina ya serikali na wananchi ( Cost sharing) ili kuipunguzia mzigo serikali.
vi.Apunguze idadi ya watumishi wa umma na mishahara yao.
vii.Abinafsishe viwanda alivyopora na vile alivyopora.
Nyerere aliyakataa masharti huku akinukuliwa kwamba anayedhani Tz itayakubali masharti hayo ni mwendazimu akiwa ziarani Uingereza (Scotland?). Mwisho alienda Mara ya pili mezani IMF na WB wakasimama kwenye masharti yao.
Nchi ilikuwa taabani na Nyerere ikabidi ang'atuke kulinda msimamo na heshima yake.
Mwinyi akachukua nchi na kutekeleza masharti.