Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Ukikaa vijiwe vya Kahawa Tanga hasa kwamsisi, Handeni na Pangani ukasikiliza Stori za wananchi utatambua umuhimu wa kuziweka mamlaka za uteuzi mikononi mwa Mungu.
Watu wanaratiba kabisa yakwenda kuongeza nguvu za kimamlaka wengine wanatumia magari binafsi huku wachache wakitumia magari ya umma. Likipita gari kuingia chocho au likipaki mfano kwamsisi unasikia Mzee huyo anakwenda kupata huduma.
Wapo watu wanaacha walinzi na V8 mbali wanapanda bodaboda kuficha identity; baadhi wanatuma gari kwenda kuchukua wataalam nakuwapeleka Dodoma au DSM kutoa tiba ya madaraka.
Unapoongoza wizara, Idara au nchi ambayo watu wake wanaamini katika tamaduni na baadhi wanamwamini Mungu NI vigumu kujua kama umefanya uteuzi Kwa kuzingatia vigezo au umekuwa drived na nguvu za Giza au nguvu za wataalam wa tamaduni.
Unashangaa hata wavaa magwanda wanaopambana na waganga wa kienyeti nao wanaponea hukohuko. Baadhi kama sasa hivi ilivyosomwa ripoti ya CAG mambo huku kwetu NI bam bam wateja wamekimbilia ukanda WA chalinze na Tanga kupooza ripoti isisomwe Kwa sauti.
Kabla ya kulaumu mamlaka za uteuzi wanapoteua asiyejiweza tumwangalie kiundani aliyeteuliwa ana nguvu za ziada?