Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 26,961
- 77,890
- Thread starter
- #21
Sure mkuu. Kwa nchi kama Tanzania ambao tumezoea kununua magari used itatusumbua ila ukinunua jipya au ambalo battery yake imebadirishwa kabla haujauziwa nadhani itakua fresh.Kiboko yake betri ikiisha muda Bei ya ku replace itapita Kwa mbali sana Sababu ni karibu nusu ya Bei ya Kununua gari la umeme
Kwa mfano, Tesla Model 3 niliona wanajisifu (sasa sijui ni lugha ya Market au ni ukweli) kwamba battery ya gari lao lina Life Expectancy ya Miles 300,000 hadi Miles 500,000 hivi, au 1,500 battery cycles.
Kwa lugha nyepesi, kwa dereva wa kawaida (achana na magari ya makampuni au serikali), ambae kwa mwaka anaendesha 20,000 kilometa au tuseme average ya kilometa 55 hivi kwa siku, under normal conditions battery itadumu kwa miaka 22 hadi 37.