Kwa kasi ya Mchina na Electric Vehicles (EV), sio muda tutapishana nazo Dar

Kwa kasi ya Mchina na Electric Vehicles (EV), sio muda tutapishana nazo Dar

Niliona Porsche Panamera full EV aisee niliipenda, inakimbia balaa halafu kimya.
Wana hio Tycan, nilikua naiona kama Safety Car kwenye Formula E
1280px-2020_Porsche_Taycan_4S_79kWh_Front.jpg
 
Duh! gari za umeme maintenance ni gharama sana hata marekani ambako Tesla ndio chimbuko lake...kwa gari za umeme bado sana kulikamata soko maana uzalishaji wake inavoonekana ni gharama sana pamoja na miundombinu wezeshi hasa Africa safari kufikia huko bado sana
 
Wakuu, tukubali magari ya umeme yanazidi kuongezeka kwa kasi sana ndani ya hii miaka mitano. Na inavoelekea yatazidi kuongezeka maradufu. Mfano tu angalia hii chart nimeitoa Wikipedia.

View attachment 2936011

Sasa kwa rate hii, nina imani na Tanzania sio muda tutaonesha ubabe wa kuagiza hizi chuma.

Mchawi ni gharama na Watu kuogopa issue ya mafundi.

Tukianza na gharama, sasa imekua sio issue tena.

Makampuni makongwe kama Tesla, wana offer gari mpya kwa bei kubwa sana unakuta Model 3 inauzwa $60,000/= mpya. Ukinunua used ndio unakuta $35,000/= kabla ya TRA. Bado yamoto sana.

Hawa Wachina BYD wamekuja kusolve issue ya bei kwa kutuletea gari mpya hadi ya $13,000/= imagine.

Hawa jamaa mwaka jana wameajiri mainjinia zaidi ya 20,000 kwenye Research & Development Department tu. Hii inamaanisha vitu vingi vizuri vipo njiani.

Mwaka huu 2024 wamekuja na hii gari BYD e2 Honor Edition kea bei ya $13,000/= tu.

View attachment 2936015View attachment 2936016View attachment 2936017

Theoretically hadi sasa ikiwa full charge inatembea Kilometa 400, Motor 70kW, Battery 4.9kWh, maximum speed ni 130 kph, Output power 94HP, uzito wake 1340 kg, Fast Charge 0.5 hours na Slow charger 6 hours izo ni baadhi.

Sasa kama serikali yetu sikivu kupitia TRA wakafanya mchakato kama walivyohaidi kwamba magari ya umeme yatakua na ushuru bure basi itapendeza sana.
View attachment 2936021
Watu watajiripua, tutaenjoy magari mazuri bila makelele mengi njiani na eco friendly.

Pia serikali ingeanza kwa kuonesha mfano kwa kuingiza mabasi ya Mwendokasi yawe ya umeme na magari ya baadhi ya mashirika yawe ya umeme, mfano posta delivery ya mizigo mjini.
Dar nishakutana na gari kadhaa za umeme pure, sio hybrid, ni umeme pure kwa sasa tuna mudu Nissan Leaf model ya kwanza, nyingi ni 30kwh yaani ikiwa battery ikiwa na 0% itahitaji umeme wa unit 30 kujaa yaani umeme wa shilingi 10,715 kujaa, ambapo wengi wanasema inawapeleka kati ya 200 na 250km ndipo chaji kwisha ambapo ni very economy, andaa kama 20mill hivi kupata 1st generetion ya nissan leaf kuipata yenye battery health nzuri kabla hatujaanza kuwawaza akina BYD na Tesla
 
Duh! gari za umeme maintenance ni gharama sana hata marekani ambako Tesla ndio chimbuko lake...kwa gari za umeme bado sana kulikamata soko maana uzalishaji wake inavoonekana ni gharama sana pamoja na miundombinu wezeshi hasa Africa safari kufikia huko bado sana
Nakukatalia, maintainance gani ya gari la umeme ni ghali? Gari la umeme ni gharama kulinunua sio kuli maintaine
 
Mwanangu Mad Max sijui unapendea nini haya magari!! Japokuwa ulimwenguni unaenda kwenye EV's kwangu Mimi bado natamani combustion engine ziendelee kutengenezwa..
haya magari ya UMEME Kwa maisha yetu ya kiafrica naona kama bado sio rafiki kwetu, ndiyo maana kampuni ya Toyota wamependekeza Kwa manufacturers wawekeze kwenye hydrogen fuel( eco friendly) pia ni zero emissions kama UMEME Tu

Technology ya hydrogen fuel ni kama ilivyo petroleum na diesel engine.... Najua baada ya miaka 10 mbele Tanzania tutakuwa tunatumia magari ya kichina kwasababu ya bei zake chini pia serikali Yao wamedhamiria kuteka soko lote la Asia, Latin America na Africa Kwa kuingiza magari yao
Haya magari yanahitaji pull factors pia, mfano kuanza kufunga mfumo wa kuchajia wa public.
 
Back
Top Bottom