Kwa Kauli Hii ya Twaha Mwaipaya, Jeshi la Polisi Limechukua Hatua Stahiki

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
Screenshot_20240812_180253_Parallel Space.jpg
Screenshot_20240812_180325_Parallel Space.jpg

Nimenukuu barua ya Polisi ya tarehe 11/ 08/ 2024
Screenshot_20240812_182137_Parallel Space.jpg

Hata mbuyu ulianza kama mchicha. Twaha Mwaipaya anataka GEN Z ya Tanzania iigize yaliyotokea Kenya. Kongole Tanpol kwa hatua mliyochukua.
 
Kosa la hizo statement liko wapi? Kuwaambia vijana waamke wapiganie haki zao? Kutumia haki yao kisheria kukusanyika kwenye mkutano wa siasa? Au ni sheria gani ya nchi imevunjwa kwenye hizo kauli?

Tatizo lenu mnasoma hizo statement mkitawaliwa na fikra potofu, fikra hasi, kwamba hizo kauli zinachochea vurugu, kwanini muogope hizo kauli kama mnaamini hamjakosea popote?

Mnajua ukweli nyie ni waovu, mnakandamiza haki za watu ndio maana hamtaki wapiganie haki zao, hivyo kwenu wao kuamka kudai haki zao, kwenu ni kauli ya hatari sababu ya uovu wenu.
 
Kosa la hizo statement liko wapi? Kuwaambia vijana waamke wapiganie haki zao? Kutumia haki yao kisheria kukusanyika kwenye mkutano wa siasa?

Kuna watu hawana kabisa critical thinking.Wamejawa na fikra za mapokeo.
 
Mimi sijaona matamshi hayo yana viashiria gani vya kuvunja amani au kuleta vurugu!
 
View attachment 3068006View attachment 3068007
Nimenukuu barua ya Polisi ya tarehe 11/ 08/ 2024
View attachment 3068017
Hata mbuyu ulianza kama mchicha. Twaha Mwaipaya anataka GEN Z ya Tanzania iigize yaliyotokea Kenya. Kongole Tanpol kwa hatua mliyochukua.
ni muhmu sana jeshi imara la polisi likamzidishia mbinyo zaidi kisawasawa, ili aelezea zaidi na kwa kina, mipango hiyo ya kihalifu na kuwataja washirika wenzake wote, ili iwe fundisho kwa wahalifu wengine nchini :pulpTRAVOLTA:
 
Yule aliyesema wapinzani wakipotezwa wasiulizwe alichukuliwa hatua gani? Ili tuone utendaji stahiki wa polisi?
Huyo naye ashughulikiwe kadri ya kauli zake.
 
Kauli njema hiyo.

Kukemea wizi wa kura Ili kupata viongozi sahihi Kwa maendeleo ya nchi yetu ni jambo thabiti kabisa.
 
Kosa la hizo statement liko wapi? Kuwaambia vijana waamke wapiganie haki zao? Kutumia haki yao kisheria kukusanyika kwenye mkutano wa siasa?

Tatizo lenu mnasoma hizo statement mkitawaliwa na fikra potofu, fikra hasi, kwamba hizo kauli zinachochea vurugu, kwanini muogope hizo kauli kama mnaamini hamjakosea popote?

Mnajua ukweli nyie ni waovu, mnakandamiza haki za watu ndio maana hamtaki wapiganie haki zao, hivyo kwenu wao kuamka kudai haki zao, kwenu ni kauli ya hatari sababu ya uovu wenu.
Kuna Wakenya zaidi ya 50 wamefariki kwenye maandamano ya Gen Z. Kuna Wakenya zaidi ya 200 wamejeruhiwa na wanatibia majeraha kwenye hospitali mbalimbalk. Zaidi ya hapo kuna uharibifu wa mali za umma na binafsi.

Je nini vijana wa Gen Z wa Kenya walichokipata? Rutto bado ni Rais. Kavunja cabinet halafu kawarudisha nusu ya waliokuwapo.

Wazee kama kina Raila Odinga ndiyo wamefaidi kwa kuwa tayari wameingia kwenye Serikali ya Mseto.

Sasa kuwajaza jazba vijana wa Kitanzania wakadai haki kama Wakenya walivyodai siyo kitu cha kukikalia kimya. Waswahili wanasema "Ukichelea mwana kulia utalia mwenyewe"
 
Mimi sijaona matamshi hayo yana viashiria gani vya kuvunja amani au kuleta vurugu!
Ni wewe huyo hujaona kwa vile huna mafunzo yanayohusu chanzo cha ghasia, athari za ghasia na namna ya kuepuka ghasia.

Kwenye risk management hiyo inaitwa risk mitigation strategy.

Zima tukio kabla HALIJATOKEA
 
View attachment 3068006View attachment 3068007
Nimenukuu barua ya Polisi ya tarehe 11/ 08/ 2024
View attachment 3068017
Hata mbuyu ulianza kama mchicha. Twaha Mwaipaya anataka GEN Z ya Tanzania iigize yaliyotokea Kenya. Kongole Tanpol kwa hatua mliyochukua.

..Polisi wametawaliwa na HOFU.

..Kuna statement nyingine nyingi zimetolewa na Mwaipaya, na viongozi wa Chadema, na zinaashiria AMANI.

..CCM imeshindwa kuongoza nchi ndio maana inamshuku kila aliyetofauti nao kuwa anataka kuwatoa kwa nguvu.
 
Uoga tu....vibinti vile mlivovikamata vilikuwa vinaenda kuleta vurugu gani? Watu wanataka kujiwekea maazimio yao mnaleta mihemuko yenu...umbwa kabisa nyie
Mdharau mwiba huota tende!! Hata vibinti vya Kenya vilikuwa vidogo kama hivyo
 
Kuna Wakenya zaidi ya 50 wamefariki kwenye maandamano ya Gen Z. Kuna Wakenya zaidi ya 200 wamejeruhiwa na wanatibia majeraha kwenye hospitali mbalimbalk. Zaidi ya hapo kuna uharibifu wa mali za umma na binafsi.

Je nini vijana wa Gen Z wa Kenya walichokipata? Rutto bado ni Rais. Kavunja cabinet halafu kawarudisha nusu ya waliokuwapo.

Wazee kama kina Raila Odinga ndiyo wamefaidi kwa kuwa tayari wameingia kwenye Serikali ya Mseto.

Sasa kuwajaza jazba vijana wa Kitanzania wakadai haki kama Wakenya walivyodai siyo kitu cha kukikalia kimya. Waswahili wanasema "Ukichelea mwana kulia utalia mwenyewe"
Suala la waandamanaji kuuawa na kujeruhiwa, na watu kuharibiwa mali zao, hiyo yote ni uzembe wa jeshi la polisi halikuwajibika kuwalinda waandamanaji, na kulinda mali za raia wengine, sio kosa la waandamanaji.

Ruto alivunja baraza la mawaziri na kuondoa ule muswada wa sheria kandamizi, hii yote ni faida waliyopata waandamanaji kwa kumuwajibisha Rais wao.

Vijana wa kitanzania hawajajazwa jazba, wameamshwa kudai haki zao, unavyosema wamejazwa jazba ni kwasababu umetawaliwa na hisia kwenye fikra zako, hutumii akili, au labda pia una upeo mdogo ndio sababu.
 
Ni wewe huyo hujaona kwa vile huna mafunzo yanayohusu chanzo cha ghasia, athari za ghasia na namna ya kuepuka ghasia.

Kwenye risk management hiyo inaitwa risk mitigation strategy.

Zima tukio kabla HALIJATOKEA
Hakuna cho chote! Kama wangekusanyika huko na silaha ndiyo tungeamini kuna viashiria vya kuvunja amani.
Inaonekana bado Chadema ni homa ya Chama pendwa hasa kipindi hiki kinachokaribia uchaguzi!
 
View attachment 3068006View attachment 3068007
Nimenukuu barua ya Polisi ya tarehe 11/ 08/ 2024
View attachment 3068017
Hata mbuyu ulianza kama mchicha. Twaha Mwaipaya anataka GEN Z ya Tanzania iigize yaliyotokea Kenya. Kongole Tanpol kwa hatua mliyochukua.

Yaani Jeshi lisamamishe mikutano kwasababu ya kauli ya mtu. Mbona Nape alikuwa anaongea vitu kila siku ni lini mkutano wa CCM umesimamishwa!! ni lini makamu mwenyekiti na watu wamewekwa jela! Hivi ni utamaduni gani huu wa vijana wajinga jinga kila siku kutafuta kiki! mtakuja kuishi nchi ya ajabu sana miaka ijayo mnatakiwa kupenda jitihada za kuweka usawa na katiba mpya bila hivyo mtakuwa wafanyakazi wa watoto na wajukuu wa vigogo milele
 
Back
Top Bottom