Napata shida kidogo kuona makosa ya Twaha hapo.
Hii inaibua maswali kadhaa,Ukinijibu tutaelewana.
1.Tunaenda kuweka hatma ya Taifa letu,kijana yoyote njoo uwanja wa Ruanda mbeya.Je kuweka hatima ni kosa?
2.Kuna viongozi wamekamatwa kwa kosa la kusafiri kuja Mbeya.Je mtu kuja Mbeya ni kosa?
3.Kujitambua kama Vijana wakenya,
Kuna jinai gani hapo.Kuna viashiria vipi kwamba mkutano utafanya maandamano kama ya kenya.
Vipi angesema tunaendakujitambua kama vijana wa CCM walivyo jitambua kungekua na kosa?
Haya ni madhara ya kufanya maovu serikalini kwa hiyo kila ukiona kuna dalili ya watu kuamka na kuhoji wewe unajihisi ni wewe unaepingwa.
Hao polisi itafika muda watakuwa hawana nguvu tena ya kudhibiti haya maandamano na watakuwa wakwanza kuomba maridhiano lakini wayakuwa wamechelewa.