Kwa kauli hii ya Waziri, kuna moto unafukuta Diamond Vs Serikali (Hakuna Msanii Mkubwa Kuliko Nchi)

Serikali yetu ipo tu kwa kuropoka lakin ukiwauliza ni kitu gan wamewah kiwaboost wasanii hakuna
 
Wasanii wa nchi za dunia ya kwanza huwezi linganisha na hawa wakina Steve Nyerere au Masanja Mkandamizaji.

Kule shule ipo na kichwani wapo vizuri vile vile.

Huku msanii kakulia kwenye kula ugali kila siku usitegemee kamwe awe vizuri kwenye lolote.
Huijui historia ya Arnold Schwarzeneeger vizuri wewe, umechanganywa na RANGI yake tu.
 
Mimi mtazamo wangu naona kuwa kuwa haya ni masuala madogo kwa sababu yule haendi kulopoka bali kusemq yale atakuokua akiagizwa kuyasema. Ingekua mfumo unaoutaka uwe hivyo unavyopendekeza basi tusingekua na afisa habari wa TLS ambaye sio wakili wala mwanasheria kwenye chama cha madaktari yaani kila tasnia isiwepo na watu nje ya tasnia, nadhani haiwezekani.
Mbona mawaziri wengi wanasimamia wizara ambazo sio wanataaluma nazo?
 

Ni kweli mkuu kwa ulichokisema 💯

Lakini watu wanadhani usemaji ni suala la kuongea ongea tu, kuwa spokeperson ni kuishikilia brand nzima ya wasanii na kuwa sura na sauti ya watu unaowawakilisha

Kama wasanii wameona steve hastahili kuwa utambulisho wao, mimi ni nani nipinge.
By the way nilikuwa na mashaka mwanzoni ila kwa clips nilizoziona kuhusu press conference aliyoiitisha iliyojaa character assasination na jazba, hata mimi naona hastahili, wasanii wapo sawa kabisa
 
Mbona Ukraine mchekeshaji amekua kiongozi wa nchi?

US pia ilikua na raisi ambaye alikua mcheza sinema?

Arnold Schwarzeneeger ambaye ni mcheza sinema ila alikuja kua Gavana wa jimbo la California?

Rais wa Ukraine amesoma (LLB).

Ronald Reagan bila shaka ndio unamtaja amesomea (BA Economics/Sociology).

Arnold Schwarzenegger amesoma BA(Business Administration/Fitness Marketing).
 
Diamond ni mkubwa kuliko huyo wazir.. wazir atashindwa hyo vita... Wanaomback diamond ni wakubwa mno.. diamond amekua taswira ya nchi.. na ncho haiko tayar kumpoteza
 
Rais wa Ukraine amesoma (LLB).

Ronald Reagan bila shaka ndio unamtaja amesomea (BA Economics/Sociology).

Arnold Schwarzenegger amesoma BA(Business Administration/Fitness Marketing).
So,msemaji anatakiwa asome level ipi? Nimejibu hoja iliyisema "Mchekeshaji hawezi kua msemaji wa wana muziki"

Msemaji sio decision maker,ni muwasilishaji tu wa kinacho ongewa na wahusika wa idara husika,
Msemaji wa Tanesco sio lazima awe fundi umeme.
 
Hao wote uliowataja walipita kwa BALLOT PAPER na wakakubalika na waliowapigia kura.

STEVE hajapigiwa kura na hao anaowaongoza Hawamtaki, mbona unachanganya Mambo.

Mifano uliyoitoa haifanani
Kwahiyo Steve amepitaje mpaka kufikia hapo alipo?

Mifano yangu imetokana na comment niliyoiquote kua "Mchekeshaji hawezi kua msemaji wa wanamuziki"
 
Ideally, inatakiwa awe angalau amesomea field mojawapo kati ya public relations, journalism, mass communication etc. Kwa taasisi kubwa watataka na uzoefu katika tasnia usika, kama ni masuala ya umeme, afya etc. utaambiwa hiyo ni added advantage.

Kwa common sense atakayeyazungumzia mambo ya wanamziki lazima awe na ufahamu wa hali na changamoto zaidi za anaowawakilisha, kwa sababu sekta ya muziki ndio imeanza kukua kwa miaka ya karibuni na kuingia kibiashara zaidi. Kwa kuanza ingekuwa na maana zaidi kama angetoka kati ya wanachama wa hilo shirikisho na alitakiwa apelekwe angalau hata kozi fupi zitakazomuongoza kwenye hayo majukumu yake.

Tatizo Bongo tulishajiwekea msemaji ni mtu anayeweza kutoa maneno ya shombo mbele ya media na kiki za hapa na pale.

Kwa baadhi ya wanaompinga Steve nimewaelewa zaidi kwa madai yao kwamba nafasi hiyo inampa majukumu mawili ( Spokesperson+Chief Strategist).
 
Mbona Ukraine mchekeshaji amekua kiongozi wa nchi?

US pia ilikua na raisi ambaye alikua mcheza sinema?

Arnold Schwarzeneeger ambaye ni mcheza sinema ila alikuja kua Gavana wa jimbo la California?

Tatizo sio uchekeshaji ila huyu ni mchekeshaji asiye na weledi wa mambo ya music.

Tivu hata common sense tu hana let alone technicalities za mambo ya music. Hafai kuwa kiongozi wa kada yeyote labda familia yake.

Tivu ake hajui hata utamshi wa maneno ukimsikiliza ni kituko tu. Hii ishu ni kituko all around.

FidQ ameniangusha sana kwenye hii ishu.
 
Mchengerwa anafurahisha genge.

Kilq Waziri anakuja na matamko. Hakuna mikakati wala utekelezaji.

Wasanii tuna maoni mengi mazuri wameyafutika kwenye shajara, lakini utasikia kila siku LETENI KERO ZENU.

Wasitufanyie hadaa
Mkuu naomba japo nisikilize EP yako
 
Issue inayozungumziwa hapo ni mchekeshaji kuwa kiongozi wa muziki, sijui umenipata?
Sema Boda Tz..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ukraine wamempa Uraisi kabisa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…