Kwa kauli hii ya Waziri, kuna moto unafukuta Diamond Vs Serikali (Hakuna Msanii Mkubwa Kuliko Nchi)

Leo ndo nimejua diamond ni Simba mpak serikali haimpend lakin anazid kutembea ma mbele uko
 
Kwa wenye akili wameshajua Waziri yupo upande wa Diamond.... Anawataka Basata kumaliza tofauti zao na msanii huyo kwa kumnyenyekea na sio kuoneshana mabavu
 
Issue hii ameitolea maelezo vizuri sana mbunge wa muheza BW. Hamisi mwinjuma kwamba shirikisho lina katiba yao Kwaio uteuzi ule haujafuata katiba na aliyeteuliwa Hana sifa zinazoainishwa Kwenye katiba ndo maana hawamtaki.
 
Mbona Ukraine mchekeshaji amekua kiongozi wa nchi?

US pia ilikua na raisi ambaye alikua mcheza sinema?

Arnold Schwarzeneeger ambaye ni mcheza sinema ila alikuja kua Gavana wa jimbo la California?
Ronald Reagan Mzee NWO alikuwa star wa Hollywood,akawa rais na akaipaiaha US na kuikalisha USSR kuelekeo mwisho vita baridi.
 
Hao wote uliowataja walipita kwa BALLOT PAPER na wakakubalika na waliowapigia kura.

STEVE hajapigiwa kura na hao anaowaongoza Hawamtaki, mbona unachanganya Mambo.

Mifano uliyoitoa haifanani
Issue ya Steve naona mnaipaisha bure tuu hivi kuwa msemaji ni tatizo kweli?? Haji Manara si ni msemaji? Yaani vikao vinakaa na kufanya maamuzi then msemaji anaujulisha umma yaliyoamuliwa au mimi ndiyo sijaelewa??
 
Hivi ili useme madaktari ni lazima na wewe uwe daktari? Yaani wewe kazi yako ni kuujulisha umma yale ambayo madaktari wameazimia kwenye vikao na mikutano yao..
 
Wasanii wa nchi za dunia ya kwanza huwezi linganisha na hawa wakina Steve Nyerere au Masanja Mkandamizaji.

Kule shule ipo na kichwani wapo vizuri vile vile.

Huku msanii kakulia kwenye kula ugali kila siku usitegemee kamwe awe vizuri kwenye lolote.
Na wewe ni msanii?
 
Kama wewe ni afisa habari mzuri, na inayejua kazi yako basi unaweza kabisa leo kuwa msemaji wa madaktari, kesho msemaji wa wafugaji etc etc cha msingi ni kujua lengo kuu shirikisho linalokuajiri au kukupa kazi, kujua changamoto zake, kujua nini wanakipigania etc.. Mambo mengi watakupa wao kupitia vikao vyao ili uwahabarishe umma na pia utapewa mipaka ya mambo wasiyopenda. Sasa kuhusu wasanii nadhani kwanza hawako organized kabisa kwa jinsi nilivyoona majibizano yao kwenye kikao. Pia ili kupata muafaka kwa wote pale mnapokuwa hamkubaliani ilitakiwa wapeane muda wa kutosha wa kujadili hilo jambo na ikibidi waitishe mkutano mkuu wenye maamuzi ya mwisho. Kingine waache kudharauliana kati ya bongo fleva, taarabu, mziki wa dansi, singeli, gospel na categories nyingine maana kuna wanaojiona wao ndiyo shirikisho kuliko wengine.
 
Diamond ni mkubwa kuliko huyo wazir.. wazir atashindwa hyo vita... Wanaomback diamond ni wakubwa mno.. diamond amekua taswira ya nchi.. na ncho haiko tayar kumpoteza
Sasa kama ni mkubwa kuliko huyo waziri si aunde shirikisho lake mwenyewe? Majuzi tuu alisikika akilalamika kuwa kila akienda nje ya nchi analipushwa elfu 50 pale airport na eti hajui za nini. Basata wakamjibu kuwa ndiyo utaratibu kwani kuna kanuni inayomtaka msanii akienda nje ya nchi ku perfom anapata kibali ambacho malipo yake ni elfu 50. Niajabu kwa msanii mnayesema mkubwa na mwenye management kushindwa kujua taratibu simple za serikali kama hizi.
 
Diamond kazidi Sana dharau anataka kujiona yupo kuliko serikali anaishi enzi za makonda sasa ngoja wamnyosheee .

Basata na wizara wamewapa sana mualiko akawa anawatuma akina fella tu ye haendi sasa Kazi hajapeleka na hata kama angeona ina mapungufu busara ni kupeleka afu ndiyo utoe ushauri wakati hatua zingine zinaendelea . Tofaut na hapo hii mtifuano haboi akijifanya mjanja sana wanamsogezea tra hapo wamuulize vizur
 
Ana tabia mbovu mbovu kama zipi? Vp kuhusu Diamond yeye hana tabia mbovu mbovu?
Kama kutunga nyimbo za tia mate iteleze, kufukua mitaro... Actually huyu dogo tabia zake za kitaani kupiga mademu na kuwaacha zinaakisi kabisa nyimbo zake na mfumo wake wa maisha usiofaa kuigwa na vijana wetu.
 
Diamond anatakiwa ajue kusoma alama za nyakati kipind hiki akileta nyodo watamnyonyoa vibaya

Kipind cha makonda aligombana na familia ya msoga na hata kudharau mawaziri wote kisa tu makonda anamlinda mwambie nyakati zimebadilika
 
WCB tumesema hivi "endeleeni na tuzo zenu bila sisi kushiriki"

Mbona mambo yanazidi kuwa mengi, tulishakataa kuingia kwenye nomination tangu enzi zile za Tuzo za Kili
 
Kikubwa ulichokisema ni kuwa afisa habari mzuri, ukiangalia wasemaji au maafisa habari wanaoteuliwa kuwakilisha makampuni au mashirikisho, wengi ni watu wenye chimbuko la vyombo vya habari, kada ya mawasiliano au Public relations

Sababu kubwa ni kuwa hawa watu wanajua kuongea professionaly, kuandaa materials ya media na pia wana ujuzi katika kujibu maswali ambacho ni kitu muhim sana. Sasa kama wanataka kupata mtu mzuri bhasi waangalie vigezo vyao
 
Hivi ili useme madaktari ni lazima na wewe uwe daktari? Yaani wewe kazi yako ni kuujulisha umma yale ambayo madaktari wameazimia kwenye vikao na mikutano yao..
Na unatakiwa kuwa na uwezo wa kujibu maswali pale unapoulizwa tena kwa ufasaha,
Na hili haliwezi kufanyika kama huijui industry yako nje ndani na uwezo binafsi wa kujua mipaka yako yako plus emotional intelligence

usemaji sio usomaji au kazi ya copy and pasting. Ingekuwa ni rahisi hivyo bhasi wangekuwa wanachukua Tu hata secretary anaendaa minutes za vikao ili awasilishe hayo mawazo kama ana uwezo wa kuongea, ila wanachagua kuwekeza pesa ili wapate mtu the best watakaemlipa sawa na thamani ya brand yao

Kumbuka neno la msemaji ni neno la shirikisho kiujumla kwa hiyo akibugi step anadhalilisha shirikisho zima. It's a matter of brand sio uwezo wako wa kupayuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…