Uchaguzi 2020 Kwa kauli hizi za Dkt. Magufuli, Je atakuwa tayari kuachia madaraka kama atashindwa Uchaguzi?

Uchaguzi 2020 Kwa kauli hizi za Dkt. Magufuli, Je atakuwa tayari kuachia madaraka kama atashindwa Uchaguzi?

VIVIANET

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2015
Posts
2,129
Reaction score
2,918
Ndugu zangu wapendwa naomba tutafakari kwa kina kuhusu kauli zilizotolewa na Magufuli kwamba hayupo tayari kuacha taifa likaangamia, liingie mikononi mwa matapeli na waongo.

Kwa kauli hizi inaonyesha wazi, kwamba Magufuli yeye tu ndio mtakatifu na mwaminifu, ila wagombea wengine ni matapeli na waongo. Sasa swali langu ni hili je hao matapeli na waongo wakichaguliwa na wananchi yeye atakubali kuachia madaraka?

Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa ndugu yetu anaamini peke yake ndiye anayestahili kuliko wananchi wengine wote. Kama wananchi wameona hao ni watu sahihi wewe ni nani hata useme ni matapeli? Je hii siyo dalili ya kubaki madarakani kwa nguvu? Nini maana ya Uchaguzi? Kwani taifa linakuwa tu salama likiwa mikononi mwake?

Je hili taifa siyo mali ya Mungu? Ni nani anayeweza kulifanya taifa liwe salama zaidi ya Mungu?

Naomba tujadili maana hii kauli imenishitua sana.
 
Huyu Magufuli ni tatizo zaidi ya matatizo ya nchi.

Na hasa anapojiona yeye ni mwema kuliko wenzake na kumbe ndiye mbovu kuliko wote ila anabebwa na mfumo aliouandaa tu, lkn ingekuwa haki bin haki ,hoja kwa hoja asingepata hata kura 1M
Sema kwavile sisi watz ni bora uzima kuliko haki ya mtu basi watuburuze tu
 
Yeye ndio mzalendo peke yake wengine wote ni matapali
 
Ashindwe uchaguzi kwa lipi hasa? Kwa hizi sera za kudalalia mabeberu raslimali za Taifa na kueneza ushoga kwa mgongo wa haki za binadamu na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza.
 
Je na chadema kama magufuli akishinda mko tayari kukubali na msisingizie kuwa mmeibiwa kura? Maana nyie wenyewe mmetangaza mtaingia porini.

Chadema wanayo haki ya kutoamini kushindwa kutokana na utendaji wa tume. ni mgombea yupi wa ccm amewahi kuenguliwa?

Kwa nini wakurugenzi walikuwa wanawahujumu wapinzani wakati wa mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu?

Kwa nini Magufuli aliwahi kutamka kwamba hawezi kukubali mkurugenzi amtangaze mpinzani kwa sababu anamlipa yeye? Kwa hiyo chadema wanasimamia kauli na matendo ya serikali
 
Back
Top Bottom