Kwa kauli ya Rais Samia aliyoitoa mbele ya Mabalozi imeonyesha alikusudia kabisa kilichotokea Oktoba 29

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
2,268
Reaction score
7,119
Nimeshangaa sana mimi kama Mwalimu.

Rais Samia pia alikiri changamoto zilizotokea kutokana na vurugu na ukosefu wa utulivu siku ya uchaguzi na muda mfupi baada yake, akisema:

“Licha ya mafanikio haya makubwa, kwa masikitiko tunatambua changamoto zilizotokea kutokana na vurugu na ukosefu wa utulivu siku ya uchaguzi na muda mfupi baada yake. Hatua tulizochukua zilikuwa muhimu ili kudumisha utaratibu wa Kikatiba na kuhakikisha usalama wa Wananchi wote pamoja na Jamii ya Kidiplomasia.”

Kuna watu watakuja watasema waliouawa walikuwa waharifu. Huu ni upuuzi. Sikatai kuwa kuna uharifu ulifanyika. Lakini mharifu wa kupora na kukwapua mali madukani ambae hana silaha anastahili kupigwa risasi?

Watu kuimba kuwa wanataka yaliyotokea Madagascar yatokee hapa nchini ili Samia aondoke ni kosa ? Mpaka wamiminiwe masasi?

Leo hii bila hata aibu anakili mbele ya ulimwengu kuwa watu walipigwa risasi ili abaki madarakani.

Vipi kuhusu DP world ya waaarabu kupewa bandari? Mradi wa bandari Bagamoyo ambao Kikwete ameulazimisha kwa nguvu zote?

Mwalimu muuza Kangala.
 
Lakini mharifu wa kupora na kukwapua mali madukani ambae hana silaha anastahili kupigwa risasi?
Ulivyojitambulisha kama mwalimu nilisoma kwa umakini nikidhani nitaambulia madini kumbe mashudu matupu. Yaani mtu aliyeenda kuchoma kituo cha mafuta unataka achekewe? Halafu kilichotokea tarehe 29 Oct 2025 ni jaribio la mapinduzi lililofeli. Na baada ya jaribio la mapinduzi serikali yoyote duniani huchukua hatua chungu sana ili kuleta utulivu. Halafu pia acha unafiki... wewe ni miongoni mwa watu mnaoongoza kuwaua wezi wa kuku kwa kuwachoma moto hadharani mkijiita kuwa ni wananchi wenye hasira kali. Atakayethubutu kurudia kufanya ya tarehe 29 asije akalaumu.
 
Nimeshangaa sana mimi kama Mwalimu.

Rais Samia pia alikiri changamoto zilizotokea kutokana na vurugu na ukosefu wa utulivu siku ya uchaguzi na muda mfupi baada yake, akisema:

“Licha ya mafanikio haya makubwa, kwa masikitiko tunatambua changamoto zilizotokea kutokana na vurugu na ukosefu wa utulivu siku ya uchaguzi na muda mfupi baada yake. Hatua tulizochukua zilikuwa muhimu ili kudumisha utaratibu wa Kikatiba na kuhakikisha usalama wa Wananchi wote pamoja na Jamii ya Kidiplomasia.”

Kuna watu watakuja watasema waliouawa walikuwa waharifu. Huu ni upuuzi. Sikatai kuwa kuna uharifu ulifanyika. Lakini mharifu wa kupora na kukwapua mali madukani ambae hana silaha anastahili kupigwa risasi?

Watu kuimba kuwa wanataka yaliyotokea Madagascar yatokee hapa nchini ili Samia aondoke ni kosa ? Mpaka wamiminiwe masasi?

Leo hii bila hata aibu anakili mbele ya ulimwengu kuwa watu walipigwa risasi ili abaki madarakani.

Vipi kuhusu DP world ya waaarabu kupewa bandari? Mradi wa bandari Bagamoyo ambao Kikwete ameulazimisha kwa nguvu zote?

Mwalimu muuza Kangala.
kwenye r weka l ili tukutambue kama ni mtanzania
 
Back
Top Bottom