Kwa Kichagga zinaitwa "ngoda" sijawahi kuziona popote zaidi ya Moshi. Zinaitwaje kwa kiswahili?

Kwa Kichagga zinaitwa "ngoda" sijawahi kuziona popote zaidi ya Moshi. Zinaitwaje kwa kiswahili?

Chanika zipo, tena mti wake umeota makaburini watoto kila Sikh wanaangua....Zinaitwa Ngweda sio ngoda
 
Hizi sii helimu kweli?? Je zipo sehemu nyingine pia Tanzania???

Hapa Dar wanauza wapi?
hizo sio helimu ndugu, helimu ni kubwa kwa hizi,na pia helimu nyama (tunda) halijashikana na mbegu ya ndani,hizi nyama imeshikana na mbegu ya ndani na inabidi kuimung'unya (sijui kama ni kiswahili hiki)
 
umenikumbusha enzi hizo primary school moshi tulikua tunaziita konazi
 
Hizi ni tunda zinaitwa Ngoda,miiti yake ni mikubwa kama miparachichi tu. Kwa mwaka zinatoka mara 1 tu misimu ya miezi ya 12 mpka mwezi wa kwanza mwanzoni.

Ladha yake ni chachu kwa umbali kama embe dodo ambalo halijaiva vizuri yani ina ugwadu kwa mbali. Ukila nyingi sana hutaweza kutafuna kitu sababu meno yatauma. Ila ni nzuri sana.
Zina umbo kama la zambarau

Je kwenu zipo? Zinaitwaje?
View attachment 1587998

Ngweda, miaka ya tisini huko tulikuwa tunakwenda msitu wa Njoro kufuata hizi makitu na mikongoraaa!!

Ule msitu sijui bado upo vile??
 
Hizi ni tunda zinaitwa Ngoda,miiti yake ni mikubwa kama miparachichi tu. Kwa mwaka zinatoka mara 1 tu misimu ya miezi ya 12 mpka mwezi wa kwanza mwanzoni.

Ladha yake ni chachu kwa umbali kama embe dodo ambalo halijaiva vizuri yani ina ugwadu kwa mbali. Ukila nyingi sana hutaweza kutafuna kitu sababu meno yatauma. Ila ni nzuri sana.
Zina umbo kama la zambarau

Je kwenu zipo? Zinaitwaje?
View attachment 1587998
Mkuu samahani nikunyooshe kidogo zinaitwa Ngweda mti wake ni mithili ya mti maji tena inaota pembezoni mwa mito ukifika Moshi mjini nenda pale chem chem idara ya maji ipo kama 7 hivi ni matunda murua yenye radha
 
Back
Top Bottom