Kwa kigezo hiki, Mbappe atashinda Ballon d'Or mwaka 2026?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Lamine Yamal ameshinda Kombe la Dunia – lakini je, nyota huyo chipukizi wa Hispania amefanya vya kutosha kumpiku Harry Kane, Kylian Mbappé, Ousmane Dembélé katika mbio za Ballon d'Or?, Baada ya enzi ya utawala wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kuelekea ukingoni, ushindani wa tuzo ya Ballon d'Or umekuwa mkali.

Ballon d'Or Power Rankings 207.jpg.webp

Waandaaji wa tuzo ya Ballon d'Or wameeleza kuwa kushinda Kombe la Dunia pekee hakutoshi kumhakikishia mchezaji kutwaa tuzo hiyo ya kifahari. Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya tuzo hiyo, wamebainisha kuwa mafanikio katika Kombe la Dunia ni miongoni mwa vigezo muhimu, lakini si kigezo cha moja kwa moja cha kushinda Ballon d'Or.

1784800063563.png

Kwa upande wa Kylian Mbappé, mshambuliaji huyo alikuwa na msimu bora wa 2025/26, akifunga mabao 25 na kutoa asisti 5 katika mechi 31 za La Liga na kuibuka mfungaji bora wa ligi hiyo. Katika UEFA Champions League, alifunga mabao 15 katika mechi 11 na pia kumaliza akiwa kinara wa ufungaji.

Katika Kombe la Dunia 2026, Mbappé alifunga mabao 10 na kutwaa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu (Golden Boot), huku akiweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa mashindano hayo akiwa na mabao 22.

1784797855120.png

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tangu mwaka 1995, ni wachezaji wanne pekee kati ya saba walioweza kushinda Ballon d'Or baada ya kutwaa Kombe la Dunia, ikiwa ni asilimia 57 pekee. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa ushindi wa Kombe la Dunia haujawa dhamana ya kupata tuzo ya Ballon d'Or.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa ili mchezaji ashinde Ballon d'Or, anapaswa kuwa ndiye aliyekuwa bora zaidi katika msimu mzima wa soka, na si kwa kiwango alichoonyesha kwenye Kombe la Dunia pekee. Waandaaji wa tuzo hiyo wamesisitiza kuwa tathmini huzingatia mchango wa mchezaji katika mashindano yote ya msimu, si mafanikio ya mashindano ya Kombe la Dunia pekee.

Ballon d'Or 2026 Power Rankings:
  1. Lamine Yamal (Barcelona/Hispania)
  2. Harry Kane (Bayern Munich/Uingereza)
  3. Lionel Messi (Inter Miami/Argentina)
  4. Rodri (Manchester City/Hispania)
  5. Ousmane Dembélé (Paris Saint-Germain/Ufaransa)
  6. Kylian Mbappé (Real Madrid/Ufaransa)
  7. Michael Olise (Bayern Munich/Ufaransa)
  8. Jude Bellingham (Real Madrid/Uingereza)
  9. Erling Haaland (Manchester City/Norway)
  10. Khvicha Kvaratskhelia (Paris Saint-Germain/Georgia)
Orodha hii ni makadirio (Power Rankings) yanayoonyesha wachezaji wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kuwania tuzo ya Ballon d'Or 2026 kulingana na kiwango chao katika msimu, na si orodha rasmi ya walioteuliwa.
 
Fabian Ruiz hayupo hapo?
 
Ballon d'Or ni tuzo ambazo zimepungua credibility, kuna mambo ya siasa yameingia kwenye hizo tuzo.

Tuzo ambazo zinamlenga mchezaji binafsi, inakuwaje tena hazijikiti kwenye takwimu za mchezaji binafsi bali zinaangazia kwenye mafanikio ya timu?

Kama unatoa tuzo kwa kuangalia performance ya mtu, sioni maana yeyote ya kuangalia mafanikio ya timu ikiwa kiujumla, vinginevyo iitwe tuzo ya timu sio mchezaji binafsi.

Mbappe, Kane wamefanya makubwa lakini hiyo tuzo ni kama wanatafutwa wachezaji ambao timu zao zimechukua makombe fulani fulani.

Wachezaji hao ukiwapima kwa individual performance dhidi ya Mbappe na Kane, hawafiki hata nusu ya walichokifanya hawa jamaa wawili.

Ballon d'Or mara nyingi hai define ubora wa mchezaji, ina define una ushawishi gani ndani ya mfumo kuweza kusababisha upigiwe kura.

Tuzo yeyote inayopatikana kwa kura, kwangu mimi sijawahi kuiona kama ina mantiki yeyote.

Kocha wa Sudan aliwahi kulalamika kuwa 2019 alimpigia kura Mo Salah lakini alishangaa kuona kwenye list ya kura, FIFA wamechapisha kuwa alimpigia Messi.

Haya ni mambo ambayo yanafanya niheshimu sana tuzo anayopewa mfungaji bora kwasababu ni tuzo ambayo haihitaji vikao wala mjadala tofauti na hizo tuzo zingine ambazo watu wanaweza kumpa yule wanayemtaka tu kwasababu ya wingi ws kura au ku bend baadhi ya sheria.
 
Onesha uwezo upate tuzo.
 
Kama ni Performance ya mtu basi Rodri, Mbape sio wa kukosa juu kabisa lakini Kwa timu kuchukua makombe basi no doubt Fabian Ruiz anastahili kuchukua....
 
Back
Top Bottom