Kwa kigezo hiki, Mbappe atashinda Ballon d'Or mwaka 2026?

Kwa kigezo hiki, Mbappe atashinda Ballon d'Or mwaka 2026?

Uwezo wa kuwa na convincing power kwenye cabinet ya waandaji?

Au labda unipe tafsiri yako ya maana ya neno uwezo ambayo ina pingana na takwimu walizonazo Mbappe na Harry Kane.
Hivyo ndivyo watangulizi nguli wa hivi karibuni walivyopata hizo tuzo mfululu, sio kila Ballon d'Or ya Messi au Cr 7 ilikua ya haki isiyo na malalamiko ila ndo ivo kuna namna wakuu wao walicheza na system.

Ukipinga basi njoo na wazo lako but mind you, dunia haina haki.
 
Hivyo ndivyo watangulizi nguli wa hivi karibuni walivyopata hizo tuzo mfululu, sio kila Ballon d'Or ya Messi au Cr 7 ilikua ya haki isiyo na malalamiko ila ndo ivo kuna namna wakuu wao walicheza na system.

Ukipinga basi njoo na wazo lako but mind you, dunia haina haki.
Ndio maana nasema kujaji ubora wa mchezaji kwa kuangalia tuzo sioni kama ni njia sahihi kwasababu hizo tuzo ni mara nyingi zimekuwa rigged.
 
Kwa kuwa ni mweusi hatopewa!
Mtu kaongoza La Liga kwa mabao, UEFA Champions, na World Cup 2026, na kachezq mpaka nusu fainali.
Lakini hatopewa, watampa Rodri. Watasema ni kiungo bora wa mashindano. 😊
 
Wampe Yamal tu ..Rodri na fabian Ruiz awastahili kupewa iyo tuzo wote nusu ya msimu kwenye timu zao walikuwa majeruhi leo mtu acheze mechi 8 uniambie ni bora si ushubwada uwo..Yamal kafanya kila kitu kuanzia ngazi ya klabu mpala WC
 
Kwa kuwa ni mweusi hatopewa!
Dembele wakati anachukua hiyo tuzo alikuwa mweupe?
Mtu kaongoza La Liga kwa mabao, UEFA Champions, na World Cup 2026, na kachezq mpaka nusu fainali.
Kwahiyo unataka apewe kwa sababu kaongoza kwa mabao?

Kwahiyo kigezo cha Ballon d'or kiwe kuongoza kwa mabao na kucheza nusu fainali?

Wakati anachukua Dembele mfungaji bora UEFA alikuwa Raphina na Guirassy kwa kigezo chako wao walistahili zaidi kuliko Dembele?
 
Kwa ajili ya performance binafsi pamoja na mchango ulioutoa kwa timu.
Mchango ulioutoa kwenye timu ndio performance binafsi. Usifanye kama ni vitu viwili tofauti.

Mchango wako binafsi unaweza kuonekana wala haihusiani na timu yako kubeba kombe.

Mfano, striker role yake yeye ni kufunga. Utamuhukumu vipi kwamba hajaweza kuibeba mechi kwenye mechi ambayo alifunga hattrick na timu yake ikafungwa bao 4?
 
Lamine Yamal ameshinda Kombe la Dunia – lakini je, nyota huyo chipukizi wa Hispania amefanya vya kutosha kumpiku Harry Kane, Kylian Mbappé, Ousmane Dembélé katika mbio za Ballon d'Or?, Baada ya enzi ya utawala wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kuelekea ukingoni, ushindani wa tuzo ya Ballon d'Or umekuwa mkali.


Waandaaji wa tuzo ya Ballon d'Or wameeleza kuwa kushinda Kombe la Dunia pekee hakutoshi kumhakikishia mchezaji kutwaa tuzo hiyo ya kifahari. Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya tuzo hiyo, wamebainisha kuwa mafanikio katika Kombe la Dunia ni miongoni mwa vigezo muhimu, lakini si kigezo cha moja kwa moja cha kushinda Ballon d'Or.


Kwa upande wa Kylian Mbappé, mshambuliaji huyo alikuwa na msimu bora wa 2025/26, akifunga mabao 25 na kutoa asisti 5 katika mechi 31 za La Liga na kuibuka mfungaji bora wa ligi hiyo. Katika UEFA Champions League, alifunga mabao 15 katika mechi 11 na pia kumaliza akiwa kinara wa ufungaji.

Katika Kombe la Dunia 2026, Mbappé alifunga mabao 10 na kutwaa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu (Golden Boot), huku akiweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa mashindano hayo akiwa na mabao 22.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tangu mwaka 1995, ni wachezaji wanne pekee kati ya saba walioweza kushinda Ballon d'Or baada ya kutwaa Kombe la Dunia, ikiwa ni asilimia 57 pekee. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa ushindi wa Kombe la Dunia haujawa dhamana ya kupata tuzo ya Ballon d'Or.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa ili mchezaji ashinde Ballon d'Or, anapaswa kuwa ndiye aliyekuwa bora zaidi katika msimu mzima wa soka, na si kwa kiwango alichoonyesha kwenye Kombe la Dunia pekee. Waandaaji wa tuzo hiyo wamesisitiza kuwa tathmini huzingatia mchango wa mchezaji katika mashindano yote ya msimu, si mafanikio ya mashindano ya Kombe la Dunia pekee.

Ballon d'Or 2026 Power Rankings:
  1. Lamine Yamal (Barcelona/Hispania)
  2. Harry Kane (Bayern Munich/Uingereza)
  3. Lionel Messi (Inter Miami/Argentina)
  4. Rodri (Manchester City/Hispania)
  5. Ousmane Dembélé (Paris Saint-Germain/Ufaransa)
  6. Kylian Mbappé (Real Madrid/Ufaransa)
  7. Michael Olise (Bayern Munich/Ufaransa)
  8. Jude Bellingham (Real Madrid/Uingereza)
  9. Erling Haaland (Manchester City/Norway)
  10. Khvicha Kvaratskhelia (Paris Saint-Germain/Georgia)
Orodha hii ni makadirio (Power Rankings) yanayoonyesha wachezaji wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kuwania tuzo ya Ballon d'Or 2026 kulingana na kiwango chao katika msimu, na si orodha rasmi ya walioteuliwa.
Lamine.
 
Back
Top Bottom