Dembele kafanya kipi cha maana , individual performance kazidiwa mpaka na kvara.
Dembele hamna kitu hapa hata ni zali tu lilimtokea lakini mchezaji wa kawaida sana.
Ni kweli, ni kwasababu alikuwa majeruhi lakini mchango wake kwa timu kuchukua champion ulikuwepo tena mkubwa tu na hata kombe la dunia alikuwa vizuri ni vile tu kuna mbape ambae ametumika kama straiker lkn bado alikuwa na mchango mkubwa tu
Ukijumlisha na champion na ligi na kufika nusu fainali anastahili kuliko kane ambae ana magoli mengi ya farmer ligi na kombe la mkulima bila champion, lakini pia hata safari yao kwenda nusu fainali timu walizokutana nazo sio sawa na za ufaransa bado simpi kura yangu kushinda balon dior
Yamal ndio kabisaa, kabebwa na wachezaji kama rodri, cubersi na luiz bila hawa yule mtu wa chenga angeigharimu sana spain
Rodri bado simpi kura maana city hakufanya maajabu, city ya msimu huu ilikuwa liverpool iliyochangamka
Luiz kachukua yote ligi, champion na kombe la dunia lakini mara nyingi alikuwa akitokea bench kwa maana sio mchezaji tegemewa katika timu
Mbape ni magoli tu ambayo kayapata kwa ubinafsi mara nyingi hachezi kuibeba timu yeye anataka kufunga pekeake ndio maana timu alizochezea hazichezi mfumo wa timu kwanza mchezaji baadae wana ule ukoloni wa ronaldo hapa simpi kura kabisaa
Kwangu mimi Dembele anastahili kuliko hao wengine, messi ndio kabisaa maana mechi za kombe la dunia pekeake hadi fainal hazitoshi kumpa balon dior