Kwa kigezo hiki, Mbappe atashinda Ballon d'Or mwaka 2026?

Dembele wakati anachukua hiyo tuzo alikuwa mweupe?

Kwahiyo unataka apewe kwa sababu kaongoza kwa mabao?

Ndio, kuwa mfungaji bora tournaments tatu, La Liga, Champions League na WC, na kuwa mfungaji bora wa muda wote WC sio kitu kidogo. Goli 10 tournament moja na goli 21, tournament tatu sio jambo dogo!

Goli 10, WC yenye timu 48, mechi 104, sio jambo dogo. Mpira ni magoli, CR7, Messi amewahi pewa hii tuzo kwa kuongoza tuu ufungaji bora La Liga.
 
Lamine Yamal ameshinda Kombe la Dunia – lakini je, nyota huyo chipukizi wa Hispania amefanya vya kutosha kumpiku Harry Kane, Kylian Mbappé, Ousmane Dembélé katika mbio za Ballon d'Or?, Baada ya enzi ya utawala wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kuelekea ukingoni, ushindani wa tuzo ya Ballon d'Or umekuwa mkali.

Waandaaji wa tuzo ya Ballon d'Or wameeleza kuwa kushinda Kombe la Dunia pekee hakutoshi kumhakikishia mchezaji kutwaa tuzo hiyo ya kifahari. Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya tuzo hiyo, wamebainisha kuwa mafanikio katika Kombe la Dunia ni miongoni mwa vigezo muhimu, lakini si kigezo cha moja kwa moja cha kushinda Ballon d'Or.

Kwa upande wa Kylian Mbappé, mshambuliaji huyo alikuwa na msimu bora wa 2025/26, akifunga mabao 25 na kutoa asisti 5 katika mechi 31 za La Liga na kuibuka mfungaji bora wa ligi hiyo. Katika UEFA Champions League, alifunga mabao 15 katika mechi 11 na pia kumaliza akiwa kinara wa ufungaji.

Katika Kombe la Dunia 2026, Mbappé alifunga mabao 10 na kutwaa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu (Golden Boot), huku akiweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa mashindano hayo akiwa na mabao 22.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tangu mwaka 1995, ni wachezaji wanne pekee kati ya saba walioweza kushinda Ballon d'Or baada ya kutwaa Kombe la Dunia, ikiwa ni asilimia 57 pekee. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa ushindi wa Kombe la Dunia haujawa dhamana ya kupata tuzo ya Ballon d'Or.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa ili mchezaji ashinde Ballon d'Or, anapaswa kuwa ndiye aliyekuwa bora zaidi katika msimu mzima wa soka, na si kwa kiwango alichoonyesha kwenye Kombe la Dunia pekee. Waandaaji wa tuzo hiyo wamesisitiza kuwa tathmini huzingatia mchango wa mchezaji katika mashindano yote ya msimu, si mafanikio ya mashindano ya Kombe la Dunia pekee.

Ballon d'Or 2026 Power Rankings:
  1. Lamine Yamal (Barcelona/Hispania)
  2. Harry Kane (Bayern Munich/Uingereza)
  3. Lionel Messi (Inter Miami/Argentina)
  4. Rodri (Manchester City/Hispania)
  5. Ousmane Dembélé (Paris Saint-Germain/Ufaransa)
  6. Kylian Mbappé (Real Madrid/Ufaransa)
  7. Michael Olise (Bayern Munich/Ufaransa)
  8. Jude Bellingham (Real Madrid/Uingereza)
  9. Erling Haaland (Manchester City/Norway)
  10. Khvicha Kvaratskhelia (Paris Saint-Germain/Georgia)
Orodha hii ni makadirio (Power Rankings) yanayoonyesha wachezaji wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kuwania tuzo ya Ballon d'Or 2026 kulingana na kiwango chao katika msimu, na si orodha rasmi ya walioteuliwa.
Sasa Messi anatafuta nini hapa?
 
Ndio, kuwa mfungaji bora tournaments tatu, La Liga, Champions League na WC, na kuwa mfungaji bora wa muda wote WC sio kitu kidogo. Goli 10 tournament moja na goli 21, tournament tatu sio jambo dogo!

Goli 10, WC yenye timu 48, mechi 104, sio jambo dogo. Mpira ni magoli, CR7, Messi amewahi pewa hii tuzo kwa kuongoza tuu ufungaji bora La Liga.
Christiano Ronaldo alikuwa anafunga magoli. Sawa kabisa. Lakini magoli yake yalikuwa yanaibeba Real Madrid katika nyakati ambazo wengi tunasema hapa jamaa hawachomozi.

Ronaldo anafunga goli dhidi ya Juve, Bayern, Atletco na magoli yake yanaamua hatima ya Madrid kushinda mataji, hususani UEFA na pengine La Liga.

Ukimleta kwenye mzani unaona kabisa bila mwamba Madrid isingetoboa pengine. So we see the impact.

Impact ya ufungaji bora wa Mbape ni ipi?

Ni sawa niseme; nimerusha ndoano mara ishirini ila sijanasa samaki hata mmoja. Na mwingine arushe ndoano mara tano aibuke na samaki 20. Nani mvuvi bora?
 
Mchango ulioutoa kwenye timu ndio performance binafsi. Usifanye kama ni vitu viwili tofauti.

Mchango wako binafsi unaweza kuonekana wala haihusiani na timu yako kubeba kombe.

Mfano, striker role yake yeye ni kufunga. Utamuhukumu vipi kwamba hajaweza kuibeba mechi kwenye mechi ambayo alifunga hattrick na timu yake ikafungwa bao 4?
Haya nimekubali, wewe unaona nani anafaa kupewa hii tuzo?
 
Nianivyo Yamal amefanya vizuri kuliko Pedri, hasa kwenye La Liga.
Round hii, maana ya vizuri sio tena kuchukua kombe?

Sasa hiyo maana uliyotumia hapo ndio ambayo tunazungumzia sisi kuwa ilipaswa isimame hiyo kama kigezo cha mwisho.
 
Sawa tuseme siyo kuuchukua kombe.
Mbappe na Harry Kane ndio wanaopaswa kutazamwa kama rivals kwenye hizi tuzo kwasababu namba zao ni top level kuliko hao wengine
Kwa nini unawazungumzia tu washambuliaji? Je, huoni Kuna makipa, mabeki, na viungo waliofanya kazi kubwa?

Ama kwa sababu wewe ni shabiki lialia wa Madrid unatamani sana huyo Mbappe wako apate chochote kitu?
 
Sawa tuseme siyo kuuchukua kombe.

Kwa nini unawazungumzia tu washambuliaji? Je, huoni Kuna makipa, mabeki, na viungo waliofanya kazi kubwa?

Ama kwa sababu wewe ni shabiki lialia wa Madrid unatamani sana huyo Mbappe wako apate chochote kitu?
Kwangu mimi, kipa ni tuzo inayojitegemea.

Mfano Rodri amechukua tuzo ya mchezaji bora (golden ball) lakini pia Unai Simoni naye kachukua tuzo ya Golden glove. Lakini overall ya mchezaji bora wa mashindano ni Rodri.
 
Hapa tunazungumzia mchezaji anayepaswa kuchukua Ballon d'Or. Ambapo mchezaji anayecheza kwenye nafasi yoyote anaweza kuchukua.
 
Hapa ndio mapungufu ya hizi tuzo yalipo.

Kwanini kusiwe na vipengele vinavyo tenganisha kulingana na role ya mchezaji?

Na hapo ukumbuke mpira umebebwa na tukio moja kubwa "magoli"

Yani kutakuwa na fair gani kama mchezaji mwenye magoli mengi na assist akawekwa kwenye mzani sawa na kipa mwenye clean sheets na saves kuwania tuzo moja?

No wonder kwenye historia ya hizo tuzo golikipa mmoja tu ndio aliyewahi kubeba tuzo hiyo. Swali nalojiuliza, hata huo mwaka aliwezaje kubeba hiyo tuzo.
 
Hoja yako kwa kiasi fulani ni nzuri. Hii tuzo inahitaji marekebisho makubwa maana inawanyima nafasi wachezaji wanaocheza katika baadhi ya nafasi ikiwemo goalkeeping (kama ulivyosema) na beki.

Na ukichunguza kwa makini utagundua kuwa wachezaji wanaopewa nafasi kubwa kuitwaa tuzo hii ni wale wanaocheza katika bara la ulaya husasani katika zile ligi tano bora.

Kwa upande mwingine mwaka ambao kombe la dunia linachezwa mara nyingi mtu asiyestahili kushinda hii tuzo hushinda kwa vile tu timu yake imefanya vyema, yaani ni kama mafanikio ya mtu katika kombe la dunia yanaficha yale yote yaliyofanywa kabla ya World Cup.
 
Hata kwa kigezo cha mchezaji kushinda World Cup kuwa ndio anayestahili kuchukua tuzo, bado kipengele hicho kipo vague.

2010 kuna mtu alichukua hiyo tuzo akiwa hajafunga goli hata moja, licha ya timu yake kutolewa kwenye hayo mashindano.

So mimi navyoona wangeacha namba ndio ziamue tuzo iende wapi
 
Ukisema namba tu (magoli) utakuwa unawahalaishia washambuliaji hii tuzo.
 
Mchango ulioutoa kwenye timu ndio performance binafsi. Usifanye kama ni vitu viwili tofauti.

Mchango wako binafsi unaweza kuonekana wala haihusiani na timu yako kubeba kombe.

Mfano, striker role yake yeye ni kufunga. Utamuhukumu vipi kwamba hajaweza kuibeba mechi kwenye mechi ambayo alifunga hattrick na timu yake ikafungwa bao 4?
Mkuu tumekutana tena 😂

Kama tuzo ni suala la kufunga magoli basi kina Lewandowisk, RVP, Suarezi, Harry Kane, Haland, Sarah, Caros Teves wangekuwa wamejaza hizo tuzo.
 
Hata kwa kigezo cha mchezaji kushinda World Cup kuwa ndio anayestahili kuchukua tuzo, bado kipengele hicho kipo vague.

2010 kuna mtu alichukua hiyo tuzo akiwa hajafunga goli hata moja, licha ya timu yake kutolewa kwenye hayo mashindano.

So mimi navyoona wangeacha namba ndio ziamue tuzo iende wapi
Hakuna kigezo kimoja tu kinachoamua, bali muunganiko wa vigezo. Ongeza na interest binafsi za wagawa tuzo (kigezo kisichosemwa).
 
Back
Top Bottom