Kwa kikao cha Copenhagen, vita ya Ukraine na Urusi si ya kuisha leo au kesho

Kumbe wanapeleka misaada nikajua Jeshi, mna peleka US$ 5billion mwenzenu kashikilia US$ 12 trillion.
Hawapeleki hela wanapeleka machuma machuma yanaenda kuunguzwa halafu Urusi anazidi kujimegea utajiri wa matirioni ya dola...

Kinachowauma zaidi mali ambazo wanategemea Ukraine atawakabidhi ili wafidie deni lao zinazidi kunyakuliwa na Urusi.
 
Kwani wew unapomsaidia tajiri wako wa mtaa sindano ya kushonea , yeye hana uwezo was kununua hiyo??? Huo ni kuonyesha hayupo peke yake kama wanavyohisi
 
Nonsense
 
Aya ya mwisho pigia mstari.
 
Hao jamaa hawata kubali, wana hasira sana ya kukatiwa gasi. Kwakifupi hao wazungu ni watu wabinafsi sana. utawezaje kumwekea mtu vikwazo vya kiuchumi wakati huo huo mnategemea sana gesi yake kwa kukuza uchumi wenu
Mkuu, sijui wamechanganyikiwa nini? Ninapo washangaa zaidi ni pale wanapo sema kwamba eti: Putin/Urusi anataka kufanya makosa makubwa atakapo sitisha kusambaza gesi yake kwa mataifa ya Ulaya - wanamshutu Putin kwamba ana lengo la ku-blackmail mataifa ya Ulaya -kichekesho, yaani wao kumunyanyasa Putin wanaona sawa tu,lakini Putin akijibu mapigo wanampigia kelele na kumshutumu kama nini??
 
Mijamaa ni misukule ya marekani na Putin ameletwa na Mungu kuja kuwashitua kwani wanaenda kupigika kiuchumi vibaya sana.
 
Hayo mataifa yote ni wanafiki tu..hakuna mtakatifu hapo..wote wanatetea matumbo yao..kuanzia NewYork, Berlin mpaka Moscow..
 
Mijamaa ni misukule ya marekani na Putin ameletwa na Mungu kuja kuwashitua kwani wanaenda kupigika kiuchumi vibaya sana.

Kinacho shangaza zaidi - inakuwaje viongozi wa Ulaya wenye akili timamu ambao mataifa yao ni huru kabisa, inakuwaje tena wanakubali taifa la Merikani liwaendeshe puta kama gari bovu, wakati wanajua wazi wazi kwamba EU si jimbo la 51 la Merikani - wapo wapo tu, wanaiogopa US kama nini sijui!!

Viongozi wa Ulaya ambao walikuwa majasiri na wenye misimamo thabiti-akina: Angela Merkel na Silvio Berlusconi binadamu tajwa hapo juu walikuwa hawakubaliani na baadhi ya foreign policy za Uncle SAM ambazo ni hatarishi kwa amani Duniani- na kama viongozo hao wa Ulaya wangekuwa bado wapo madarakani nakuhakikishia mgogoro wa Ukraine wala usingefikia hapa ulipo na wala Urusi hisingefikia uhamuzi wa kuchukua hatua za kuhami Taifa lao kwa ku-demilitarize na ku-deNAZI jeshi la Ukraine ambao walikuwa wanatumiwa kwa kificho kui-provoke Urusi kwa lengo kuanzisha a proxy war on behalf of Uncle SAM na hiki ndicho kinacho endelea huko Ukraine.

Watu wengi wanamshutumu Putin bila ya kuangalia a big picture, yaani chanzo/kiini alisi cha mgogoro huu ambao kama viongozi wenye busara na hekima Duniani watashindwa kumuonya vikali Biden kwamba hasichochee vita hii ya Ukraine ambayo kuna uwezekano mkubwa vikawa ndio chanzo cha WW3, lakini viongozi hao wakikaa kimya bila kumshauri vizuri au kumkemea Biden kuhusu hatari ya kulipuka WW3 by miscalculation au kimakusudi watakua wamekosea sana sana.watakuwa wamekosea sana sana. Kwa bahati mbaya sijui kama Biden na wapambe wake hatari hiyo wanaiona au la!!
 
This drawing tells it all
 

Attachments

  • FB_IMG_1657808318087.jpg
    46.8 KB · Views: 4
Hao jamaa hawata kubali, wana hasira sana ya kukatiwa gasi. Kwakifupi hao wazungu ni watu wabinafsi sana. utawezaje kumwekea mtu vikwazo vya kiuchumi wakati huo huo mnategemea sana gesi yake kwa kukuza uchumi wenu
Wataichukua hiyo has kibabe!
Muda utasema
 
Ukrain hata ikipona itanyonywa sana na hao NATO kufidia hizi pesa miaka nenda rudi, ni Kongo ya Ulaya hio.
Watanyonya nn Sasa ndio hiko kinachowauma maeneo mengi muhimu ya madini ,kiliumo na bandari yamechukuliwa na Russians
 
Ni kawaida mbona marekani alipokuwa akienda kupigana na vinchi vidogo kama Iraq na afghanistan japokuwa tunaambiwa na zana hatari za kivita na utaalam bado alihitaji msaada wa UK, France na kama Canada.
Russia pale anapigana na nchi ambayo umesikia zaidi ya nchi 26 zimekutana kuipa msaada wa silaha na mengine.
Yani hapo ukraine ni uwanja wa mapambano tu lakini wapambanaji ni zaidi ya ukraine
 
Wataichukua hiyo has kibabe!
Muda utasema
Hii vita nimeanza kuhisi kuwa huenda itabadili mambo mengi maana nadhani hakuna anayekubali kushindwa. Ikiendelea kwa mufa mrefu zaidi uchumi wa dunia utapata madhara
 
Hao jamaa hawata kubali, wana hasira sana ya kukatiwa gasi. Kwakifupi hao wazungu ni watu wabinafsi sana. utawezaje kumwekea mtu vikwazo vya kiuchumi wakati huo huo mnategemea sana gesi yake kwa kukuza uchumi wenu
Wakati na yeye mrusi anategemea sana kuuza gesi yake kwa wazungu ili apate chochote kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…