Binti Sayuni03
JF-Expert Member
- Jan 21, 2025
- 1,075
- 1,913
Habarini za jioni wana JamiiForums, husika na kichwa tajwa hapo juu.
Leo nilikuwa na safari ya kivukoni/posta, nikaona ni heri niende mbezi nikapande mwendokasi.
Nilifika mbezi mida ya saa9 hivi nikakata tiketi nikasubiri pamoja na abiria wengine kama nusu saa hivi, mpaka dakiki40.
Ikaja gari moja ya mwendokasi nikawauliza wahusika hii inaenda kivukoni, wakanijibu inaishia kimara ukifika pale utaunganishia unapoenda. Nikapanda mimi pamoja na abiria wengine.
Tulivyofika kimara tukaenda moja kwa moja upande wa kusubiria mwendokasi zinazoenda Gerezani na Kivukoni, muda si mrefu ikaja mwendokasi tupu watu tukakimbilia tukapanda halijaandikwa chochote hivyo wanaoenda Gerezani walipanda na sisi wengine wa Kivukoni tukapanda, kufika mbele kabisa ndiyo maandishi yanaanza kusomeka pale juu kuwa gari ni ya Gerezani.
Sijui kama ni sawa hii lakini kwa upande wangu nimechukizwa na hili jambo naahidi sitakaa nipande tena haya magari, yaani unalipa hela yako unahangaika tena kama unaenda bure hapana kwakweli🙌