Kwa kipekee kabisa naipongeza Serikali kwa kuanzisha kodi ya kizalendo kwenye miamala ya simu. Naomba Watanzania tuiunge mkono

Tumekusikia Mwigulu Nchemba. Chezeeni tu kodi zetu lakini siku yaja na haiko mbali sana tutawaadhibu.
 
mafisadi wanaoiba hela wanaachiwa, marais wastaafu wanajengewa mahekalu, wengine wanapewa mabenzi. wote hao tunawachangia sisi. hebu acheni ujinga
 
Kuna Watu mkisha shiba fedha za kodi kwa ubadhirifu wenu huko Serikalini mnakuja kutapika matapishi yenu huku
 
Serikali inakusanya tozo halafu inalipa wahuni wachache kuja kupush ajenda ya wizi mitandaoni.

A failed state
 
Hekoooo!!!!👍👍👍👍👍👍👍

Umewaza kama mimi.

Maza kaupiga mwingi sanaa hapo😂
 
Kama waimba mapambio wengine hana uwezo kabisa wa KUKUELEWA. Hayo mavyeo ya mapambo ni MUHIMU kwenye ushindi wa kulazimisha.
 
Bora ingehalalisha kilimo cha bangi kuliko kodi za dhulumati
 
Uzalendo wa kichwa chako


Hujakosea kusoma wala usishangae, tena ngoja nikariri kabisa

UZALENDO WA KICHWA CHAKO
 
Mkuu unajua unachokiongea lakini! Badala kulalamikia serikali imepandisha tozo wewe unaipongeza.. aisee!
 
Aisee wewe jamaa umenipa hasira... Kwel yaan... Ungekuwa kalbu yangu ningekuzaba hata kofi la baba wa kambo. Yaan kodi zote hzi zilizoongezwa na bdo ww unatetea.
 
Uzalendo upi wa wanasiasa kuibia wananchi kwa nguvu kisha kutakatisha walichoiba kwa kulipana posho?
 
Sawa, endelea kuwapongeza.

Hatutatumia mitandao ya simu kutuma pesa hiyo kodi mtaitolea wapi?

Maana nyinyi kuiweka ni kitu kimoja, na sisi kutumia ili mtukate ni kitu kingine. Watumiaji ndo kama hivi tumeamua kuacha kutumiana hela kwa simu, tumegundua wote tupo mjini hapa hapa, tutaifuata hiyo hela kwa daladala.

Wale wa mikoani tutawatumia kwa basi au kwa bank.

Hii kodi inaenda kuwaacha wazi
 
We bado kijana mdogo hizi stori ukiwa mkubwa utaelewa na utajua kabisa ushenzi ni mwingi kwenye matumizi ya kodi zetu.
Wabunge hawalipi kodi kwenye mishahara yao
Bila shaka hata Rais hakatwi kodi
Mwalimu wa grade IIIA salary ya laki 4 wanakata kodi.
 
Unafiki kiwango cha sgr.
Hivi kwanini huu uzalendo huwa mnaung'ang'aniza kwa watu wa kipato cha chini tu?
 
Mwigulu elimu yake ni ya kuungaunga na hali ni hiyo hiyo kwenye ngazi zote za uongozi ndani ya CCM miaka yote. Unamkuta mtu toka anaanza shule hadi anaingia sekondari ni mweupe kama theluji kichwani . Ghafla bin vuu anaibuka ni daktari , ana PhD na anaitumikia CCM.

Ukifanya utafiti kidogo tu unakuta majina aliyotumia huko nyuma yana utata, elimu anayodai anayo ina utata, sifa alizo nazo zina utata...sasa huo uwezo, hekima na busara atatoa wapi? Akiachana na utumishi ndani ya CCM huyooo ni waziri tena kapewa wizara nyeti kama fedha!

CCM ni kambi ya vilaza na ukiona mtu anakimbilia CCM, ujue tu kuna historia ya mapungufu makubwa kwenye uwezo, elimu, akili na fikra zake kimaisha. Na CCM inawahusudu sana watu wa aina hiyo kwani inajulikana mtaji wa CCM ni ujinga na mtoa mada ni mfano halisi wa hao watu.

Siku Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakapoachana na CCM ndipo itaweza kupiga hatua yoyote ya maana kimaendeleo kwani chama hicho ni dampo la watendaji waliochoka kiakili. Na mathalani bunge sasa limehatamiwa na hao vilaza watupu hatma ya taifa letu iko mashakani.

Adui nambari wani wa taifa ni CCM...



Huyu...yaani huyu huyu!​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…