Kwa kipekee kabisa naipongeza Serikali kwa kuanzisha kodi ya kizalendo kwenye miamala ya simu. Naomba Watanzania tuiunge mkono

Na huku JF kuna watu mmelipwa kuja kupush ajenda?
Hayo ni mawazo yangu binafsi wala sijalipwa chochote mkuu na kama kuna mtu kwa namna moja au nyingine amekwazika na wasilisho langu basi nitumie nafasi hii pia kuomba radhi na kazi iendelee
 
Sipo miongoni mwao mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa na wala sijatumwa na mtu yeyote isipokuwa ni maoni yangu binafsi kuunga mkono kodi ya mshikamano ili kama taifa tuweze kusonga mbele kwa sababu pesa itakayokusanywa kupitia hii kodi kama ambavyo serikali imesisitiza itaenda kusaidia kutatua kama sio kumaliza kabisa changamoto ya bara bara zetu za vijijini. Kwahiyo ndugu watanzania wenzangu tusilalamike kwa sababu kodi hii ina manufaa makubwa kwetu na matunda yake tutakuja tuyaone baadae. Solidarity forever!
 
Naungana na wewe mkuu, saizi serikali ikisema ianze kukamata watu wasiodai risiti na kutoa risiti mbona watajuta?

Kwanza unaweza kushitakiwa kwa uhujumu uchumi au kutozwa adhabu ya Kati ya 1,000,000 hadi 3,000,000 kwa kitendo tu cha kutodai risiti au kutoa risiti.

Mbaya zaidi watu huwa hawajisumbui kudai risiti na wauzaji hawatoi risiti kwa hiyo kodi stahiki ya serikali inapotea kwa kushirikiana Kati ya mnunuzi na muuzaji.

Sasa kwa tozo za miamala na mafuta itafidia haya mapato yanayopotea vinginevyo watu wachague Kati ya zile adhabu na kukatwa kodi za miamala.

Mwisho hii nchi ina watu walalamishi Sana na wasiotaka kuchangia maendeleo,hao hao wanaolia Lia hapa huko mtaani wanakunywa pombe,wanachangia harusi,wanaenda saruni,wanabadili nguo nk hasa watu wa mjini.

Huko Vijijini ambako Serikali inataka kutumia pesa hizi kutoa unafuu kwa watu wa huko eti wa mjini hawataki.. Serikali msisikilize kelele za wapuuzi wachache ni lazima tujenge utamaduni wa kulipa kodi na Kisha tuulizane tija ya kodi zetu.
 
Na bahati nzuri wapiga kelele humu hata huwa hawafuatilii bajeti,, Serikali ilikuawa clear kabisa kwamba wanategemea kukusanya takribani Tilioni 1 kutoka kwenye tozo hizi ambako Kati ya hizo b 600 zinaenda kumtua mama ndoo na zinazobakia zinaenda kujenga madarasa na vituo vya kutolea huduma za afya.

Tozo ya mafuta inaenda kujenga barabara za Vijijini via Tarura sasa kelele za nini?
 
Waangalie namna ya kubalance serikali kupunguza matumizi lakini Kama kila kinachoingia wahuni wanachota, juz bot watu wamechota na hatusikii wakiadhibiwa hela itachukuliwa na bado cha msingi hakitafanyika washenzi tu.
Waliochota si walisimamishwa na PM au? Afu sio kila kinachoenezwa mitandaoni ni sahihi.. wengine ni wahuni wanafanya siasa
 
Ni kweli lakini tozo za mwaka huu zimeelekezwa kwenye specific areas haziingii kwenye matumizi ya jumla ambapo ni rahisi kuzichezea.
 
Hili ni kundi tawala ambapo kokote kule Duniani wanajipendelea..lakini tukikataa wao hawaumii maana Wana magari, watoto wao wanasoma vizuri,wanawatafutia Kazi kwa hiyo sisi wa chini lazima tujichange kwa stahili hiyo
 
Waambieni Wabunge waonyeshe uzalendo Kwanza kwa kukatwa Kodi.
 
Watanzania hatuna dogo mkuu

Watu wanalalamika kulipa kodi lakini wakati huo wanataka nchi ijiendeshe kwa mapato ya ndani.

Serikali ikikopa kutoka nje wanalalamika kwamba nchi inauzwa kwa mabeberu

Tunalalamika kulipa kodi lakini tunataka tulingane na mataifa makubwa kama england, japan, china, USA, canada n.k

Kulipa kodi tunalalamika lakini kwenye kudai maendeleo na huduma za kijamii ni wa kwanza.

Hivi yote haya yatafikiwa vipi kama watu hawako tayari kushikamana kulipa kodi?

Tuache kulalamika watanzania wenzangu, nchi yetu itajengwa na sisi wenyewe
 
Hakuna hela isiyopigwa chini ya utawala wa ccm!! Wananchi tulishapoteza imani kitambo na hawa watawala.
Kwahiyo unashauri nini kifanyike maana ukisema watu wagomee kulipa kodi bado watakaoathirika ni sisi wa hali ya chini kwa sababu ukiuguliwa ukaenda hospitali ukakosa madawa unayeathirika ni wewe hawa wenzako walishajitengenezea brand akiuguliwa nachukua mgonjwa wake anaenda kutibiwa ulaya kwahiyo mambo mengine tujiongeze tu ndugu zangu...Tulipe kodi kwa msitakabali wa maisha yetu na taifa letu
 
Lini ulienda huko hospitali ukakuta dawa? Na ni hospitali gani hiyo!!!
 
Lini ulienda huko hospitali ukakuta dawa? Na ni hospitali gani hiyo!!!
Unamaanisha hospitali zetu zote hazina dawa? Na hao waliolazwa mawodini hadi muda huu wanahudumiwaje kama hamna dawa ?
 
Watu wenye mawazo kama yako ndo wanasababisha waafrika tunaonekana viazi.
 
Mpuuz we
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…