Kwa kipekee kabisa naipongeza Serikali kwa kuanzisha kodi ya kizalendo kwenye miamala ya simu. Naomba Watanzania tuiunge mkono

Una miaka mingapi?... Upo form ngapi?... What is your dream job?... Car?... House?!... Husband?!...

Wewe tujadili haya, mengine yaache
 
Kwa hiyo zile Kodi nyingine tunalipaga huwa zinaenda wapi.
 
Ongezo la makato lipo kwa kiasi cha juu kuanzia miamala ya Tsh 1000 hadi laki 2 hii maana yake ni kwamba,serikali inafahamu fika kuwa wanyonge ndo wanaofanya miamala kusaidia,ndugu,marafiki na jamaa,hivyo tozo kuwa kubwa katika muktadha huo watafikia malengo yao ila sisi wanyonge ndo tunaoumia
 
Mkuu nadhani kuna jambo hauelewi.., Hizi tozo wameziweka bila busara kabisa huenda hii ikasababisha badala ya Serikali kuongeza mapato ikapunguza hayo mapato..., na mbaya zaidi ikaharibu biashara za watu (mawakala na kampuni za simu) na kuongeza kero kwa mtumiaji (in short hakuna mshindi hapa)... kama nilivyoelezea kwa ufupi hapo chini:-

 
Waangalie namna ya kubalance serikali kupunguza matumizi lakini Kama kila kinachoingia wahuni wanachota, juz bot watu wamechota na hatusikii wakiadhibiwa hela itachukuliwa na bado cha msingi hakitafanyika washenzi tu.
Usemalo ni sahihi kabisa. Kodi zikusanywe na zitumike ipasavyo, itumike kwa kuasaidia wananchi, na palengwe hassa pale panapo hitajika, Lakini kwa sisi wa Afrika, sio Tanzania pekee hatuna viongozi wa kusimamia masuala hayo, wao cha kwanza kabisa ni kjijenga wao kwanza, na asilimia kubwa ya hao viongozi si kwamba wanaridhika pale wanapojipatia makazi, usafiri na huduma nzuri kwa famalia zao bali wanataka wajichotee hassa huku wakishinda nani mwenye hela zaidi. Sasa hilo ndio tatizo kubwa sana kwa nchi yetu na nchi nyingi za kiafrika. Ni jambo lakuleta chuki, ingwa kwa Tanzania yetu chuki hiyo bado haijafikia mahala pabaya ya kuleta vita na mauaji, na Mungu atuepushie majanga kama hayo ya vita, heri ushi tu kwa umaskini wako kuliko nchi ikaingia kwenye vita, Lakni tusiache kukemea masuala ya kifisadi na ubadhilifu wa mali za umma.
Kama ulivyo sema watu wanaiba na hawafanyi chochote. Mimi binafsi ningetamani vyama vya upinzani wajikite hassa kwenye suala hili la hao mafisadi kupewa adhabu kali, wange shindikiza serikalin itunge sheria mpya ya na kali kwa wezi wa mali za umma. Enzi za Slaa ndio angalau tulikua tukisikia wakiongelea sana ufisadi lakini sikuhizi naona kimya.
 
unalipa kodi alafu kuna jizi moja linakutwa na mabilioni limeficha nyumbani kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…