Pre GE2025 Kwa kipigo hiki cha CHADEMA, Mbowe achia chama kwa Heche kubadili kabisa aina ya siasa ya kufanya hiyo yako haina matokeo tena na haiaminiki kwa umma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wanapoondolewa wagombea wa upinzani hamuongei yakija matokeo mnakuja Kama wajinga wasiojua kuwa ccm wamepita bila kupingwa?
Kwanini waondolewe ? kama mwenyekiti angekuwa imara haya usinge yaona nakwambia , kuna wakati watu walikuwa imara CCM wakawa hawana la kufanya, wakati ule Dr Getrude Buriani anapigwa chini na Lema pale Arusha unafikiri ilikuwa rahisi HAPANA uongozi kuanzia juu ulikuwa imara sana
 
Wewe udhaifu wa Mbowe huoni? mpaka hapa Chama kina hali mbaya unataka alaumiwe nani? kutoka Chama cha kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni hadi wabunge wa COVID 19 , timu ikishindwa kufanya vizuri anatolewa kocha sio wachezaji, hivyo hivyo ni wakati wa Mbowe kukaa pembeni kuja watu ambao wanaweza kwenda na kasi ya sasa, kuendelea kumkumbatia Mbowe nikujiletea kifo kwenye Chama
 
Hata Mbowe akiachia ngazi hakuna kitakachobadilika kwenye Chaguzi za Kitaifa ikiwa katiba ni ile ile tunayoitegemea ifanye na kusimamia Chaguzi zetu.
 
Huyu Mbowe anawatesa sana. Mmetangaza kifo cha chama chake lakini wamo. Mmewafunga, mmewapiga risasi, mmewapiga matofali, mmewazushia mambo lakini bado hamjiamini kuwa mnaweza kushinda bila mkono wa Mungu! Ni jambo la aibu.

Amandla...
 
Hizi sio zama zile. Hao viongozi imara unaowasema wameisha unga juhudi. Waliobaki ni wakina Mbowe ambao ni wabishi. Na hilo linawasumbua sana.

Amandla...
 
Hizi sio zama zile. Hao viongozi imara unaowasema wameisha unga juhudi. Waliobaki ni wakina Mbowe ambao ni wabishi. Na hilo linawasumbua sana.

Amandla...
Mbowe hana ubishi wowote kwasasa ndio maana Chama kimerudi enzi ya kale, apishe watu wengine walete mawazo mapya
 
Huyu Mbowe anawatesa sana. Mmetangaza kifo cha chama chake lakini wamo. Mmewafunga, mmewapiga risasi, mmewapiga matofali, mmewazushia mambo lakini bado hamjiamini kuwa mnaweza kushinda bila mkono wa Mungu! Ni jambo la aibu.

Amandla...
Wewe unaleta ushabiki , mimi nakupa uhalisia ni wakati sahihi sasa Mbowe kupisha watu wengine kufanya maamuzi juu ya Chama
 
Wewe unaleta ushabiki , mimi nakupa uhalisia ni wakati sahihi sasa Mbowe kupisha watu wengine kufanya maamuzi juu ya Chama
Shabiki ni wewe maana zaidi ya kulalama haujatoa mchango wowote wa maana. Swali ni hao wengine ni wakina nani wakati wote wako pamoja nae! Na hayo mawazo mbadala ni yapi?

Amandla...
 
Ngoja tuone minyukano hii itaishaje
 
Ukitaka uonekane huna akili na mazombi ya Mbowe, wewe sema Mbowe atoke pale kwenye uenyekiti, mimi naungana na wadau wengine muda umefika Mbowe kupisha akili mpya
anzisha chama chako au chenu..uimara wa chadema ni uongoz wa mbowe... uimara wa ccm ni matumizi ya polisi
 
Mbowe bado anahitajika Chadema kwa usalama na uhai wake. Mawakala wa CCM ndio wanataka Mbowe aondoke, asiondoke abaki hadi demokrasia itengemae nchini.
Uzuri ni kwamba, kwenye ushindi wa Serikali za mitaa, je, VAR zilizokuwepo zinaonyesha wazi kosa liko ndani ya 18 au nje ya box? Kama zimeonyesha sahihi, basi yawezekana ni kama kamera za Azam kwenye ligi kuu. Hazinaga ushawishi kwa refa
 
Mbuzi hawezi pata ushindi mahakama ya fisi,wanatia aibu kwa taifa
 
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…