Kwa kizazi hiki inawezekana kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu?

Kwa kizazi hiki inawezekana kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu?

Haya mambo yalikuwepo toka kitambo tu,sema vijana wa siku hizi hawajui kutunza siri,

Ushahidi upo hata humu JF mtu hata akikutana na mdada wa JF tu nje ya JF anakuja kumfungulia uzi,

Zamani watoto wa nje ya ndoa walijulikana pale anapofariki Baba yao,pia maradhi hayakua mengi,

Sababu nyingine,wakati huu ni wakati wa utandawazi,mambo yamekua rahisi sana kupata mwingine muda wowote ule,ni hela yako tu.
Tunajaribu kuona kama itawezekana
 
Hili ni suala mtambuka, yaani HALITATULIKI.

Sisi ni wanyama, njaa, kiu na ngono lazima vituendeshe kama wanyama wengine.
Sisis ni binadamu.tumepewa ufahamu tofauti na wanyama

Ni kweli suala halitatuliki lakini Kuna namna tunaweza fanya kuepusha madhara Kwa wengine tukiona haiepukiki.na tukiongozwa na huo ufahamu tuliopewa.
 
Mungu atusaidie kizazi hiki hali ni mbaya. Kuna muda unajiuliza tofauti ya sodoma na gomora na kizazi hiki iko wapi?

1. Wanaume kuwa mashoga imekuwa jambo la kawaida (wanajiuza mpaka kwenye mitandao) na wateja ni wengi tu.
2. Kuingiliana au kuwaingilia wanawake kinyume na maumbile imekuwa kawaida na watu hawaogopi kabisa
3. Kuchepuka ndio usiseme (hata wew umeliona)
4. Watu kufanya mapenzi kwa makundi bila hata haya imekuwa kawaida wanaita 'threesome'

Mungu anaweza kukichoma hiki kizazi hata kabla ya siku ya mwisho sababu yaliyokuwa yanafanyika sodoma na gomora hata sasa yanafanyika. Tuna sababu ipi ya kutopata adhabu kama ya watu wa sodoma na gomora??
 
Ni possible kabisa, wapo watu safi na wema , changamoto is wapo wachache, na demand yao ni kubwa
Na pia ni namna mioyo inavyomungana.muaminifu anaungana kipanga,mwaminifu mwingine anaungana na mwaminifu.hiyo ya kwanza lazima alie mtu
 
Kwamba zamani yaani kizazi kile ndio haya mambo hayakutokea ? Sema tu sasa hivi na wanawake wamejiunga kwenye game kwa uzaidi ila kwa wanaume hii itakuwa ni muendelezo tu..., kwanza wengine hata Imani zao zinawaruhusu....
 
Waaminifu wapo na wahuni wapo. Na yeyote hapo anaweza akahama kundi mda wowote.

Kama haya unayaona live sio mtandaoni badilisha circle ya watu wako, unaweza ukahisi ndivyo dunia ilivyo. Kumbe kuna waaminifu wengi tu.
 
Back
Top Bottom